Monday, May 26, 2008

Maswali Bungeni 26/5/2008

1. Kwa kuwa ni muda mrefu sasa ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi Kambi ya Finya, umesimama na kwa kuwa nyumba za makazi ya polisi zilizopo police line Wete ni mbovu sana, zimechakaa na zinavuja mno wakati wa mvua hali ambayo inasababisha usumbufu mkubwa na kuhatarisha usalama kwa familia zinazoishi humo na kwa kuwa polisi wengi na hasa wa vyeo vya chini wana ari ya kujenga nyumba binafsi za kuishi lakini kipato chao ni kidogo:-

(a) Je, Serikali itamalizia lini ujenzi wa nyumba za polisi Kambi ya Finya?

(b) Je, ni lini Serikali itazifanyia matengenezo nyumba za Police Line ili ziwe na hali nzuri?

(c) Je, Serikali haiwezi kuwasiliana na taasisi za fedha nchini ili polisi wapatiwe mikopo ya kujenga nyumba zao za binafsi?

bonyeza hapa kwa- majibu

2. Kwa kuwa, Wananchi wa Mji wa Mererani wanajishughulisha na biashara na uchimbaji wa madini ya Tanzanite, lakini wamekuwa wakipata taabu ya barabara kati ya Mererani na KIA; na kwa kuwa Rais wa Awamu ya Tatu na Awamu ya Nne walipoiona hali hiyo ngumu waliahidi kujenga barabara hiyo isiyozidi kilomita 20 kwa kiwango cha lami:- Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kujenga barabara hiyo muhimu sana kiuchumi, kutimzia ahadi zilizotolewa na Ma-Rais hao.

Jibu kutoka kwa Mh. Celina Ompeshi Kombani REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT

NAIBU WAZIRI alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, napenda kujibu Swali la Mheshimiwa Chrisopher Ole-Sendeka Mbunge wa Simanjiro kama ifuatavyo. Majibu


3. Kwa kuwa Serikali ina mikakati mizuri ya kuwawezesha wananchi hususan wanawake kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwapatia mikopo ya kufanyia biashara ndogo ndogo; na kwa kuwa Mkoa mpya wa Manyara una matatizo mengi makubwa ya mazingira ya kufanyia biashara hizo ikiwa ni pamoja na elimu ya ufahamu, kero za maji, uhaba wa Zahanati kwa baadhi ya vijiji na kutokuwepo na hospitali ya Mkoa.

(a) Je, Serikali ina mipango gani ya upendeleo kwa Mkoa wa Manyara ya kuboresha Mazingira chini ya Mpango wa MKUMBITA?

(b) Je, Serikali itafikisha lini mradi wa SELF Mkoani Manyara ikizingatiwa kuwa hakuna taasisi za fedha zinazofikisha huduma huko zaidi ya SACCOS zilizoanza hivi karibuni?

Jibu kutoka kwa Mh. Dr. Batilda Salha Burian PLANNING, ECONOMY AND EMPOWERMENT

NAIBU WAZIRI alijibu: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Martha Umbulla, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- Majibu

Maswali na Majibu Bungeni 26/5/2008

Swali

Kwa kuwa muda mrefu sasa, wananchi waishio Londrosi West Kilimanjaro katika Wilaya ya Siha, wamekuwa wakitaabika kutokana na ubovu wa barabara itokayo Ngare Nairobi Londrosi Gate; na kwa kuwa ubovu huo unakwamisha shughuli za kiuchumi hasa kwa upande wa watalii wanaotaka kupanda Mlima Kilimanjaro:-



(a) Je, ni Mamlaka gani inayotakiwa kushughulikia barabara hiyo?



(b) Je, ni hatua gani zinachukuliwa na Serikali kurekebisha hali hiyo?


ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION
Answer From Hon. Dr. Milton Makongoro Mahanga INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Aggrey D. J. Mwanri, Mbunge wa Siha, lenye sehemu (a) na (b), kwa pamoja kama ifuatavyo:-


Mheshimiwa Spika, barabara ya Ngare Nairobi - Londrosi Gate inashughulikiwa na Mamlaka mbili tofauti; sehemu ya Ngare Nairobi hadi Simba Farm yenye urefu wa kilomita 1.5 kwa upande moja ambayo ni barabara ya Mkoa (Sanyajuu – Kimwanga) iko chini ya uangalizi wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Kilimanjaro na kwa upande mwingine, barabara itokayo Simba Farm – Londrosi Gate yenye urefu wa kilomita 10, iko chini ya uangalizi wa KINAPA na kampuni ya West Kilimanjaro.


Bonyeza hapa - Muendelezo wa majibu

JK aenda japani leo:

Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka nchini leo jioni (25 Mei, 0 kuelekea Japan kuhudhuria mkutano wa nne unaohusu maendeleo ya Afrika, ujulikanao kama Tokyo International Conference on African Development (TICAD) utakaofanyika katika jiji la Yokohama.

Kabla ya kuhudhuria mkutano huo, Rais Kikwete atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Yasuo Fukuda, tarehe 27 Mei, 08 kuzungumzia mahusiano na ushirikiano wa nchi mbili hizi katika maswala ya kiuchumi na kidiplomasia na pia kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Kikwete anatarajiwa kumweleza mwenyeji wake juu ya maendeleo na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika na kujadili utatuzi wake.

Japan ni mshirika mkubwa wa maendeleo ya Tanzania ambapo Japan ni moja ya nchi zinazoisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuchangia katika bajeti na pia imechangia katika misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula, barabara na maji.

Mkutano wa nne wa TICAD utaanza tarehe 28-30 Mei, ambapo viongozi wote wa bara la Afrika wamealikwa kuhudhuria pamoja na viongozi wa Japan, wakuu wa mashirika mbalimbali ya kimataifa duniani kama vile Umoja wa Mataifa, mashirika ya fedha duniani, taasisi sizizo za kiserikali kutoka bara la Asia na Afrika, nchi rafiki na wenza katika maendeleo duniani.

Mbali na mkutano wa TICAD Rais pia atashiriki mikutano na makongamano mbalimbali yanayohusu uchumi, miundo mbinu, maendeleo na maswala mbalimbali yanayohusu utunzaji wa mazingira barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Aidha Rais Kikwete ataongoza mkutano utakaojadili tatizo la chakula duniani ambapo atazungumzia swala hili kwa kina hususan katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo barani Afrika na hatimaye atashiriki katika kupitisha azimio la Yokohama.

Rais pia anatarajia kutumia nafasi hiyo kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Afrika watakaohudhuria mkutano huo.

Rais atafuatana na

  1. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Benard Membe,
  2. Waziri wa Fedha - Mhe. Mustapha Mkulo,
  3. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Zanzibar - Mhe. Haroun Suleiman,
  4. Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko - Mhe. Cyril Chami
  5. na Mbunge wa Muleba Kusini
  6. na Mwenyekiti wa Kamati Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama - Mhe. Wilson Masilingi.

Rais anatarajiwa kurejea Dar-es-Salaam tarehe 31 Mei, 2008.

Imetolewa na Ikulu-Dar-es-salaam25.05.08

Wednesday, May 21, 2008

Balali ameaga dunia


Jamani kama Mungu anatusamehe kila inapoitwa leo naomba na sisi tumsamehe aliyekuwa Governor wa BOT (David Balali)


Mzee Daudi Balali (pichani) amefariki, (soma Jamii Forums) na mazishi yake yatakuwa Washington D.C. hapa Marekani!


Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema poponi Ameni.

Tuesday, May 20, 2008

Lipo tatizo la msingi ambalo sisi kama Watanzania au Waafrika tumegoma kabisa kulipa mjadala wa kina. Tunaogopa kabisa kuligusa kwa sababu ambazo kimsingi nilikwishazijadili huko nyuma.

Tatizo ni kwamba nchi hii haina misingi ya kile inachokiamini kwa dhati ambacho watu wake wanaweza kukipigania hata kama watakufa wakiwa wanakipigania. Msingi mkuu sasa hivi ni pesa. Kila mtu anapigania tumbo lake na la watoto wake.

Na kutokana na mlolongo wa matukio, na pia ukweli nilioueleza hapo juu ninaweza kabisa kuvaa joho la Sheikh Yahya Hussein na kutabiri kwa hakika kwamba kabla mwaka huu au kipindi hiki cha kwanza cha Rais Kikwete hakijafika ukingoni basi kutakuwa kumetokea mabadiliko zaidi katika Serikali.

Bonyeza hapa

Kweli Tanzania Haina Amani? (Hebu kuweni wakweli jamani)



Tanzania tuna Amani jamani.

Unajua ukiongelea ishu ya UFISADI Dunia nzima ni mafisadi na tanzania tunaichukulia mzaha mzaha ndio maana ishu inakwenda inarudi na tanzania tatizo sisi ni masikini ndio maana tuna pigana na Vijisenti alafu na wanoiba wanaiba nyingi kwa wakati mmoja badala ya kuiba kidogo kidogo.


Mna lolote la kuchangia wadau?

Hoja hiyo Mezani................................Kazi kwenu



Wananchi Africa Kusini waua Wageni Nchini Mwao





MMalawi akiokolewa na Polisi!


Leo kuna habari ya fujo zilizotokea huko Afrika Kusini. Wanasema kuwa wananchi wenye hasira wanaua wageni/wahamiaji kutoka nchi zingine amboa wako kwao. Mpaka sasa watu 22 wameuliwa. Kisa eti ni chanzo cha wao kukosa kazi! Wengi ya waliouliwa wanatoka nchi za kiafrika kama Zimbabwe, Mozambique na Malawi.

Wageni huko wanakimbilia vituo vya polisi na makanisani kuomba hifadhi kusudi wasiuliwe.Hivi Afrika Kusini imelaaniwa nini? Watu ni wepesi kusahau. Miaka mingapi Tanzania na nchi nyingi za dunia ziliwasaidia waAfrika Kusini mpaka walivyopata Uhuru wao.


Mnakumbuka Mwalimu Nyerere alivyozuia timu ya Olympiki ya Tanzania kushiriki katika michezo kwa vile Wazungu kutoka Afrika Kusini walikuwa wanashiriki wakati weusi huko wananyanyaswa na Apartheid? Mnakumbuka Dakawa na Mzimbo huko Morogoro? Na tusisahau hao WaSouth Africa walioacha mbegu Bongo!Hebu tukumbuke ni MSouth Africa aliyesababisha ajali iliyotoa roho mpendwa Waziri Mkuu wetu, Edward Moringe Sokoine! Na yule jamaa yuko wapi?

Je, ni moja wa hao wanaotaka kuona waBongo huko wanauliwa!Askofu Desmond Tutu amewaomba waache kuua watoto wa watu waliowasaidia kutoka kwenye mikono ya Apartheid. Ni aibu!



BBC Yaongeza muda

BBC Yaongeza muda kwa vijana wafanyabiasharaTarehe ya mwisho ya kuwasilisha michanganuo sasa ni Ijumaa Mei 23.

Vinaja wanaowania kushiriki katika shindano la Faidika na BBC sasa wana muda zaidi hadi Ijumaa Mei 23 kuwasislisha michanganuo yao.

Vijana wenye umri kati ya miaka 16 hadi 24 wana wiki moja zaidi ya kuwaslisha mchanganuo unakaonufaisha jamii yao kwa kutumia zawadi yenye thamani ya dola Elfu Tano za Marekani.

Mchanganuo usizidi maneno 1,500,
lugha ni Kiswahili.

Unaweza kusikia maelezo zaidi ya jinsi ya kuandika mchanganuo bora katika matangazo ya Dira ya Dunia kila siku kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC na pia kwenye mtandao wetu bbcswahili.com.

Salim Kikeke, Meneja Mradi wa Fadika na BBC 2008, amesema “ Vijana wametuambia wanahitaji muda zaidi kufanyia kazi kile ambacho huenda kikabadili kabisa maisha yao, ndio maana tumeamua kuongeza wiki moja katika tarehe ya mwisho ya kupokea michanganuo”.

Michanganuo inaweza kutumwa kwa njia ya:
E-Mail kwa: faidika@bbc.co.uk,
au kutumwa kwa njia ya posta katika ofisi zetu za kanda.
Faidika na BBC 2008,
Building Maison de la Bible,
Avenue de la Mission,
2eme etage,
En face de PAR,
Bujumbura.

Tanzania
Faidika na BBC 2008,
Jengo la PPF,
Ghorofa ya 8,
Barabara ya Sokoine na Morogoro,
P O Box 79545, Dar es Salaam.

Uganda
Faidika na BBC 2008,
1A, Ruth Towers,Plot 15A,
Clement Hill Road,
P O Box 7620, Kampala.

Michuano ya kitaifa itafanyika kama ifuatavyo: Burundi, Jumatatu Juni 2; Rwanda na DRC, Jumanne Juni 3; Tanzania, Jumatano, Juni 4; Kenya, Ahamisi Juni 5, na Uganda Ijumaa Juni 6.

Washindi sita kutoka katika michuano ya kitaifa, watapambana kuwania zawadi ya kwanza, katika fainali itakayofanyika Uganda, Jumatano Juni 18. Fainali itatangazwa moja kwa moja kupitia Idhaa ya Kiswahili ya BBC na pia kwenye mtandao, katika bbcswahili.com

UFISADI: Viongozi wameiweka CCM kwenye Auto-Pilot?



WENGI wetu tunafahamu kwamba ndege kubwa ya abiria inayosafiri masafa marefu, mathalan London hadi New York, kuna wakati rubani hutegesha mitambo ili ijiendeshe yenyewe (Automatic Pilot).

Kwa kawaida rubani na msaidizi wake hufanya hivyo ili nao wapate nafasi ya kunyoosha miguu, kunywa kahawa au hata kwenda maliwatoni.

Lakini si kila safari unaweza kuiweka ndege katika Auto-Pilot. Ni shurti safari iwe ya masafa marefu.

