Tuesday, April 22, 2008

Maoni ya Watanzania

Pole jamaa wote wa Dito na CCM kwa ujumla,lakini hiyo ni njia ya wote na yeye Dito katangulia nasi tupo nyuma.TANGULIA BABA!NENDA BABA!wasalimie JK wa Butiama na umwambie TZ inayumbishwa na JK wa Chalinze.

na sungura, Tz, - 21.04.08 @ 08:51 #7617

Bwana Ditopile apumzike kwa amani peponi. Wakikutana na dereva wa daladala ahera wasameheane. Viongozi wetu mafisadi wajifunze katika tukio hili. Mali, utajiri, ubinafsi, umwamba, ukuu wa mkoa, uwaziri, bastola, nk. pamoja na mwili wenyewe tunaoustarehesha mahotelini na vx landcruisers tutaviacha hapahapa duniani. Roho pekee itaenda mbele za haki. Ee Mungu uniumbie roho safi. Roho nyenyekevu na iliyopondeka ee Mungu hutaidharau.

na Christian - 21.04.08 @ 09:10 #7623

Mungu wa milele ni HAKIMU mwenye HAKI. Amependa kuiita kwake kesi ya mauaji ya maskini Mbonde aihukumu mwenyewe. Kila mmoja kati ya wahusika hawa wawili wamekutwa mauti wakiwa njiani. Mmoja akiwatafutia watoto wake riziki ya mlo mmoja kwa siku na mwingine akijimwaga na TV Hilux Hotel. Mmoja akiwa na kondakta wake na mwingine akiwa na mkewe (!!!) chumbani. Kwako Baba wa mbinguni tunaomba REHEMA. Kwako hakuna kujuana wala kupenyeza vijisenti. Kwako hakuna dereva wa daladala wala mkuu wa mkoa. Kwako sote tu binadamu uliotuumba kwa sura na mfano wako. UTUREHEMU, e Bwana.

na Muumini - 21.04.08 @ 09:16 #7626

KWANZA WAPO POLE SANA WAFIWA NA NAWAOMBA WAWE MUNGU AWAPE MOYO WA UVUMILIVU, KWA WAANDISHI NAONA MNAPOTOSHA KUSEMA ALIYEKUWA MKUU WA TABORA, ANDIKENI ALIYEWAHI KUWA MKUU WA TABORA.

na Mselema, TANZANIA, - 21.04.08 @ 09:57 #7641

Hizi habari eti Br. Ditto amekutwa na mauti akiwa na mkewe imetoka wapi? Mbona ukweli unapindishwa hata katika tukio tukufu la kifo! Bro. Ditto alikuwa na msichana mwingine chumbani pale Hilux hotel. Au kwa kuwa waislaimu waweza kuoa wake wengi basi msichana huyu anabambikiziwa kuwa mke ili kutunza heshima ya Ditto? Lakini ficho hili limekuja kwa kuchelewa maana hapa Morogoro hili jambo limeshakuwa gumzo mtaani, na chanzo cha habari hii ni hapohapo Hilux hotel. Yaleyale ya njia ya panda ya Bagamoyo na Kawe! Mwanamke katomea gizani baada ya kuona zali! Tumuachie Mungu, mkewe halali na familia yake. Apumzike kwa amani. Amina.

na Rashid, Kilakala, Morogoro., - 21.04.08 @ 10:15 #7645

Mshahara wa dhambi ni mauti.Ndo fundisho kwa wale wanaopenda kunyanyasa wengine kwa fedha,na kiburi na kupindisha sheria za nchi kwa kutumia fedha.Mungu aliona kabisa kesi hii mzee Dito angeshinda,hivyo ameamua kumwondoa asije tena akaua watanzania wengine,maana inawezekana angerudia kosa makusudi akijua sheria haina nguvu ya kumuhukumu.Mungu si Athumani hana upendeleo.ALAZWE HUKO WALIKOLAZWA WATU WA AINA YAKE WAKINA IDD AMINI DADA,SAMWEL DOE,ALDOLF HITLER,

na Marian, Germany, - 21.04.08 @ 10:17 #7646

Allah ametuleta duniani kwanjia anayoijua yeye Mfalme wa ardhi na mbingu.Anajua tulilolijua, kwanini Dito amemchukua, wewe na mimi tutaondokaje ni yake yeye. Alijua dereva Mbonde alivyomchukua. Tuwaombee awalaze pema peponi.Tuliobaki tusiwe mashetani kwa kuhukumu uwezo wa Allah. ''INALILAH WAINAHILAH RAJUHUUN''

na Makalo B. , Tnga, Tz, - 21.04.08 @ 10:28 #7650

Kweli tujifunze kutoka kwa Ditto. duniani uongo mwingi,rushwa,ukubwa kwa MUNGU wote sawa haki haipotei tusali na tutende mema siku zote Mungu atusaidie

na ALEX PETER, MBEYA, - 21.04.08 @ 10:51 #7708

Jamani tusipende kuhukumu wenzetu wapokufa mimi na wewe hatujui tutakufaje na tunasahau neno la mungu linasema tusameheane na usihukumu usije ukahukumiwa.

na mwenda kwao, porini, - 21.04.08 @ 08:28 #7718


kwa niaba ya
Ulimboka Tuntufye,
Technical Training Supervisor- Process and Services,
Geita Gold Mine Ltd,
P.O.Box 532,
Geita - Mwanza.
Phone:- +255 (0) 28 2520 500 Ext. 1261
Cell phone:- + 255 (0) 755 37 12 19