Aidha, ndege haiwezi kuwekwa Auto-Pilot kabla rubani hajaielekeza mambo fulani fulani; kama vile kule anakotaka ielekee, iende kasi gani na iruke umbali gani kutoka usawa wa bahari.

Kwa habari zaidi bonyeza hapa

Tsvangirai afuta mpango wa kurudi Zimbabwe kutokana na njama ya kutaka kumuuwa.



Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai.

Hofu za njama ya mauaji dhidi ya kiongozi wa upinzani Zimbabwe imechelewesha kurudi kwake nchini humo kulikokuwa kukisubiriwa kabla ya marudio ya uchaguzi dhidi ya Rais Robert Mugabe hapo tarehe 27 mwezi wa Juni.

Baada ya kuwepo nje kwa zaidi ya mwezi mmoja Morgan Tsvangirai alikuwa akitarajiwa kurudi nyumbani leo hii lakini amebadili mipango dakika ya mwisho baada ya kudokezwa juu ya jaribio la kutaka kumuuwa.

Msemaji wa kiongozi huyo George Sibotshiwe amesema wamepokea habari kutoka duru za kuaminika asubuhi hii ya kuwepo kwa mpango wa kumuuwa Tsvangirai. Msemaji huyo anasema kwa hivi sasa hawawezi kusema iwapo mpango huo umeungwa mkono na serikali na habari hizo tayari wamezifikisha kwa wakuu wengine wa nchi na kwamba ni jambo la uhakika kusema kuna ni tishio zito dhidi ya maisha yake na wanaamini kutokana na ushauri wa wanausalama wao isingelikuwa jambo la busara kwa Tsvangirai kwenda Zimbabwe leo hii.

Tsvangirai ambaye mwishoni mwa juma lililopita alisema angelirudi Zimbabwe hivi karibuni alitowa madai kadhaa ya kutaka kuhakikishwa maradio ya uchaguzi huo yanakuwa huru na wa haki ikiwa ni pamoja na kupelekwa nchini humo kwa wanajeshi wa kulinda amani wa kigeni na waangalizi wa uchaguzi.
Mohamed Dahman

Whose hands it's in....

As you see now, it depends whose hands it's in. So put your concerns, your worries, your fears, your hopes, your dreams, your families and your relationships in God's hands because... It depends whose hands it's in.

This message is now in YOUR hands.


What will YOU do with it?



It Depends on WHOSE Hands it's in!

Monday, May 19, 2008

VIJANA MNATUPELEKA WAPI?

Leo katika pita pita zangu nilinasa sehemu Fulani katika foleni eneo la ilala , tulikaa pale kwa muda mrefu kidogo karibu dakika 20 , magari hayaendi huku au kule , pembeni yetu kulikuwa na vijana wamepanda nyuma ya pick up , mbele yao wakina mama wako katika basi wanaenda katika msiba .

Ghafla hawa vijana wakaanza kuimba Nambari wani eehh nambari wani ni CCM , si mnaona sasa , mikanga yenu mliyopewa hiyo wakati ule ? angalia sasa hii ndio barabara waliyoahidi , rudisheni mikanga yenu hii ndio CCM iliyowapa mikanga hiyo mkawachagua .

Wale wakina mama hawakuwa na jibu lolote , lakini walikuwa wanaogopa sana manake vijana walikuwa na hasira walikaribia mpaka kushuka katika gari walilopanda wao waende kwa wale wakina mama waliovaa zile kanga .

Hawa ni mfano wa vijana ambao kwa siku za karibuni wameonekana kulaumu chama cha mapinduzi na serikali kwa ujumla wakiona chochote mbele yao , nilitaka kuwauliza hivi ccm inahusika nini na mkandarasi aliyejenga barabara hiyo ? au ccm ndio walikagua barabara hiyo kabla yaijakabidhiwa ? yote hayo ni maswali ambayo nilitaka kuuliza .

Ni sawa na wale vijana wengine waliotiwa nguvuni kwa tuhuma za kumzomea raisi mstaafu Benjamin William mkapa kwa sababu zao binafsi , au sijui hawa vijana wanalipwa au wanapewa kitu gani mpaka wanakuwa na ujasiri wa kudhalilisha wenzao kiasi hicho .

Tabia hizi kwa kweli zinauzi na kukatisha tamaa sana , kama vijana wa leo ambao tunategemea wawe mstari wa mbele katika kujenga jamii bora zinazoangalia mbele kuanza kuzomeana njiani , kuimba nyimbo za ajabu ajabu , kuandamana katika mavyuo na mashuleni sijui kuchoma moto na kufanya vurugu nyingine .

Kwa mtindo huu vijana wasitegemee kufika popote au kusikilizwa na mtu wowote , kama mawazo yao ni kuungwa mkono na vyama vya upinzani kama wale wananchi wa tabata dampo basi watafute mengine na kama kuzomea huku , au kuimba nyimbo za kashfa hizi zinafadhiliwa na upinzani au mtu wowote yule

Waelewe nyimbo hizo na aina nyingine zozote za vitu wanavyofanya ni kuvunja sheria za jamhuri ya muugano wa Tanzania , na sheria ina mkono mrefu itakufuata popote ulipo na kukufikisha katika vyombo husika ili uweze kujibu tuhuma zinazokukabili

Vijana sasa wafanye mengine kuna mengi ya kufanya zaidi ya kuzomea , kuimba nyimbo za kashfa , kuchoma moto shule , kufanya fujo mashuleni na sehemu zingine .

Ni ushauri kutoka kwa kaka Yona Maro

UFISADI NHIF

Jamani wadau nasikia kuna ufisadi ndani ya NHIF,

  1. Mgongano wa Kimaslahi na “Hongo” kwa viongozi wa Bodi na Wizara ya Afya
  2. Kupindisha taratibu maksudi kwa maslahi Binafsi
  3. Ufujaji wa fedha
  4. Huduma Mbovu za Mfuko
  5. Dharau na Mienendo isiyokubalika katika jamii
Je mnalolote la kuongelea juu ya huu UFISADI

Wednesday, May 14, 2008

KANUNI YA BUNGE INAYOMPA NGUVU MWANANCHI (JAPO HAITUMIKI)

Hapa chini nakuleteeni nukuu ya kanuni moja ya Bunge kama ilivyowasilishwa na Dkt. Wilbroad Slaa, hivi majuzi (Mei 2, 2008) kwenye mdahalo wa ulingo wa maendeleo hapa mjini Arusha.

Kanuni ya 34 ya Kanuni za Bunge inatoa nafasi adimu sana ambayo katika Bunge letu haijawahi kutumika tangu uhuru kwa vile si Wabunge au Wananchi wanaoielewa vizuri kanuni hii. Kanuni hii inatamka ifuatavyo, Mbunge yeyote anaweza kuwasilisha Bungeni maombi kuhusu jambo lolote kwa niaba ya watu wanaotoa ombi hilo Ombi la aina hii linachukua nafasi kubwa Bungeni, na linachukua nafasi precedence kuliko hata shughuli za Serikali. Matakwa pekee ni kuwa lazima liwe limewekewa saini na Wananchi (Wasiopungua 200) wenye kutaka ombi hilo liwasilishwe, na mbunge asiwe na maslahi yoyote na ombi hilo yeye mwenyewe. Hii ni nafasi muhimu sana, kama ingeliweza kutumika. Inahitaji uelewa mkubwa, ujasiri wa wananchi na wananchi kutokuwa na uwoga katika kutafuta na kudai haki zao.

Je, hapo hapawezi kuwa mahali pa kuingilia ikizingatiwa hii ni kanuni ya Bunge, si ya chama chochote? Je tuendelee kungoja utashi wa wabunge kuwasilisha hoja binafsi? Je inatosha wananchi waendelee kuwalaumu wabunge kwamba hawasikilizi kero zao?

Dkt. Slaa anasema, Inahitaji uelewa mkubwa.
Nani atawajengea uelewa mkubwa wananchi? Mimi nimekutumia wewe mbiu hii (bila kujali iwapo unajua au la), ni vema ukiimuvuzisha zaidiĆ¢.

Tuesday, April 29, 2008

Mwalionaje hili tukio? (Hivi Kweli kuna wachawi?)

Kijana Ramadhani Mussa (18) ambaye amekamatwa na kichwa cha mtoto mwenzie na kuanza kukinyoya damu hadharani pale kwenye lango la Hosptali ya Taifa Muhimbili, alishawahi kukutwa kwenye makanisa kadhaa ya jijini Dar es salaam akidai kudondoka na ungo na kisha kuombewa na wachungaji wa makanisa hayo, lakini mara ya mwisho alionekana ni kijana tapeli tu au wachungaji waliokuwa wakimuombea walikuwa wanafanya usanii kuvutia 'wauimini'!
Awali mtoto huyu inadaiwa alikutwa usiku wa manane kwenye Kanisa la Kilutheran pale Manzese na kuombewa na Mchungaji Jonathan wa Kanisa hilo baada ya kudai kuwa amedondoshwa na wachawi wakiwa kwenye ungo, ingawa waumini wengine walimuona kijana huyo kama mchawi na kutaka kumpiga.

Baadae inadaiwa alipelekwa Hospitali ya Mwananyamala ambako nako alitoweka kimiujiza, kabla ya kukutwa kwenye kanisa lingine Tabata na hatimaye Mikocheni kwa Mchungaji Rwakatare ambako ndiko alipoombewa akiwa na mwenzake kwa muda kabla ya kuambiwa kuwa ni 'matapeli' kwani hizo ndizo zao kujifanya wamedondoka kwenye ungo na kuibukia Makanisani ili kujipatia pesa!
Akiongea na kituo cha ITV jana, Mchungaji Rwakatare, ambaye pia ni Mbunge wa CCM wa kuteuliwa, alisema "Mungu amejitetea mwenyewe" kwa kuonesha kuwa walichokuwa wanakisema kuwa watoto hao walikuwa na mapepo hawakuwa wanaongopa.
"Laiti kama wangewaachia wawaombee, yule mtoto asingekufa wala yasingetokea yaliyotokea, lakini kwa sababu kuna watu wanajaribu kuwa kama Mungu, ndiyo maana haya yote yanatokea!
"Wamuache Mungu awe Mungu", alisema Mchungaji Rwakatare na katika hili inaoenekana mtumishi huyu wa Bwana amejipatia 'tano' zingine!






Haya ni maoni ya ndugu Baha.
Binafsi anadhani hili suala linapaswa kutazamwa katika mapana na mazingira yake,kwa ufupi tumezoea kusikia wachawi wa aina ya huyo mtoto wakila nyama za maiti makaburini ingawa haijawahi kudhibitishwa, wakichukua watu kichawi na kuwapoteza lakini si kwa staili aliyochukuliwa huyu mtoto,huyu alitekwa akajichwa kiwiliwili kikatupwa chooni na kichwa akaondoka nacho huyo mtoto na huko anadai kwamba nyama nyingine wenzake wanaendelea kula!!iweje kikutwe kiwiliwili kama wenzie wapo kweli?na walikuwa wanakula? Hapa jeshi la polisi ikiwezekana kutumia staili ya Abu Ghraib ama hata Guantanamo bay kumhoji huyu mtuhumiwa namba moja nadhani hiyo ifanyike!mara nyingine inabidi tusahau kidogo kuhusu human right ya baadhi ya binadamu! yes apate kibano cha nguvu kama ni kichaa kimtoke na kama ni mashetani yapate adabu yake then atueleze kisa cha kuondoa uhai wa mtoto mzuri kama yule asiyejua hili wala lile!na hao akina Lwakatare na walokole wenzie waendeshe hizo sara basi tuondokane na aina hiyo ya watu!hasa mzizi akina Elizabeth na Kichaka kama anavyodai Sheikh Yahya.Ama hii ni mbinu ya mafisadi kutusahaulisha kwamba kuna EPA, RICHMOND<>

WAJUE MAFISADI NA UOZO WALIOFANYA

FAHAMU UKWELI WA NCHI YAKO KWA MANUFAA YAKO, TAIFA NA JAMII YAKO!!..
Huyu muiran anataka kutwambia nini:Check haya madudu yanayofanyika.
(1). Tanzania ni nchi yenye rasimali na utajiri wa hali ya juu Africa na ulimwenguni, lakini ni masikini ya kutupwa kwa kiwango cha nafasi ya tatu kwa umasikini duniani kwani nyie viongozi wa ngazi za juu mnaleana kukumbatia ufisadi na mafisadi mufilisi ambayo nitayataja leo kwa ufisadi wake

(2). Utajiri wa rasilimali zinazoporwa na mafisadi ulionao zingeweza kufanya mambo makubwa na mazuri yafuatayo:
(i) Kusomesha Watanzania wote bure kuanzia Chekechea hadi kiwango cha PhD
(ii) Kuwalipa posho Watanzania wasio na ajira kila mwezi kama yanavyofanya mataifa yenye utajiri kama wetu
(iii) Kuwa na kilimo na mifugo bora na endelevu yenye kuingiza zaidi ya 60% ya pato la taifa kuliko sasa ambapo sekta hiyo inachangia 12% tu ya pato la taifa kutokana na kuhujumiwa na mafisadi wafanyabiashara kwa manufaa binafisi kma Wasira na Diallo
(iv) Kuwa na matibabu bure kwa kila mtanznia kwani kodi wanazotozwa wafanyakazi, wafanyabiashara na wakulima ni kubwa mno. Pia zaidi ya 90% ya pato la taifa inaporwa na mafisadi uliowaweka katika ngazi ya uwaziri, makatibu wakuu na kurugenzi mbalimbali kote nchini zikiwamo halimashauri
(v)Kuwa na viwanda vikubwa, vya kisasa vyenye kuingizia taifa zaidi ya 46% ya pato la taifa. Lakini cha kushangaza serikali imefunga ndoa na kunguruwaporaji wa uchumi wa kihindi na Kiarabu kama Jeetu P, Chavda na R. Aziz
(vi) Tanzania ingekuwa ni kisiwa cha uzuri na mandhari murua ya maendeleo ya kuja kujifunizia matifa mbalimbali ulimwenguni lakini cha ajabu ndiyo imekuwa jalala la kila nyanja ya umasikini(vii) Ndugu Kikwete, pamoja na kwamba Mafisadi lowassa, karamagi na msabaha wameshaachia ngazi, bado kuna mafisadi wengine uliowakumbatia na kuwaweka karibu na wewe huku wakiifilisi nchi kama mafisi ya kienyeji ni hawa wafuatao:
Zakhia Meghji:-
(A) aligawa holela vitalu vya uwindaji akaipotezea Tanzania Tsh 3,304, 903,050/- akiwa waziri wa Mali Asili na Utalii.Ovyo zaidi hata wanafamilia wake walijiingiza katika ufisadi huo kwa kumiliki baadhi ya vitalu kibadhilifu
(B) Alipotosha ripoti ya mkaguzi wa BOT mwaka 2005/2006
(C) Kuchonga bajeti angamizi ya mwaka 2007/2008
(D) Kuidhinisha matumizi mabovu zaidi ya millioni 143 kwa mawaziri mafisadi kwenda kuifagilia bajeti ya kihuni ya 2007/2008 mikoani. Mafisadi hao hawakusita kukomba millioni 143 Tsh kwenda kuzomewa mikoani.
(E) Kufumbia macho shughuli fisadi na za kitaprli za BOT ambayo iliipatia Tangold ltd Kampuni feki kiasi zaidi ya Sh 37.7 billioni ambayo haikuwa na usajiri wowote, akidanganya kuwa ni matumizi nyeti ya serikali kumbe ni ulaji wake na vigogo wenzake
(F) Kubarikli uporaji wa fedha BOT tsh 18,465,755,495.39/- zilizopelekwa kwenye makampuni mbalimbali feki kuanzia decemba 2005 hadi 2007.

Benjamini Mkapa:
(A) Kufanya biashara akiwa ikulu ambacho ni kinyume kabisa na katiba ya nchi yetu
(B) Kuanzisha makampuni mufilisi akiwa ikulu ambayo yamelipora taifa zaidi ya Tsh 908,798,045,050/- akiwa ikulu hadi leo kwa makampuni ya kihuni kama ANBEN ltd, Fosnik ltd na Tanpower
(C) Wizi wa zaidi ya Tsh Trillioni 8,86 BOT kwenye kampeini za uraisi na ubunge zilizotuwekea rais mufilisi. Mkapa anatakiwa asimame kuelekea kizimbani na kujibu wizi huo ulioifilisi nchi ikawa kama dampo la umasikini
(D) Uporaji fedha za taia hili kupitia ununuzi wa rada feki Tsh 50 billioni ambayo aliishupalia kama ruba
(E) Uuzwaji angamizi wa mashirika ya umma na viwanda kwa hila zote, kwani hata yale yaliyokuwa yakijiendesha kwa faida kubwa yaliuzwa kwa bei ya tupatupa (throw away prices) (F) Kushiriki mikataba mibovu ya madini alilipotezea taifa zaidi ya Tsh 959,588,789,005/- kwa kipindi chote Hivyo huyu ni fisadi lililokubuhu.

Edward Lowassa
(A) Anahusika moja kwa moja na ufisadi kupitia kampuni haramu ya RICHMOND na shoga wake DOWANS ambao wamelipora taifa zaidi y ash billioni 273/- kwa umeme hewa
(B) Upotevu wa sh millioni 12.5 /- kupitia kampuni feki ya Water City ambayo aliibariki licha ya kuambiwa kuwa ilikuwa haifai, lakini E.L. aliing'ang'ania kama alimasi
(C) Kuliingiza taif kwenye mkataba mufilisi ,fisadi na angamizi wa Buzwagi . E.L. alikuwa pamoja na fisadi kuu Karamagi kusaini mkataba angamizi na filisi hotelini uingereza. Hivyo analipotezea taifa zaidi ya billioni 3,895/- kila mwaka kwa muda wa miaka 25 kama ulivyo mkataba
(D) Kujiingiza kwenye uporaji kwa kutumia ujenzi wa mahekalu ya hoteli ambayo hayalingani na kipato chake, akibisha data hallisi tutazianika hadharani.

David Ballali
(A) Amelipotezea taifa kifisadi zaidi ya sh 693,795,398,805.39/- kupitia BOT kwa malipo hewa kwa makampuni hewa ya kitapeli ya EPA, Jeetu P.ltd, Alex Stewart, Tangold ltd, Mwananchi gold co.ltd, Green F. Co.ltd na mengine mengi, (B)Kulipotezea taifa matrillioni ya fedha kwa kukwamisha ukaguzi halisi wa BOT (
C) Trillioni 5.3 alizochota kwa ajiri ya kampeini haramu za urais za mwaka 2005 zilizozaa rais mlea mafisadi – The breeder of corrupt leaders at all level

Basil Pesambili Mramba
(A)Alibarikina kuhusika na uporaji wa sh 17,697,556,594.85/- kutoka BOT akiwa waziri wa fedha kwenda kwa makampuni mbalimbali feki na watu binafsi hasa magabacholi wa kihindi na kiarabu
(B) ununuzi wa ndegefeki ya rais, rada feki ya rais. Alitangaza Watanzania hata wakila majani ndege feki ya rais lazima ingenunuliwa. Je, mr.. Mrmba, uliona Watanzania ni mbuzi hata wale majani?
(C) Uuzaji feki wa Air Tanzania kwa makaburu. Asingeiingilia kikwete Hapa Mrambaji angetajirika ukomo.
(D) Ubinafisaji holela na kwa kiburi na uhujumu wa rasilimali za tiafa kwa masilahi yake akiwa waziri wa fedha , walishirikiana na fisadi ambaye ni rafiki wake wa damu -Abdallah Kigoda

Andrew Chenge
(A) Kalipotezea taifa zaidi ya sh 17,857,616,400/- zilizoporwa na Tangold ltd kutoka BOT . Chenge hili hawezi kukwepa kwani alikuwa mkurugenzi wa Tangold ltd at the same time akiwa mkurugenzi wa BOT
(B) Kulipotezea taifa mabillioni ya fedha kwa kuridhia mikataba mibovu/feki/angamizi ya madini akiwa mwanasheria mkuu wa serikali. Takribani zilipotea zaidi y ash 2,890,687,084,573/- kwa kipindi chake chote. Kama anabisha tutazitoa kwa unyambulisho wake.
(C) Zaidi ya billioni 800 zianpotea kwa mwaka kwa mikataba mibovu ya ujenzi wa barabara ama kwa kuweka makampuni feki ambayo huishia kuchota fedha na kutoroaka nchini na vitita vya fedha. Ana kurugenzi wezi wizarani kwake lakini amefumbia macho kwa manufaa yake binafisi. Chenge unasubiri nini kung'atuka?

Gray Mgonja
(A) Alibariki na kuhisika na uporaji wa sh 17,857,616,400/- BOT kwenda kampuni yao ya tangold ltd akiwa mkurugenzi wa BOT pia hapo hapo akiwa mkurugenzi wa Tangold ltd kampuni ambyo hikuwa na usajili.
(B) Kunyamazia ufisadi wa uporaji wa trillioni za fedha BOT kenda kwenye makampuni hewa akiwa mkurugenzi BOT

Peter Msolla
(A) Uporaji wa sh millioni 5000 zilizokuwa zimetolewa na EUROPEAN OVERSEAS ANGENTS miaka ya 90 akiwa makamu mkuu wa SUA. Fedha hiyo ilikuwa imetolewa kukiendeleza chuo(SUA) kitaaluma, miundo mbinu kama barabara za ndani , tafiti mbalimbali na kuwa dila ya maendeleo ya kanda ya mashariki mwa Tanzania (Morogoro, Pwani, Tanga, Dar-es salaam). Cha ajabu fedha hiyo iliishia kwenye midomo ya mamba mafisadi (Prof Msolla, Prof Ishengoma, Mr A.. Magoma (mhasibu wa kufoji ), keshia Prof Mgongo na maswahiba wao.. Planner mkuu wa wizi huo alikuwa Magoma wakisaidiana na Msolla. Wakaamua kununua magari ya kifahali na kujenga majumba ya kifahali yakiwapo magesti house kwa siri.
(B)Uporaji wa fedha za DANIDA millioni 490 zilizokuwa zimetolewza kwa ajili ya mradi wa OTAITISI (OTITIS) .Fedha hiyo iligawanwa hapo vet –SUA na kunguru mafisadi wachache. Msolaa akachukua 80% ya fedha hiyo na kujenga majumba makubwa ya kifahali . Ng'ombe wa Mradi huo wakaishia kulala kwenye matope yafikapo kwenye kimo cha tumbo lao wakiwa wamesimama.. Wafadhili walikasirika kupita upeo, wakajitoa. Ukweli huu hauhitaji hata kupeleleza pale VET-SUA.
(C) Hujuma ya fedha ya punguzo la wafanyakazi SUA Tsh 2,245,045,000/- ilyotolewa na benki ya dunia 30/6/1996. Ilipangwa kwamba mtu mwenye mshahara mdogo kabisa apewe Tsh millioni 8. Jambo la kushangaza ni kwamba kila mtu aliyepunguzwa kazi alipewa asilimia kumi tu (10%) ya malipo yake. Hivyo mwenye mshahara mdogo alipewa sh 300,000/- tu. Aliyekuwa anatakiwa kulipwa millioni 20/- alipewa millioni tatu tu. Yeye Msolla na mafisadi wenzie (A.Magoma, Prof Luoga akiwa VC-SUA, Prof Mgongo, keshia na maswahiba wao waligawana 90% ya fedha yote iliyotolewa na benki ya dunia... Mafisadi hawa wakawa wanaishi kama wapo peponi. Wakanunua magari ya kifahali na kujenga majumba ya KUFURU yakiwamo magesti house bubu (kwa siri) na kununua mashamba kila kona Mkoani Morogoro.
(D) Wizi wa millioni 442/0 SUA kuamkia tarehe 22/4/2006.Yaani, Kati ya shs 442, shs millioni 400/- zilikuwa peti keshi zilizokusanywa kwa miaka miwili . Hivyo Msolla, Keshia, Prof Luoga na Magoma waliziiba zile millioni 400/- mchana kweupe tarehe 21/4/2006 kutoka kwenye sefu, baadaye wakaingiza sh millioni 42/- za malipo ya wafanya kazi SUA, ndipo kesho yake tarehe 22/4/2006 wakatangaza kuwa sh millioni 42/- za malipo ya wafanyakazi SUA zaibiwa Kwa uhakika zilizohamishwa kiporaji zilikuwa sh millioni 442(millioni 42 zikiwa malipo ya wafanyakazi SUA na millioni 400 zikiwa peti keshi ) . Sababu ya uporaji huo wa kifisadi ni: (i) kujiandaa kwa kustaafu kwa prof. Luoga, Mr Magoma na Msolla (ii) Kutokuwa na imani na kikwete kwani SUA walitegemea Sumayi ndiye angekuwa rais ambaye ni fisadi mwenzao. Hata hivyo hawakujua kuwa hata Kikwete ni mama na mlezi wa mafisadi (iii) Kupata fedha lukuku za kufanyia kampeini za ubunge kwa Msolla na hatimaye uwaziri. Hivyo kesi hiyo aliisimamia Prof Monera kwa ahadi kwamba kama angefanikiwa kuivunja kesi hiyo angekuwa VC. Monera alifanikiwa kuizima kesi hiyo, Prof Luoga na Msolla wakampendekeza kwa rais awe VC ili siri hii isifichuke. Kikwete akaingia kwa jeuri yake kichwakichwa akaweka fisadi pandikizi kuwa VC- la SUA ambalo linakomba fedha ya SUA nay a wafadhili likishirikiana na Mufilisi mwenzie Prof Msolla kiasi kwamba, fedha ya wafadhili inayopitia Wizarani (Sayansi na Elimu ya juu) kwenda SUA igawanwe na kukombwa vizuri.

Joseph Mungai :
(A) Aliingizasilabasi feki kuanzia chekechea hadi elimu ya sekondari kwa Watanzania wa kawaida huku watoto wao wanasoma nje ya nchi.Watoto hapa nchini hawakujua walichokuwa wanasoma, si jogg ama mchemsho. Akaua elimu kupindukia. Alifanya hivyo ili fedha nyingi zibaki wizarani ili azitumie na mafisadi wenzie kwa masilahi binafsi. Zaidi ya billioni 300 zilikuwa zinaliwa wizarani kwa ufisadi huu.
(B) Alikula takribani sh millioni 8/- za bima na rikizo za waalimu na mapunjo mbalimbali ya waalimu yakiwamo ya mishahara ya walimu wa shule za msingi na sekondari.Waalimu wakapiga kelele kudai haki zao wakaonekana kutimiza usemi kwamba KELELE ZA MLANGO HAZIMKOSESHI USINGIZI MWENYE NYUMBA.
(C) Kupora fedha inayobaki wizarani mwisho mwa mwaka. Kapuya alichagua baadhi ya maofisa wa elimu wa mikoa/wilaya na maedimasta wa shule za sekondari ambako alikuwa akituma fedha mwishoni mwa mwaka (mwezi wa 5) na baadaye kutuma wahasibu mafisadi kuifuata fedha hiyo. Alikuwa akipora kati y ash billioni 3-4 kwa mtindo huo kila mwaka alitafuna na maswahiba wake
Juma Ngasongwa (A) Kalipotezea taifa zaidi y ash Billioni 9,845/- kwa kipindi akiwa waziri wa Mali Asili na Utarii kwa kupewa pipi kidogo na kuachia uwindaji haramu na angamizi kwa rasilimali na uchumi wan chi. Ufisadi huu ulimfanya afukuzwe uwaziri wakati wa MZEE RUKSA kwani mzee ruksa alikuwa makini. Hakuwa kama kikwete ambaye amefunga ndoa na mafisadi kama Kapuya, Ngasongwa, Meghji, Ballali, Msolla, Diallo,Benno Ndullu nk. (B) Kuchochea vurugu SUA... Yeye alipoona kuwa wanafunzi wa SUA wamemkataa kwa kuwa alikuwa haeleweki anachofundisha , si DS ama DESKI CHAFU, alianza vurugu zilizomfanya afukuzwe kazi SUA katika miaka ya 90. akakimbilia siasa. Vilevile mzee ruksa akamfukuza kazi Mali asili na utalii katika miaka ya 90. ***** Mkapa akamrudisha kuhujumu, pia Kikwete akameza matapishi hayo hayo.
Stephanop Wasira
(A) Mamillioni ya fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kupunguza makali ya mbolea ameyakomba.. Yaani, fedha ya sabusidi ya mbolea zaidi y ash billioni 12,5 ameifagia na kufanya bei ya mbolea kuanza kupaa juu kama kunguru kila kukicha katika mikoa ya nyanda za juu kusini –The big four (Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa).Kilimo katika mikoa hiyo hutegemea mbolea asilimia mia moja(100%). Sasa mbolea haishikiki kwa wakulima wengi (90%) kwani ni kati y ash 40000/-sh 55000/- kwenye mfuko wa kilo 50. Kwa eka moja inahitajika mifuko 4-5 kutegemea na hali ya udongo husika. Mbaya zaidi , si kikwete wala wasira anayetembelea mikoa ya Mbeya, Iringa ama Rukwa tangu wawahadae wananchi kuwaletea maisha mazuri. Huu ni utapeli wa unaotakiwa ulaaniwe na kila mpenda haki.Kila leo utamwona Kikwete akitembelea KWA WASUKUMA (MWANZA NA SHINYANGA), BUKOBA NA MUSOMA, PWANI NA MOROGORO MAANA AMEYAONA MAJITU HAYO ZUMBUKUKU.

Nazir Karamagi
(A) Kufanya ufisadi wa kusaini mikataba angamizi ya madini kama ya Buzwagi nje ya nchi hotelini!!!!!!!!!!!! Uliolikosesha taifa sh 9,239,389,394.25/- kwa kipindi chote
(B)Kuligharimu taifa zaidi ya billioni 173 kutokana na uroho wa kujitumbukiza kwenye sakata la kampuni tapeli ya RICHMOND na binti ya DOWANS
(C) Kunyamazia kupanda kwa umeme kwa malipa kodi maskini ili kufidia gharama angamizi za TANESCO zinazotokana na mafisadi vigogo kutolipa gharama za umeme.

Ibrahim Msabaha
(A) Kulipotezea taif zaidi y ash billioni 174 kutokana na kufunga ndoa na kampuni mufilisi , feki na tapeli ya RICHMOND . Anatakiwa akamatwe atiwe ndani na alipe deni hilo .

Benno Ndullu
(A) Kabariki ufisadi na uharamia wa sh 693,795,398,800/- zilizohamishwa kijambazi na kaka zake (Ballali, Mramba, Zaakhi M) akiwa naibu gavana wa BOT. Hili halikwepi. Tunajua amewekwa pale na kikwete ili kuficha ushahidi wa mafisadi wenzie wakiwemo watoto wa vigogo. Hapa tayari anaingia kwenye kundi la mafisadi. (B) Kutomshauri kikwete avunje bodi inayoshughulikia kutafuta kiini cha ufisadi BOT,kwani bodi hiyo imejaa mafisadi kama G. Mgonja, Zakhia Meghji nk Hivyo hakuna chochote kitakachofanyika zaidi ya kwenda kuficha ushahidi.

Edward Hosea
(A): Amekomba zaidi ya billioni 65 kwa kupokea rushwa nene na kutoa taarifa feki kwenye uchunguzi wa RICHMOND , sakata la Buzwagi, mikataba mibovu ya madini, sakata na hujuma za wahindi kupanga kwenye nyumba nzuri za National Housing kuliko wazawa, Sakata la DOWANS na hujuma nyingine nyingi... Ni fisadi anayetakiwa ajiyzuru mara moja.

USHAURI KWA WAPINZANI
(1) Shinikizeni kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi itakayochaguliwa na wabunge mseto. Yaani wabunge 2 CCM, 2 CHADEMA, 2 CUF, I TLP, I UDP na isiwajibike kwa kingunge yoyote bali kwa masilahi ya kitaifa. Msipofanya hivyo, mtakuwa wasindikizaji watindikiwa katika uchaguzi wa mwaka 2010. Hata tahahir huwa hashiki moto.
(2) Tembeleeni vijijini mkawaelimishe watu wanaodanganywa na CCM kila kukicha, kwani huko ndiko kuna zaidi ya 85% ya wapiga kura nchini..Wanaishi maisha magumu kama wako mahabusu ya uhaini ndani ya nchi yao lakini hakuna wa kuwaelimisha Kikwete ndio amewasusa watu wa Mbeya, Iringa, Rukwa na Ruvuma huku akiita mikoa hiyo THE BIG FOUR na kunadi kuwa kilimo ni uti wa mgongo na kuwasuta akisema kuwa mbolea ya ruzuku haipo , wasibweteke, watainunua tu hata kama bei yake inapaa kama tai kila kukicha.. Kwa akili finyu ya watanzania, mwaka 2010 atajipitisha kwao na kuwafanya wasahau kuwa aliwahi kudondoka chini akiwahadaa maisha bora katika kura za mwaka 2005. Hivyo wapinzani tembeleeni vijijini maana mjini watu wanawaelewa.
(3) Piteni mkiwaambia watanzania kuwa MAFIGA MATATU YA KIKWETE ni kurudisha utawala wa chama kimoja wenye kubariki kila ufisadi na mafisadi wa uchumi wetu na rasilimali za taifa. Utawala wa kidikiteta na mufilisi bila kuhojiwa na mtu yeyote kwani bunge linakuwa na mafisadi wanaotetea mafisadi , ufisadi na hujuma ya kila aina kwa Watanzania ili mradi tu yapore utajiri wa taifa hili.

USHAURI KWA JK
(1) Wale wote wanaohusika na ufisadi usiwarudishe madarakani(uwaziri ama ukatibu mkuu ama ukurugenzi, kwa mfano
(A)WIZARA YA MIFUGO IMEOZA TANGU WAZIRI WAKE,MAKATIBU WAKUU NA KURUGENZI ZAKE NDIYO MAANA HAIPAFOMU CHOCHOTE. FEDHA ZAIDI YA MILLIONI 600 ZIMEKUWA ZIKITUMWA KWENYE RANCHI ZA KUZALISHA MITAMBA NA KWENDA KUCHUKULIWA BILA KUFANYA KAZI ILIYOKUSUDIWA
(B) WIZARA YA KILIMO OVYO M KWANI MBOLEA ZIMEPANDA NA ZINAPANDA KILA KUKICHA, WASIRA AMEKOMBA FUNGU LA MBOLEA ZA RUZUKU TAKRIBANI BILLIONI 12.5... DATA TUNAZO.
(2) ACHANA NA KUCHAGUA WATU KWA KUFUATA URAFIKI, UKOO, NAFIKIRI UMEYAONA MWENYEWE
imeletwa kwenu kwa niaba ya Yona Maro :- Bonyeza hapa kwa habari zaidi

Habari Ndio Hiyo…….. Maoni ya Wananchi

Ndugu JK.....
Watu wananchi wanasema hivi:
(!).Tanzania ni nchi yenye rasimali na utajiri wa hali ya juu Afrrica na ulimwenguni, lakini ni masikini ya kutupwa kwa kiwango cha nafasi ya tatu kwa umasikini duniani kwani nyie viongozi wa ngazi za juu mnalea n a kukumbatia ufisadi na mafisadi mufilisi ambayo nitayataja leo kwa ufisadi wake


(2). Utajiri wa rasilimali zinazoporwa na mafisadi ulionao zingeweza kufanya mambo makubwa na mazuri yafuatayo:

(i) Kusomesha Watanzania wote bure kuanzia Chekechea hadi kiwango cha PhD

(ii) Kuwalipa posho Watanzania wasio na ajira kila mwezi kama yanavyofanya mataifa yenye utajiri kama wetu

(iii) Kuwa na kilimo na mifugo bora na endelevu yenye kuingiza zaidi ya 60% ya pato la taifa kuliko sasa ambapo sekta hiyo inachangia 12% tu ya pato la taifa kutokana na kuhujumiwa na mafisadi wafanyabiashara kwa manufaa binafisi kma Wasira na Diallo
(iv) Kuwa na matibabu bure kwa kila mtanznia kwani kodi wanazotozwa wafanyakazi, wafanyabiashara na wakulima ni kubwa mno. Pia zaidi ya 90% ya pato la taifa inaporwa na mafisadi uliowaweka katika ngazi ya uwaziri, makatibu wakuu na kurugenzi mbalimbali kote nchini zikiwamo halimashauri

(v)Kuwa na viwanda vikubwa, vya kisasa vyenye kuingizia taifa zaidi ya 46% ya pato la taifa. Lakini cha kushangaza serikali imefunga ndoa nakunguruwaporaji wa uchumi wa kihindi na Kiarabu kama Jeetu P, Chavda naR. Aziz

(vi) Tanzania ingekuwa ni kisiwa cha uzuri na mandhari murua ya maendeleo ya kuja kujifunizia matifa mbalimbali ulimwenguni lakini cha ajabu ndiyo imekuwa jalala la kila nyanja ya umasikini
(vii) Ndugu Kikwete, pamoja na kwamba Mafisadi lowassa, karamagi na msabaha waneshaachia ngazi, bado kuna mafisadi wengine uliowakumbatia na kuwaweka karibu na wewe huku wakiifilisi nchi kama mafisi ya kienyeji ni hawawafuatao:Zakhia Meghji:-
(A) aligawa holela vitalu vya uwindaji akaipotezea Tanzania Tsh 3,304, 903,050/- akiwa waziri wa Mali Asili na Utalii.Ovyo zaidi hata wanafamilia wake walijiingiza katika ufisadi huo kwa kumiliki baadhi ya vitalu kibadhilifu
(B) Alipotosha ripoti ya mkaguzi wa BOT mwaka 2005/2006

(C) Kuchonga bajeti angamizi ya mwaka 2007/2008

(D) Kuidhinisha matumizi mabovu zaidi ya millioni 143 kwa mawaziri mafisadi kwenda kuifagilia bajeti ya kihuni ya 2007/2008 mikoani. Mafisadi hao hawakusita kukomba millioni 143 Tsh kwenda kuzomewa mikoani.

(E) Kufumbia macho shughuli fisadi na za kitaprli za BOT ambayo iliipatia Tangold ltd Kampuni feki kiasi zaidi ya Sh37.7 billioni ambayo haikuwa na usajiri wowote, akidanganya kuwa ni matumizi nyeti ya serikali kumbe ni ulaji wake na vigogo wenzake
(F) Kubarikli uporaji wa fedha BOT tsh 18,465,755,495.39/- zilizopelekwa kwenye makampuni mbalimbali feki kuanzia decemba 2005 hadi 2007. Benjamini Mkapa:

(A) Kufanya biashara akiwa ikulu ambacho ni kinyume kabisa na katiba ya nchi yetu

(B) Kuanzisha makampuni mufilisi akiwa ikulu ambayo yamelipora taifa zaidi ya Tsh 908,798,045,050/- akiwa ikulu hadi leo kwa makampuni ya kihuni kama ANBEN ltd, Fosnik ltd na Tanpower
(C) Wizi wa zaidi ya Tsh Trillioni 8,86 BOT kwenye kampeini za uraisi na ubunge zilizotuwekea rais mufilisi. Mkapa anatakiwa asimame kuelekea kizimbani na kujibu wizi huo ulioifilisi nchi ikawa kama dampo la umasikini
(D) Uporaji fedha za taia hili kupitia ununuzi wa rada feki Tsh 50 billioni ambayo aliishupalia kama ruba
(E) Uuzwaji angamizi wa mashirika ya umma na viwanda kwa hila zote, kwani hata yale yaliyokuwa yakijiendesha kwa faida kubwa yaliuzwa kwa bei ya tupatupa (throw away prices)
(F) Kushiriki mikataba mibovu ya madini alilipotezea taifa zaidi ya Tsh 959,588,789,005/- kwa kipindi chote Hivyo huyu ni fisadi lililokubuhu. Edward Lowassa

(A) Anahusika moja kwa moja na ufisadi kupitia kampuni haramu ya RICHMOND na shoga wake DOWANS ambao wamelipora taifa zaidi y ash billioni 273/- kwa umeme hewa

(B) Upotevu wa sh millioni 12.5 /- kupitia kampuni feki ya Water City ambayo aliibariki licha ya kuambiwa kuwa ilikuwa haifai, lakini E.L. aliing'ang'ania kama alimasi

(C) Kuliingiza taif kwenye mkataba mufilisi ,fisadi na angamizi wa Buzwagi . E.L. alikuwa pamoja na fisadi kuu Karamagi kusaini mkataba angamizi na filisi hotelini uingereza.Hivyo analipotezea taifa zaidi ya billioni 3,895/- kila mwaka kwa muda wa miaka 25 kama ulivyo mkataba

(D) Kujiingiza kwenye uporaji kwa kutumia ujenzi wa mahekalu ya hoteli ambayo hayalingani na kipato chake, akibisha data hallisi tutazianika hadharani. David Ballali

(A) Amelipotezea taifa kifisadi zaidi ya sh693,795,398,805.39/- kupitia BOT kwa malipo hewa kwa makampuni hewa ya kitapeli ya EPA, Jeetu P.ltd, Alex Stewart, Tangold ltd, Mwananchi gold co.ltd, Green F. Co.ltd na mengine mengi,

(B)Kulipotezea taifa matrillioni ya fedha kwa kukwamisha ukaguzi halisi wa BOT

(C) Trillioni 5.3 alizochota kwa ajiri ya kampeini haramu za urais za mwaka 2005 zilizozaa rais mlea mafisadi - The breeder of corrupt leaders at all level Dasil Pesambili Mramba

(A)Alibarikina kuhusika na uporaji wa sh17,697,556,594.85/- kutoka BOT akiwa waziri wa fedha kwenda kwa makampuni mbalimbali feki na watu binafsi hasa magabacholi wa kihindi na kiarabu

(B) ununuzi wa ndegefeki ya rais, rada feki ya rais. Alitangaza Watanzania hata wakila majani ndege feki ya rais lazima ingenunuliwa. Je, mr. Mrmba, uliona Watanzania ni mbuzi hata wale majani?

(C) Uuzaji feki wa Air Tanzania kwa makaburu. Asingeiingilia kikwete Hapa Mrambaji angetajirika ukomo.

(D) Ubinafisaji holela na kwa kiburi na uhujumu wa rasilimali za tiafa kwa masilahi yake akiwa waziri wa fedha , walishirikiana na fisadi ambaye ni rafiki wake wa damu -Abdallah Kigoda Andrew Chenge

(A) Kalipotezea taifa zaidi ya sh 17,857,616,400/- zilizoporwa na Tangold ltd kutoka BOT . Chenge hili hawezi kukwepa kwani alikuwa mkurugenzi wa Tangold ltd at the same time akiwa mkurugenzi wa BOT

(B) Kulipotezea taifa mabillioni ya fedha kwa kuridhia mikataba mibovu/feki/angamizi ya madini akiwa mwanasheria mkuu wa serikali. Takribani zilipotea zaidi y ash 2,890,687,084,573/- kwa kipindi chake chote. Kama anabisha tutazitoa kwa unyambulisho wake.
(C) Zaidi ya billioni 800 zianpotea kwa mwaka kwa mikataba mibovu ya ujenzi wa barabara ama kwa kuweka makampuni feki ambayo huishia kuchota fedha na kutoroaka nchini na vitita vya fedha.Ana kurugenzi wezi wizarani kwake lakini amefumbia macho kwa manufaa yake binafisi. Chenge unasubiri nini kung'atuka? Gray Mgonja

(A) Alibariki na kuhisika na uporaji wa sh 17,857,616,400/- BOT kwenda kampuni yao ya tangold ltd akiwa mkurugenzi wa BOT pia hapo hapo akiwa mkurugenzi wa Tangold ltd kampuni ambyo hikuwa na usajili.

(B) Kunyamazia ufisadi wa uporaji wa trillioni za fedha BOT kenda kwenye makampuni hewa akiwa mkurugenzi BOT Peter Msolla

(A) Uporaji wa sh millioni 5000 zilizokuwa zimetolewa na EUROPEAN OVERSEAS ANGENTS miaka ya 90 akiwa makamu mkuu wa SUA. Fedha hiyo ilikuwa imetolewa kukiendeleza chuo(SUA) kitaaluma, miundo mbinu kama barabara za ndani , tafiti mbalimbali na kuwa dila ya maendeleo ya kanda ya mashariki mwa Tanzania (Morogoro, Pwani, Tanga, Dar-es salaam). Cha ajabu fedha hiyo iliishia kwenye midomo ya mamba mafisadi (Prof Msolla, Prof Ishengoma, Mr A. Magoma (mhasibu wa kufoji ), keshia Prof Mgongo na maswahiba wao.. Planner mkuu wa wizi huo alikuwa Magoma wakisaidiana na Msolla. Wakaamua kununua magari ya kifahali na kujenga majumba ya kifahali yakiwapo magesti house kwa siri.

(B)Uporaji wa fedha za DANIDA millioni 490 zilizokuwa zimetolewza kwa ajili ya mradi wa OTAITISI (OTITIS) .Fedha hiyo iligawanwa hapo vet -SUA na kunguru mafisadi wachache. Msolaa akachukua 80% ya fedha hiyo na kujenga majumba makubwa ya kifahali . Ng'ombe wa Mradi huo wakaishia kulala kwenye matope yafikapo kwenye kimo cha tumbo lao wakiwa wamesimama.. Wafadhili walikasirika kupita upeo, wakajitoa. Ukweli huu hauhitaji hata kupeleleza pale VET-SUA.

(C) Hujuma ya fedha ya punguzo la wafanyakazi SUA Tsh 2,245,045,000/- ilyotolewa na benki ya dunia 30/6/1996. Ilipangwa kwamba mtu mwenye mshahara mdogo kabisa apewe Tsh millioni 8.
Jambo la kushangaza ni kwamba kila mtu aliyepunguzwa kazi alipewa asilimia kumi tu (10%) ya malipo yake. Hivyo mwenye mshahara mdogo alipewa sh 300,000/- tu.
Aliyekuwa anatakiwa kulipwa millioni 20/- alipewa millioni tatu tu. Yeye Msolla na mafisadi wenzie (A.Magoma, Prof Luoga akiwa VC-SUA, Prof Mgongo, keshia na maswahiba wao waligawana 90% ya fedha yote iliyotolewa na benki ya dunia. Mafisadi hawa wakawa wanaishi kama wapo peponi. Wakanunua magari ya kifahali na kujenga majumba ya KUFURU yakiwamo magesti house bubu (kwa siri) na kununua mashamba kila kona Mkoani Morogoro.

(D) Wizi wa millioni 442/0 SUA kuamkia tarehe 22/4/2006.Yaani, Kati ya shs 442, shs millioni 400/- zilikuwa peti keshi zilizokusanywa kwa miaka miwili .
Hivyo Msolla, Keshia, Prof Luoga na Magoma waliziiba zile millioni 400/- mchana kweupe tarehe 21/4/2006 kutoka kwenye sefu, baadaye wakaingiza sh millioni 42/- za malipo ya wafanya kazi SUA, ndipo kesho yake tarehe22/4/2006 wakatangaza kuwa sh millioni 42/- za malipo ya wafanyakazi SUA zaibiwa Kwa uhakika zilizohamishwa kiporaji zilikuwa sh millioni 442(millioni 42 zikiwa malipo ya wafanyakazi SUA na millioni 400 zikiwa peti keshi ) . Sababu ya uporaji huo wa kifisadi ni:

(i) kujiandaa kwa kustaafu kwa prof. Luoga, Mr Magoma na Msolla
(ii) Kutokuwa na imani na kikwete kwani SUA walitegemea Sumayi ndiye angekuwa rais ambaye ni fisadi mwenzao. Hata hivyo hawakujua kuwa hata Kikwete ni mama na mlezi wa mafisadi
(iii) Kupata fedha lukuku za kufanyia kampeini za ubunge kwa Msolla na hatimaye uwaziri.Hivyo kesi hiyo aliisimamia Prof Monera kwa ahadi kwamba kama angefanikiwa kuivunja kesi hiyo angekuwa VC.
Monera alifanikiwa kuizima kesi hiyo,
Prof Luoga na Msolla wakampendekeza kwa rais awe VC ili siri hii isifichuke.Kikwete akaingia kwa jeuri yake kichwakichwa akaweka fisadi pandikizi kuwaVC- la SUA ambalo linakomba fedha ya SUA nay a wafadhili likishirikiana na Mufilisi mwenzie Prof Msolla kiasi kwamba, fedha ya wafadhili inayopitia Wizarani (Sayansi na Elimu ya juu) kwenda SUA igawanwe na kukombwa vizuri. Joseph Mungai

A) Aliingizasilabasi feki kuanzia chekechea hadi elimu ya sekondari kwa Watanzania wa kawaida huku watoto wao wanasoma nje ya nchi.
Watoto hapa nchini hawakujua walichokuwa wanasoma, si jogg ama mchemsho. Akaua elimu kupindukia.
Alifanya hivyo ili fedha nyingi zibaki wizarani ili azitumie na mafisadi wenzie kwa masilahi binafsi.
Zaidi ya billioni 300 zilikuwa zinaliwa wizarani kwa ufisadi huu.

(B) Alikula takribani sh millioni 8/- za bima na rikizo za waalimu na mapunjo mbalimbali ya waalimu yakiwamo ya mishahara ya walimu wa shule za msingi na sekondari.
Waalimu wakapiga kelele kudai haki zao wakaonekana kutimiza usemi kwamba KELELE ZA MLANGO HAZIMKOSESHI USINGIZI MWENYE NYUMBA.

(C) Kupora fedha inayobaki wizarani mwisho mwa mwaka. Kapuya alichagua baadhi ya maofisa wa elimu wa mikoa/wilaya na maedimasta wa shule za sekondari ambako alikuwa akituma fedha mwishoni mwa mwaka (mwezi wa 5) na baadaye kutuma wahasibu mafisadi kuifuata fedha hiyo. Alikuwa akipora kati ya sh billioni3-4 kwa mtindo huo kila mwaka alitafuna na maswahiba wake Juma Ngasongwa

(A) Kalipotezea taifa zaidi y ash Billioni 9,845/- kwa kipindi akiwa waziri wa Mali Asili na Utarii kwa kupewa pipi kidogo na kuachia uwindaji haramu na angamizi kwa rasilimali na uchumi wan chi.Ufisadi huu ulimfanya afukuzwe uwaziri wakati wa MZEE RUKSA kwani mzee ruksa alikuwa makini. Hakuwa kama kikwete ambaye amefunga ndoa na mafisadi kama Kapuya, Ngasongwa, Meghji, Ballali, Msolla, Diallo,Benno Ndullu nk.

(B) Kuchochea vurugu SUA. Yeye alipoona kuwa wanafunzi wa SUA wamemkataa kwa kuwa alikuwa haeleweki anachofundisha , si DS ama DESKI CHAFU, alianza vurugu zilizomfanya afukuzwe kazi SUA katika miaka ya 90. akakimbilia siasa.Vilevile mzee ruksa akamfukuza kazi Mali asili na utalii katika miaka ya 90.Bwege Mkapa akamrudisha kuhujumu, pia Kikwete akameza matapishi hayo hayo. Stephanop Wasira

(A) Mamillioni ya fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kupunguza makali ya mbolea ameyakomba.
Yaani, fedha ya sabusidi ya mbolea zaidi y ash billioni 12,5 ameifagia na kufanya bei ya mbolea kuanza kupaa juu kama kunguru kila kukicha katika mikoa ya nyanda za juu kusini -The big four (Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa).
Kilimo katika mikoa hiyo hutegemea mbolea asilimia mia moja(100%). Sasa mbolea haishikiki kwa wakulima wengi(90%) kwani ni kati y ash 40000/-sh 55000/- kwenye mfuko wa kilo 50. Kwa eka moja inahitajika mifuko 4-5 kutegemea na hali ya udongo husika. Mbaya zaidi , si kikwete wala wasira anayetembelea mikoa ya Mbeya, Iringa ama Rukwa tangu wawahadae wananchi kuwaletea maisha mazuri.
Huu ni utapeli wa unaotakiwa ulaaniwe na kila mpenda haki.Kila leo utamwona Kikwete akitembelea KWA WASUKUMA (MWANZA NA SHINYANGA), BUKOBA NA MUSOMA, PWANI NA MOROGORO MAANA AMEYAONA MAJITU HAYO ZUMBUKUKU.
Nazir Karamagi (A) Kufanya ufisadi wa kusaini mikataba angamizi ya madini kama ya Buzwagi nje ya nchi hotelini!!!!!!!!!!!! Uliolikosesha taifa sh9,239,389,394.25/- kwa kipindi chote

(B)Kuligharimu taifa zaidi ya billioni173 kutokana na uroho wa kujitumbukiza kwenye sakata la kampuni tapeli ya RICHMOND na binti ya DOWANS

(C) Kunyamazia kupanda kwa umeme kwa malipa kodi maskini ili kufidia gharama angamizi za TANESCO zinazotokana na mafisadi vigogo kutolipa gharama za umeme. Ibrahim Msabaha

(A) Kulipotezea taif zaidi y ash billioni 174 kutokana na kufunga ndoa na kampuni mufilisi , feki na tapeli ya RICHMOND . Anatakiwa akamatwe atiwe ndani na alipe deni hilo . Benno Ndullu
(A) Kabariki ufisadi na uharamia wa sh 693,795,398,800/- zilizohamishwa kijambazi na kaka zake (Balali, Mramba, Zaakhi M) akiwa naibu gavana wa BOT.
Hili halikwepi. Tunajua amewekwa pale na kikwete ili kuficha ushahidi wa mafisadi wenzie wakiwemo watoto wa vigogo. Hapa tayari anaingia kwenye kundi la mafisadi.

(B) Kutomshauri kikwete avunje bodi inayoshughulikia kutafuta kiini cha ufisadi BOT,kwani bodi hiyo imejaa mafisadi kama G. Mgonja, Zakhia Meghji nk Hivyo hakuna chochote kitakachofanyika zaidi ya kwenda kuficha ushahidi. Edward Hosea

(A): Amekomba zaidi ya billioni 65 kwa kupokea rushwa nene na kutoa taarifa feki kwenye uchunguzi wa RICHMOND , sakata la Buzwagi, mikataba mibovu ya madini, sakata na hujuma za wahindi kupanga kwenye nyumba nzuri za National Housing kuliko wazawa, Sakata la DOWANS na hujuma nyingine nyingi.
Ni fisadi anayetakiwa ajiyzuru mara moja.USHAURI KWA WAPINZANI(1) Shinikizeni kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi itakayochaguliwa nawabunge mseto.
Yaani wabunge 2 CCM, 2 CHADEMA, 2 CUF, I TLP, I UDP na isiwajibike kwa kingunge yoyote bali kwa masilahi ya kitaifa. Msipofanya hivyo, mtakuwa wasindikizaji watindikiwa katika uchaguzi wa mwaka 2010. Hata tahahir huwa hashiki moto.(2) Tembeleeni vijijini mkawaelimishe watu wanaodanganywa na CCM kilakukicha, kwani huko ndiko kuna zaidi ya 85% ya wapiga kura nchini..
Wanaishi maisha magumu kama wako mahabusu ya uhaini ndani ya nchi yao lakini hakuna wa kuwaelimisha Kikwete ndio amewasusa watu wa Mbeya, Iringa, Rukwa na Ruvuma huku akiita mikoa hiyo THE BIG FOUR na kunadi kuwa kilimo ni uti wa mgongo na kuwasuta akisema kuwa mbolea ya ruzuku haipo , wasibweteke, watainunua tu hata kama bei yake inapaa kama tai kila kukicha..
Kwa akili finyu ya watanzania, mwaka 2010 atajipitisha kwao na kuwafanya wasahau kuwa aliwahi kudondoka chini akiwahadaa maisha bora katika kura za mwaka 2005.
Hivyo wapinzani tembeleeni vijijini maana mjini watu wanawaelewa.

(3) Piteni mkiwaambia watanzania kuwa MAFIGA MATATU YA KIKWETE nikurudisha utawala wa chama kimoja wenye kubariki kila ufisadi na mafisadi wa uchumi wetu na rasilimali za taifa.
Utawala wa kidikiteta na mufilisi bila kuhojiwa na mtu yeyote kwani bunge linakuwa na mafisadi wanaotetea mafisadi , ufisadi na hujuma ya kila aina kwa Watanzania ili mradi tu yapore utajiri wa taifa hili.USHAURI KWA JK

(1) Wale wote wanaohusika na ufisadi usiwarudishe madarakani(uwaziri amaukatibu mkuu ama ukurugenzi, kwa mfano

(A)WIZARA YA MIFUGO IMEOZA TANGU WAZIRI WAKE,MAKATIBU WAKUU NA KURUGENZI ZAKE NDIYO MAANA HAIPAFOMU CHOCHOTE.FEDHA ZAIDI YA MILLIONI 600 ZIMEKUWA ZIKITUMWA KWENYE RANCHI ZA KUZALISHA MITAMBA NA KWENDA KUCHUKULIWA BILA KUFANYA KAZI ILIYOKUSUDIWA

(B) WIZARA YA KILIMO OVYO M KWANI MBOLEA ZIMEPANDA NA ZINAPANDA KILA KUKICHA, WASIRA AMEKOMBA FUNGU LA MBOLEA ZA RUZUKU TAKRIBANI BILLIONI 12.5. DATA TUNAZO.

(2)ACHANA NA KUCHAGUA WATU KWA KUFUATA URAFIKI, UKOO, NAFIKIRI UMEYAONAMWENYEWE

Yona Maro

Membe na Chenge wavurunda mkataba Uchina

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameelezwa kukerwa na jinsi mawaziri wa serikali yake wanavyofanyakazi bila uangalifu. Watu waliokaribu na Rais Kikwete na walioongozana naye katika ziara ya India, China na Marekani, waliliambia gazeti hili kuwa kukwerwa huko kulitokana na baadhi ya mawaziri kuharibu mkataba.
Walisema kuwa mkataba huo uliokuwa kwa upande mmoja usainiwe na waziri wa Tanzania na upande mwingine waziri wa China, uliharibika baada ya kusainiwa na mawaziri wawili wa Tanzania, hivyo kuharibu itifaki.
Wakizungumza kwa sharti la kutokutajwa majina gazetini, walisema kuwa mkataba huo ulikuwa batili baada ya kusainiwa na mawaziri hao waandamizi, hali iliyomfanya Rais Kikwete kuja juu kutokana na uzembe huo.Vyanzo hivyo vya habari vilidai kuwa mkataba huo ulisainiwa na mawaziri hao wawili kutokana na jinsi ulivyokuwa umeendaliwa licha ya ukweli kwamba ulikuwa ukihusu zaidi wizara moja.
Walidai kuwa mkataba huo uliokuwa ukihusisha masuala ya wizara ya miundombinu, katika mazingira yasiyoeleweka ulianza kusainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na kisha kusainiwa na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge.
Vyanzo hivyo vilidai kuwa Waziri Membe alisaini mkataba huo baada ya kuwepo kwa sehemu yake ya kusaini, huku nyuma kukiwa na sehemu ya kusaini Chenge.
Kulingana na vyanzo hivyo, inadaiwa kuwa baada ya kusainiwa, mkataba huo ulikuwa batili kwa kuwa ulipaswa kuhusisha waziri mmoja wa Tanzania na mwingine wa China.
Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja aliyehusika na uzembe huo katika mkataba huo ambao unadaiwa uliandaliwa mapema tangu kuwapo kwa taarifa ya safari ya Rais Kikwete nchini China.
Pia haikuweza kufahamika hatua ambazo Rais Kikwete anaweza kuzichukua dhidi ya mawaziri wake hao kutokana na uzembe wa kuandaa mikataba kama ilivyojitokeza.

Wednesday, April 23, 2008

Rais mtaafu Mkapa, mkewe waumbuliwa bungeni kwa mgodi wa Kiwira










MBUNGE wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), amewatuhumu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, mkewe Mama Anna Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, kuwa walinunua mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira, wilayani Rungwe, Mbeya kwa kificho.

Mbunge huyo alidai bungeni jana kuwa mwaka 2004, Mkapa kwa kushirikiana na mkewe pamoja na Yona, walianzisha Kampuni ya TanPower Resources Ltd na mwaka mmoja baadaye wakauziwa machimbo ya Kiwira kimya kimya.

Kimaro alitoa madai hayo alipokuwa akichangia Muswada wa Sheria ya Umeme wa Mwaka 2008, bungeni, mjini hapa juzi jioni.

Alidai kuwa katika mauziano hayo ya siri, Kampuni ya TanPower Resources Limited,
ilikuwa iilipe serikali Sh700milioni katika mradi huo uliogharimu, zaidi ya Sh4bilioni, lakini kampuni hiyo ilifanya malipo ya awali ya Sh70milioni tu.

"Waliuziwa kwa Sh700milioni bila kutangazwa na wao wakalipa down payment (malipo
ya awali)Sh70 milioni," alisema Kimaro.

Aliendelea kudai kuwa mwaka 2006, Mkapa, Anna na Yona, waliingia mkataba na Shirika la
Umeme nchini (Tanesco) kwa ajili ya kufua umeme kwa makubaliano ya kulipwa Gharama za uwekezaji ('capacity charge') Sh146milioni kila siku, bila kujali kwamba wamefua umeme au la.
"Sasa mimi nauliza huu ni uadilifu kweli? Haya ni maadili kweli? Tufike mahala
tuseme inatosha. Hivi tunawafundisha nini vijana hawa ambao ni mawaziri?," alihoji
Kimaro na kuongeza:

"Rais Jakaya Kikwete alisema urais wake hauna ubia na mtu. Basi aseme huu ni mwisho kwa wanaotuhujumu, tuwaambie basi na washughulikiwe kwa mujibu wa sheria."

Awali, akichangia muswada huo, Kimaro alisema ipo haja ya kuwa makini katika kuupitisha muswada huo kwa kuwa wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika umeme, si rahisi kwenda vijijini kusambaza nishati hiyo.

Kutokana na hali hiyo, aliitaka serikali kuifufua Tanesco kwa kuipa fedha ili (serikali) iwe na chombo chake cha kuzalisha umeme.

Naye Mbunge wa Mpanda Kati (Chadema), Said Amour Arfi, alishangazwa namna serikali
inavyotumia nguvu nyingi kuupitisha muswada huo.

Alisema haafiki kupitishwa kwa muswada huo na kuongeza kuwa nguvu inayotumika kuharakisha kupitishwa muswada huo si ya kawaida.

Alisema hoja ya kuwa muswada huo ukipita, wananchi wa vijijini watapata umeme wa bei rahisi, haina nguvu.

Alitoa mfano wa Kampuni ya Artumas ambayo baadhi ya wabunge waliipigia debe, kwamba haitaweza kuondoa matatizo ya umeme.

Tanesco itaingiaje katika ushindani wakati ikiwa hoi? Tanesco inavishwa majukumu
ya kisiasa,? alisema na kuonya kwamba wawekezaji watakaokuja si ajabu wakafanana na hadithi ya ubinafsishwaji wa Benki ya NMB.

Alikumbusha kuwa wakati NMB inabinafsishwa, ilisemwa kuwa itakuwa benki ya wananchi
na itawafikia watu wengi, lakini leo hii ukitaka kufungua tawi vijijini wana vigezo vyao na si jambo rahisi kufika huko.

?Na hao (wawekezaji) wakija, wataweka vigezo vyao vya kusambaza umeme vijijini ambavyo havitawawezesha wananchi wa huko kunufaika na huduma hiyo,? alibainisha.

Naye Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela alimwangaliza Waziri wa Nishati
na Madini, William Ngeleja, kutambua aina ya wawekezaji wanaotarajiwa kuwekeza katika sekta ya umeme baada ya sheria mpya ya sekta hiyo kupitishwa, kwani ndiyo watakaomwangusha ama kumwinua.

?Nakupa angalizo Mheshimiwa Waziri, ujue kuwa aina ya wawekezaji watakaoingia katika sekta ya nishati ndiyo watakaokuangusha au kukuinua, wapo Watanzania wenzetu wanajiandaa kuingia katika biashara hiyo, wengine ni wale walionufaika na mikataba mibovu kama ule wa Richmond,? alitahadharisha Mbunge huyo.

Alidai kuwa baadhi ya Watanzania, hususani walionufaika na mikataba inayolitia hasara Tanesco, wameanza kujiandaa kuwekeza kwenye sekta hiyo.

Alisema kuwa, kimsingi ni muhimu kwa serikali kuhakikisha kuwa Tanesco inakuwa imara katika kipindi hiki cha ushindani, ambacho kinahitaji nguvu zaidi kwa shirika hilo la umeme ili kukabiliana na ushindani utakaotokana na kupitishwa kwa sheria hiyo.

Aliangaliza kuwa serikali inatakiwa kutambua kuwa Mtanzania wa leo anaitambua nchi yake na hivyo kuna umuhimu mkubwa kuwa na ufahamu kwamba mageuzi ya kiuchumi ni muhimu na sharti yajengwe palipo na mfumo imara wa usambazaji wa umeme.

Kwa upande wake Mbunge wa Moshi Mjini (Chadaema), Philemon Ndesamburo ambaye mbali
ya kuunga mkono hoja hiyo alishauri kuwa umeme usiwe kitu cha anasa na badala yake kiweze kupatikana kwa kila mtu anayekihitaji.

Mbunge huyo wa Moshi Mjini alishauri kuwa pamoja na umuhimu wa serikali kuingia katika mfumo huo mpya, jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa maeneo ya mipakani yakatumia fursa ya kuwepo umeme kutoka nchi jirani.
Na Muhibu Said, Dodoma

Katibu Chadema, viongozi wa dini, wengine 12 watupwa rumande Buzwagi

KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Kahama , Lucas Petro (52) na wakazi wengine 13 , wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kufanya mkusanyiko usio halali katika mgodi wa Buzwagi kushinikiza walipwe fidia.

Mratibu Msaidizi wa Polisi Mayila Kisanjo, aliwataja wengine Mahakama ya Wilaya ya Kahama mbele ya Hakimu Hassani kuwa ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyahanga, Simon Charles (45) , Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Chapulwa kupitia Chama cha Tanzania Labour (TLP), Tabo Majabi (48) na Juma Protas (40).

Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God (EAGT), Issa Issa (28), Mwalimu wa dini ya kiislamu Kahama Mjini, Jumanne Ntalula (48), balozi katika Kijiji cha Mwime na Mapande Machibya (56), ambaye ni mkulima kijiji cha Chapulwa.

Masanja Kashinje (50), Mathias John (45), Magaka Paulo (23), Bundala Makoye (26), Gema Maganga (41), wakazi wa Kijiji cha Mwendakulima.

Wengine ni Amos Malimi (53), mkazi wa Kijiji cha Mwime na Daudi Msuya (61), mfanyabiashara wa Kahama mjini.

Alidai kuwa washtakiwa hao wanadaiwa kufanya mkusanyiko usio halali katika lango la makao makuu ya mgodi huo, uliopo Kijiji cha Mwime kushinikizwa kulipwa fidia

Washtakiwa hao ambao walitiwa nguvuni juzi asubuhi, walikanusha mashtakana kupelekwa rumande katika Gereza la Wilaya ya Kahama hadi Mei 2, kesi yao itakapotajwa tena.

Na Zulfa Mfinanga, Shinyanga

Wakazi wa Buzwagi watawanywa kwa risasi, mabomu

Familia 500 zataka kurejea katika makazi yao mgodini

WANANCHI waliohamishwa kupisha ujenzi wa Mgodi wa Buzwagi, wilayani Kahama jana walitawanywa kwa risasi na mabomu ya kutoa machozi yaliyokuwa yakipigwa na Polisi kuzima jaribio lao la kutaka kurudi kwa nguvu katika makazi yao.


Jaribio hilo ambalo lilitangazwa juzi na wananchi hao lilianza alfajiri jana
baada ya wananchi hao kukusanyika kwa wingi wakiwa na mabango mbalimbali wakitaka kurudi kwa nguvu kwenye makazi yao ambayo yapo ndani ya uzio wa Mgodi wa Buzwagi.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Magesa Mulongo alisema kuwa kabla ya wananchi hao kutaka kuvamia kurudi kwenye makazi yao walisambaza ujumbe kwenye simu za mikononi ikiwemo simu yake unaodai kuwa umetoka kwa mtu mwenye nguvu ya kushawishi wananchi.

Mulongo alisema katika ujumbe huo, wananchi walidai kwa kuwa hawana uwezo wa kuinunua dola(serikali) ili iwatusaidie, watadai haki yao kwa kuweka rehani damu yao na kwamba ujumbe huo ulisambazwa kwa viongozi mbalimbali wa Serikali.

Alisema wananchi hao tayari wamelipwa fidia kwa asilimia 98, lakini baada ya kutumia vibaya fedha hizo, wamerudi kudai upya kwa maelezo kwamba walipunjwa wakati wa kuingia mkataba wa fidia na Kampuni ya Barrick.

Kufuatia tukio la jana, ambapo watu14 wanashikiliwa na polisi wilayani hapa, Mulongo alifahamisha kuwa wananchi hao walivamia mgodi huo kwa lengo la kuuhujumu.

Alisema licha ya Kamati ya Ulinzi na Usalama kuwazuia kuvamia eneo hilo, waligoma kuondoka kwa madai ya kwamba mpaka Mbunge wao James Lembeli afike mgodini hapo.

Wananchi hao waliokuwa wakipiga makelele wakidai kuwa wamiliki wa mgodi huo
ni makaburu na mafisadi, walidai kuwa mbuge wao aliwaagiza kuwa warudi katika
maeneo yao ambayo tayari walikwishalipwa fedha na nyumba zao kubomolewa kupisha ujenzi wa mgodi huo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya, kampuni ya Barrick ilikwishajenga nyumba 205 za fidia kwa wananchi walioondolewa, lakini nyumba 50 kati ya hizo bado zipo wazi baada ya wenyewe kugoma kuhamia, kwa sababu zisizoeleweka.

Mgodi huo wa Buzwagi umejumuisha vijiji vitatu, ambapo katika kijiji cha Mwendakulima tayari wote wameondoka na Mwime, familia tisa zimegoma huku zikiwa zimelipwa fidia na bado zimo ndani ya uzio wa kampuni hiyo.

Mulongo alisema kuwa katika Kijiji cha Chapulwa familia nne zimegoma kuondoka zikiwa zimelipwa fidia isipokuwa moja ambayo ilikataa kupokea.

Katika tukio la jana wananchi hao wapatao zaidi ya 500 walikuwa wamezingira lango
kuu la kuingia mgodini hapo.

Licha Mkuu Wilaya kuwata waondoke wakafanye mkutano katika ofisi za Serikali za Vijiji vyao ili kupata mwafaka wa haki zao, wananchi hao waligoma.

Baada ya kuona vurugu zinakuwa kubwa polisi waliingilia katina walianza kurusha risasi na mabomu ya kutoa hewani ili kuwatawanya wananchi.

Katika vurugu hizo watu 14 walikamatwa, lakini vinara wa vurugu hizo walitimua mbio kukwepa mkono wa sheria na polisi wanaendelea kuwasaka.

Kuanzia jana mgodi huo upo chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi kutoka Shinyanga wakishiriana na wa wilayani Kahama.


Na Shija Felician, Kahama

Tuesday, April 22, 2008

Maoni ya Watanzania

Pole jamaa wote wa Dito na CCM kwa ujumla,lakini hiyo ni njia ya wote na yeye Dito katangulia nasi tupo nyuma.TANGULIA BABA!NENDA BABA!wasalimie JK wa Butiama na umwambie TZ inayumbishwa na JK wa Chalinze.

na sungura, Tz, - 21.04.08 @ 08:51 #7617

Bwana Ditopile apumzike kwa amani peponi. Wakikutana na dereva wa daladala ahera wasameheane. Viongozi wetu mafisadi wajifunze katika tukio hili. Mali, utajiri, ubinafsi, umwamba, ukuu wa mkoa, uwaziri, bastola, nk. pamoja na mwili wenyewe tunaoustarehesha mahotelini na vx landcruisers tutaviacha hapahapa duniani. Roho pekee itaenda mbele za haki. Ee Mungu uniumbie roho safi. Roho nyenyekevu na iliyopondeka ee Mungu hutaidharau.

na Christian - 21.04.08 @ 09:10 #7623

Mungu wa milele ni HAKIMU mwenye HAKI. Amependa kuiita kwake kesi ya mauaji ya maskini Mbonde aihukumu mwenyewe. Kila mmoja kati ya wahusika hawa wawili wamekutwa mauti wakiwa njiani. Mmoja akiwatafutia watoto wake riziki ya mlo mmoja kwa siku na mwingine akijimwaga na TV Hilux Hotel. Mmoja akiwa na kondakta wake na mwingine akiwa na mkewe (!!!) chumbani. Kwako Baba wa mbinguni tunaomba REHEMA. Kwako hakuna kujuana wala kupenyeza vijisenti. Kwako hakuna dereva wa daladala wala mkuu wa mkoa. Kwako sote tu binadamu uliotuumba kwa sura na mfano wako. UTUREHEMU, e Bwana.

na Muumini - 21.04.08 @ 09:16 #7626

KWANZA WAPO POLE SANA WAFIWA NA NAWAOMBA WAWE MUNGU AWAPE MOYO WA UVUMILIVU, KWA WAANDISHI NAONA MNAPOTOSHA KUSEMA ALIYEKUWA MKUU WA TABORA, ANDIKENI ALIYEWAHI KUWA MKUU WA TABORA.

na Mselema, TANZANIA, - 21.04.08 @ 09:57 #7641

Hizi habari eti Br. Ditto amekutwa na mauti akiwa na mkewe imetoka wapi? Mbona ukweli unapindishwa hata katika tukio tukufu la kifo! Bro. Ditto alikuwa na msichana mwingine chumbani pale Hilux hotel. Au kwa kuwa waislaimu waweza kuoa wake wengi basi msichana huyu anabambikiziwa kuwa mke ili kutunza heshima ya Ditto? Lakini ficho hili limekuja kwa kuchelewa maana hapa Morogoro hili jambo limeshakuwa gumzo mtaani, na chanzo cha habari hii ni hapohapo Hilux hotel. Yaleyale ya njia ya panda ya Bagamoyo na Kawe! Mwanamke katomea gizani baada ya kuona zali! Tumuachie Mungu, mkewe halali na familia yake. Apumzike kwa amani. Amina.

na Rashid, Kilakala, Morogoro., - 21.04.08 @ 10:15 #7645

Mshahara wa dhambi ni mauti.Ndo fundisho kwa wale wanaopenda kunyanyasa wengine kwa fedha,na kiburi na kupindisha sheria za nchi kwa kutumia fedha.Mungu aliona kabisa kesi hii mzee Dito angeshinda,hivyo ameamua kumwondoa asije tena akaua watanzania wengine,maana inawezekana angerudia kosa makusudi akijua sheria haina nguvu ya kumuhukumu.Mungu si Athumani hana upendeleo.ALAZWE HUKO WALIKOLAZWA WATU WA AINA YAKE WAKINA IDD AMINI DADA,SAMWEL DOE,ALDOLF HITLER,

na Marian, Germany, - 21.04.08 @ 10:17 #7646

Allah ametuleta duniani kwanjia anayoijua yeye Mfalme wa ardhi na mbingu.Anajua tulilolijua, kwanini Dito amemchukua, wewe na mimi tutaondokaje ni yake yeye. Alijua dereva Mbonde alivyomchukua. Tuwaombee awalaze pema peponi.Tuliobaki tusiwe mashetani kwa kuhukumu uwezo wa Allah. ''INALILAH WAINAHILAH RAJUHUUN''

na Makalo B. , Tnga, Tz, - 21.04.08 @ 10:28 #7650

Kweli tujifunze kutoka kwa Ditto. duniani uongo mwingi,rushwa,ukubwa kwa MUNGU wote sawa haki haipotei tusali na tutende mema siku zote Mungu atusaidie

na ALEX PETER, MBEYA, - 21.04.08 @ 10:51 #7708

Jamani tusipende kuhukumu wenzetu wapokufa mimi na wewe hatujui tutakufaje na tunasahau neno la mungu linasema tusameheane na usihukumu usije ukahukumiwa.

na mwenda kwao, porini, - 21.04.08 @ 08:28 #7718


kwa niaba ya
Ulimboka Tuntufye,
Technical Training Supervisor- Process and Services,
Geita Gold Mine Ltd,
P.O.Box 532,
Geita - Mwanza.
Phone:- +255 (0) 28 2520 500 Ext. 1261
Cell phone:- + 255 (0) 755 37 12 19

Friday, April 4, 2008

Habari zilizotufikia hivi punde ndege aina ya sessna imeangukauwanja wa ndege wa mwanza muda si mrefu na kuua watu wote na hakuna aliepona,,katika ndege hiyo kulikuwapo watanzania na wacanada,,mpaka sasa tunavyoandika maiti bado zina tolewa vipendevipande, ,mwenyezi mungu awalaze mahali pema peponi

Monday, March 31, 2008

SERIKALI YA MSETO ISIISHIE TANZANIA VISIWANI JAMANI

Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu yenu Wanazuoni.



Nikiwa natafakari juu ya vikao vya chama twawala, CCM, limenijia wazo kwamba, kwa madokezo tuliyopata, vikao hivyo muhimu vitajadili mambo muhimu likiwamo la muafaka wenye lengo la kumaliza mpasuko wa kisiasa (kijamii, kiuchumi nk) huko Tanzania Visiwani. Jambo kubwa linaloonekana kuwa mwarobaini wa mpasuko huo ni kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, kama ambavyo tulishadokezwa.


Hizo kwangu, ni habari njema sana. Ninaamini kwamba katika ulimwengu wa kisasa, siasa haina budi kuwa ya 'kisasa'. kwa hiyo ni vema basi tuache kubaguana, bali tukae pamoja tuijenge nchi yetu. Kenya mseto umeonekana na unaelekea kumaliza tafrani ya hivi karibuni, vivyo hivyo Afrika kusini, amani iliyofuatia Uhuru wa nchi hiyo imetokana na kukubali kuishi na kutawala pamoja.

hoja yangu ya msingi basi ni kwamba, kwa vile vikao vitakavyofanyika buti ama vya ccm ndivyo vikao muhimu zaidi vya chama kinachotawala, visiishie katika kujadili uwezekano wa kuundwa kwa serikali ya mseto huko visiwani. bali vikao hivyo viende hatua moja mbele ya kujadili uwezekano wa kuwa na serikali ya mseto kwa tanzania nzima. mseto ukiwa halali upande mmoja wa taifa hili, kwanini uwe haramu katika ngazi nyingine? ikiwa mseto umeoneka mwarobaini wa matatizo ya kisiasa mahali pengine, kwani 'kisiwa cha amani kisitazame mbele na kuufanya kuwa kinga ya matatizo yanayoweza kutokea na kukifanya kisiwa cha machafuko? isitoshe hili, litawatoa hofu baadhi wahafidhina wa visiwani wanaodhani wao tu ndiyo waliyozaliwa kwa ajili ya kutawala. wakati umefika vikao hivyo viwe pro active. tusingoje yatokee yaliyotokea zanzibar, ama kenya, ndiyo tufikiri mseto. umamkini wa ccm utajidhihirisha siyo kwa hotuba, porojo, propaganda, uzandiki n.k, bali kwa kutazama mbele.

TUFANYEJE SASA?
mimi nimeandika ujumbe mfupi wa simu ufuatao kwa mjumbe wa nec wa mkoa wangu, "mhenshimiwa mnec wa mkoa wangu mshikamoo. nadhani ni wakati sasa mtakapojadili suala la serikali ya mseto zanzibar, msiishie hapo, mwende hatua zaidi, muibue mjadala wa kitaifa, jamhuri ya muungano ya tanzania iwe na serikali ya umoja wa kitaifa/mseto kuanzia uchaguzi ujao. kikao chema."

WITO:
Mwanazuoni mwenzangu, mtumie mjumbe wa NEC yeyote unayemfahamu SMS yenye ujumbe kama huo, ikiwa unaamini katika serikali ya pamoja, ambayo uwezekano wake KUWEKA MASLAHI YA TAIFA MBELE NI MKUBWA ZAIDI. Kwa kutuma SMS hiyo tunaweza kuwa tumeanzisha mchakato muhimu sana kwa mustakabali mwema wa taifa letu

NAWASILISHA.


Kwa niaba ya
ADAM, L

Wizara ya MiundoMbinu inafanya nini?

Hii ni Mvua ya siku moja Dar Je! ingeendelea kunyesha kwa muda wa wiki moja sii ni kiama tena? Sababu kama mifereji ya kupelekea maji imeziba na wizara zinakodolea macho nini kinafuata mvua kama hii ikiendelea kwa wiki nzima.




Wednesday, March 26, 2008

Raisi Mstaafu Mkapa hamuelewi Raisi Kikwete!

Mkapa hamuelewi Kikwete, unaweza ukaona ni kama mchezo flani wa kuigiza lakini ukweli ni kwamba yanaendelea huko nyuma ya pazia ni mazito kuliko yale ambayo tunayaona na kuyasikia hata pale Habari maelezo na hali ni ya kutoaminiana hadi leo hii !

Wakati Rais Kikwete, Anaingia madarakani si kwamba alikuwa mgeni na serikali aliyokuwa anaifanyia kazi na ambayo angekuwa ndio kiongozi wake muda ule alipoingia rasmi kama Rais wa nchi, Hakuwa mgeni alikuwa anayaelewa mambo ya kifisadi yote yaliyokuwa yanaendelea hata kama naye atakuwa ni mmoja wa wahusika kama ambavyo mnyororo unavyoonyesha !

Ili kuendelea na Serikali yake safi na kutoa mambo yote ya kifisadi ambayo Watu wake wa karibu walikuwa wanamweleza kuhusu Mkapa na kama mlivyokuwa mnajua kuwa Kikwete hakua chaguo la Mkapa basi aliamua kuunda kikundi chake cha siri ambacho kilianika mambo yote ya Mkapa na kumletea kila Data za Mkapa na Kikwete akaa nazo !

Katika hali ambayo hata mwenyewe Mkapa alishangaa ni pale ,Alipomuita yule Mama Anna Mkapa siku moja pale Ikulu na kumuonyesha utitiri wa malimbikizo ya mali ambayo yule Mama pamoja ama kwa kutumia cheo cha Mumewe Mkapa aliamua kutumia kila njia na kuikamua nchi ,Ikiwa ni pamoja na sakata zima la makabidhiano la TASAF !

Baada ya Mama Anna Mkapa kukataa kuiacha pale Ikulu ,Kikwete alituma Jamaa wake waifuatilie na kuifumua kwa kuifanyia "ODITING" ya nguvu hadi walipogundua kuwa yule Mama alikwisha kuumaliza ule Mfuko na masurufu yake !

Alipomuita alimuonyesha kila kitu kuhusu TASAF, na yule Mama wa watu akabaki hana la kusema ,kwani aliombwa tu aendelee na safari zake na kumuachia jamaa afikirie namna ya kufanya !

Aliyomuonyesha yalimtoa yule Mama jasho Achilia yale Magorofa ya Kariakoo aliyonayo, wala ile hotel ya Lamada aliyojinyakulia pale Ilala karibu na Msimbazi center, Alionyeshwa ubadhirifu wote alioufanya kwa kutumia cheo cha Mumewe kama Rais.Mkapa hamuelewi Kikwete, unaweza ukaona ni kama mchezo flani wa kuigiza lakini ukweli ni kwamba yanaendelea huko nyuma ya pazia ni mazito kuliko yale ambayo tunayaona na kuyasikia hata pale Habari maelezo na hali ni ya kutoaminiana hadi leo hii !

Wakati Rais Kikwete, Anaingia madarakani si kwamba alikuwa mgeni na serikali aliyokuwa anaifanyia kazi na ambayo angekuwa ndio kiongozi wake muda ule alipoingia rasmi kama Rais wa nchi, Hakuwa mgeni alikuwa anayaelewa mambo ya kifisadi yote yaliyokuwa yanaendelea hata kama naye atakuwa ni mmoja wa wahusika kama ambavyo mnyororo unavyoonyesha !

Ili kuendelea na Serikali yake safi na kutoa mambo yote ya kifisadi ambayo Watu wake wa karibu walikuwa wanamweleza kuhusu Mkapa na kama mlivyokuwa mnajua kuwa Kikwete hakua chaguo la Mkapa basi aliamua kuunda kikundi chake cha siri ambacho kilianika mambo yote ya Mkapa na kumletea kila Data za Mkapa na Kikwete akaa nazo !

Katika hali ambayo hata mwenyewe Mkapa alishangaa ni pale ,Alipomuita yule Mama Anna Mkapa siku moja pale Ikulu na kumuonyesha utitiri wa malimbikizo ya mali ambayo yule Mama pamoja ama kwa kutumia cheo cha Mumewe Mkapa aliamua kutumia kila njia na kuikamua nchi ,Ikiwa ni pamoja na sakata zima la makabidhiano la TASAF !

Baada ya Mama Anna Mkapa kukataa kuiacha pale Ikulu ,Kikwete alituma Jamaa wake waifuatilie na kuifumua kwa kuifanyia "ODITING" ya nguvu hadi walipogundua kuwa yule Mama alikwisha kuumaliza ule Mfuko na masurufu yake !

Alipomuita alimuonyesha kila kitu kuhusu TASAF, na yule Mama wa watu akabaki hana la kusema ,kwani aliombwa tu aendelee na safari zake na kumuachia jamaa afikirie namna ya kufanya !

Aliyomuonyesha yalimtoa yule Mama jasho Achilia yale Magorofa ya Kariakoo aliyonayo, wala ile hotel ya Lamada aliyojinyakulia pale Ilala karibu na Msimbazi center, Alionyeshwa ubadhirifu wote alioufanya kwa kutumia cheo cha Mumewe kama Rais.

Bonyeza hapa

Vyama korija, demokrasia sufuri

RAI YA JENERALI


NIMEKWISHA kueleza huko nyuma jinsi Mwalimu Julius Nyerere alivyotaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kigawanyike ili viwepo vyama viwili vyenye nguvu karibu sawa ingawa vikitofautiana kuhusu masuala ya itikadi, sera na mbinu za utekelezaji.

Mantiki ya mtazamo wa Mwalimu ilijengeka juu ya uelewa aliokuwa nao kuhusu siasa za ushindani. Kwa mtazamo wake, hakuna maana ya kuwa na mfumo unaoitwa wa “vyama vingi” lakini wakati huo huo ukajenga utaratibu ambao hauruhusu upinzani wa maana.

Nyerere hakufanikiwa katika hilo, na chama chake kikaendelea kuwa kimoja na chenye nguvu kubwa miongoni mwa jamii. Umoja huu na nguvu hiyo havitokani na makubaliano ya kiitikadi wala maelewano au mwafaka kuhusu masuala makuu ya kitaifa.

Ukweli ni kwamba hakuna makubaliano ya kiitikadi kwa sababu katika chama kisichokuwa na itikadi kuu si rahisi kupata ukinzani kwani ukinzani huzuka kutokana na itikadi inayobishiwa na kundi fulani, na bila ukinzani haiwezekani yakawapo makubaliano.

Hali kadhalika, kwa mwafaka kuhusu masuala makuu ya kitaifa. Kiongozi mmoja wa chama hicho aliwahi kusema, mara tu baada ya uchaguzi kwisha, kwamba ilani ya chama chake, ambayo ndiyo ilipelekwa kwa wananchi wakamchagua, haitekelezeki. Maana halisi ya tamko lake hilo ni kwamba ilani ni ujanja unaobuniwa wa kuwazuga wapiga kura kwa kuwahadaa na ahadi nyingi ambazo hao wanaozitoa wanajua fika kwamba hawana nia ya kuzitimiza.

Kama hiyo ni kweli, basi hakuna njia ya kupata mwafaka kuhusu suala lo lote la kitaifa, kwa sababu hata hayo tuliyoyaorodhesha kwamba ni mambo yatakayopewa kipaumbele ni kiinimacho tu. Katika hali kama hiyo programu huzuka kutegemea na viongozi wakuu wanavyojihisi kwa wakati huo, na utekelezaji huwa daima ni wa zima-moto. Hapo haiwezekani kuwa na mwafaka wa kiutaratibu wala ukinzani ulioaratibiwa.

Kimsingi, Chama cha Mapinduzi kimeendelea kuwa kimoja kwa sababu bado kiko madarakani, na kimekuwa kikitumia madaraka ya dola kuendesha kazi zake za kichama. Mifano michache inaweza kusaidia kueleza ninachokisema hapa:

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri anapopanda ndege ya Serikali kwenda mikoani kukagua miradi ya maendeleo, na akiwa huko akaendesha mikutano ya chama chake, tunaweza kusema kwamba chama chake kinakuwa kimepokea ruzuku kutoka serikalini kwa maana ya usafiri, malazi, chakula, na vinywaji. Aidha, katika misafara hiyo anaambatana na maofisa kadhaa wa chama chake, ambao nao hudandia ‘takrima’ iliyoandaliwa kwa ajili ya Rais.

Hali ni hiyo hiyo inapoandaliwa ziara ya Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar, Waziri Kiongozi na mawaziri wa kila aina, pamoja na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Zaidi ya hayo tuongeze utaratibu unaotumika wa kuwateua maofisa waandamizi wa chama-tawala kuwa mawaziri wanaolipwa na Serikali, wanaosafiri kwa magari ya Serikali, n.k.

Tungeweza kupiga mahesabu yaliyotulia tungegundua kwamba Serikali ya Tanzania inatoa ruzuku kwa CCM bila kukiri hivyo. Na tukumbuke kwamba ruzuku hii ni mbali kabisa na ile inayotolewa kwa kila chama kulingana na wingi wa kura kilizopata katika uchaguzi wa Rais na wingi wa wabunge wa chama husika, huko nako chama-tawala kimetwaa mgao wa simba.

Hivi sasa iko minong’ono ambayo haikosi chembe ya ukweli kwamba hata baadhi ya masuala yanayoibuka kuhusu ‘ufisadi’ katika asasi nyeti za Taifa yametokana na chama-tawaka kuchotewa fedha kutoka asasi hizo kwa ajili ya kampeni za uchaguzi. Ni dhahiri kwamba chama hicho kimeegemea mno Serikali kiasi kwamba ni vigumu kukifikiria kikiendelea kuwapo iwapo, kwa sababu yo yote ile, kingepoteza madaraka.

Kikiwa kinaendelea kuwa madarakani kitaendelea kuvuta kila aina ya watu, wema na waovu, waongofu na mafisadi, wazalendo na wahaini, alimradi chama bado ni chimbuko la neema, ndicho kitovu cha mgawanyo wa madaraka ya dola katika ngazi zote, na kituo cha kushamirisha biashara za wanachama waaminifu.

Kuhusu suala la mlolongo wa viongozi na watawala waliopewa madaraka mbalimbali kutokana na kuwa waaminifu kwa chama-tawala, sehemu ya Zanzibar huwa naiona kama kichekesho.

Hivi kuna sababu gani hasa kwa kisiwa kisichokuwa na ukubwa wa mkoa mmoja wa Tanzania Bara (Tanganyika) kuwa na Rais, Waziri Kiongozi, Naibu Waziri Kiongozi, mawaziri dazeni na naibu mawaziri korija, makatibu wakuu wa wizara, naibu makatibu wakuu, wakurugenzi, naibu wakurugenzi, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, masheha, n.k. Inaelekea Visiwa hivyo vina viongozi wengi kuliko raia.

Lakini hata upande wa Tanzania Bara hali si tofauti sana kama tukiangalia mlololongo wa mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu na manaibu wao, wakurugenzi, wakuu wa mikoa, maofisa utawala wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa wilaya, watendaji wa tarafa na kata, hadi wenyeviti na makatibu wa vijiji.

Dhahiri, hii ni nchi inayotawaliwa kupindukia (over-governed) ingawaje maendeleo hayaonekani kwa uwiano unaofanana na ukubwa wa utawala. Dhahiri vile vile, watu wengi watakusanyika katika chombo kinachotoa fursa ya kushiriki katika hilo ‘Treni la Michuzi’ kwa sababu kuna ajira kwa ajili ya watu wengi. Hata wasiokuwa waumini wa jambo lo lote wataimba wimbo wo wote unaowahakikishia kipato kinono na maisha nafuu.

Sasa, kutokana na ukubwa wa chama, udhibiti kilichonao juu ya rasilimali za Taifa na mkusanyiko wa kimaslahi wa watu wa kila aina na tabia (silika ya kokolo), chama kimejiundia chenyewe matatizo ambayo hakikutaraji yangechukua sura iliyokuja kujitokeza. Hapa napo, kwa mara nyingine, tena, tunakutana na ile sheria ya matokeo yasiyotarajiwa (unintended consequences). Hebu tuangalie kilichotokea bila kutarajiwa.

Mwalimu Nyerere alisema kwamba hakuna mantiki ya kuwa na mfumo unaoitwa wa “vyama vingi” bila kuwa na vyama vya kweli. Wakuu wa CCM walikuwa na mawazo mengine. Walikwisha kuona jinsi walivyosumbuliwa na kile kilichoitwa G-55 wakati wa chama kimoja. Sasa, ujio wa vyama vingi uliwapa fursa ambayo waliiona kama fursa ya dhahabu.

Ni hivi: Wakati wa chama kimoja, kwa kutumia nadharia ya ubishani ndani ya chama, iliwezekana kuwa na kundi la wabunge wa chama tawala linaloipinga serikali katika masuala kadhaa na likavumiliwa, kwa sababu tulikuwa tumekumbatia nadharia ya demokrasi katika chama kimoja. Kundi la wabunge kama hao walionekana kama wanaotoa mchango muhimu katika kuifanya serikali ifanye kazi yake, na kwa maana hii lilikuwa ni kundi la upinzani usio rasmi.

Lakini baada ya kuingia katika “vyama vingi” kazi hiyo ya upinzani ilikabidhiwa rasmi kwa vyama vya upinzani, na kwa hiyo wabunge wa CCM walikuwa hawana tena nafasi ya kusimama bungeni na kukosoa serikali, hata kwa jambo ambalo hata kipofu angeona kwamba ni hovyo. Wakuu wa chama walisikika wakisema (katika kipindi cha maandalizi ya ujio wa “vyama vingi”) wakituambia baadhi yetu:

“Sasa tutawaona. Vyama vingi vinakuja, na huo ndio mwisho wenu. Ukisema fyoo dhidi ya serikali yako unapigwa ‘whip’ hata tatu. Mtakoma.”

Kwa maneno mengine nao pia walikuwa wamegundua ile sheria yangu ya matokeo yasiyotarajiwa: Kwamba lile wingu la “vyama vingi” (ambalo liliwatisha mno) lilikuwa na msitari wa fedha: Tofauti na walivyokuwa wakihofu (kwamba mfumo wa vyama vingi vingeleta demokrasia) sasa wakawa wamegundua kwamba mfumo huo ungesaidia kuua hata kale ka-demokrasia kalikokuwa kamejengeka ndani ya mfumo wa chama kimoja. Na hili wakalifanyia kazi kwa ari kubwa ili kuhakikisha kwamba “vyama vingi” maana yake ni kutokuwa na demokrasia

Walikosea sana.

Itaendelea

Raia Mwema ( Jenerali Ulimwengu)