Friday, February 29, 2008

TBS INATUKWAZA

Hakuna kitu kinachovutia kama unapoenda dukani kununua kitu ukakuta kitu hicho ndio kile kile unachotaka wewe na ubora ni ule ule ulioutegemea kutokana na matangazo uliyoyaona yanayohusu bidhaa hiyo .

Pia hakuna kitu kinacholeta huzuni unapoenda dukani kununua kitu ukaambiwa ni bora kabisa , na ndicho hicho unachotaka na ulitegemea kutokana na tangazo hilo hilo .

Lakini kitu hicho kina baadhi vya vifaa vimebadilishwa au kuwekewe vingine ambavyo havina ubora unaotakiwa na havikidhi matajio yako na masoko yako .

Wewe hujui kwa sababu ni mtumiaji tu huwezi kukagua ndani kujua vitu vingine zaidi au labda wakati unaenda hukupata ushauri kutoka kwa wataalamu wakuambie hili na lile wewe umeenda tu .

Na ndio hivyo umeshanunua kitu hicho umetumia miezi 2 kitu kimekufa data zako kule ndani zimepotea , ukifungua ndani katika hicho kifaa kuna maandishi pale HATUHUSIKI NA UPOTEVU WA DATA ZAKO umeshauwawa tena .

Ukienda dukani unaambiwa kifaa chako kimepata matatizo ya umeme kwahiyo hatulipi vitu vinavyokufa kwa sababu za umeme , unachotakiwa ni kununua vingine .

Haya sasa umeamua kuonana na wataalamu wanaiangalia , wale wanaojua zaidi wataenda katika mtandao kuangalia serial number ya hicho kifaa chako kama kweli kimetengenezwa na kampuni husika .

Unagundua kwamba HP COMPAQ hawana bidhaa yenye serial number zilizoko katika computer hiyo , ukiangalia model hiyo huwa inakuja na HDD za aina gani , unakuta HP COMPAQ original huwa zinakuja na HDD za aina Fulani ambazo katika ile yako sio ile .

Sasa utaenda kulalamika wapi ? ukienda TBS hakuna wa kukusikiliza au unatakiwa uandike maelezo marefu sana , huwezi kwenda kushitaki wakati mwingine kwa sababu hawa wadosi si unawajua wewe mwenyewe ndio unaweza kuumbuka .

TBS inatakiwa iwe macho sana na hizi bidhaa bandia zinazoingizwa nchini bila kufuatilia maadili ya bidhaa hizi na hata mashirika ya umma yanaponunua bidhaa hizi basi wahakikishe taasisi za kudhibiti ubora wanaangalia nakujua ubora au na kama zinakidhi mahitaji ya sehemu husika .
TBS iweke mambo yake wazi jinsi inavyoshugulikia mambo haya yanayohusu vifaa hivi , watoe namba zao wazi , emails na kadhalika iwe rahisi watu kuwasiliana nao zinapotokea shida kama hizi .

Unaona kama hapo juu umenunua bidhaa ya hp ambayo ni bandia hakuna wa kumlalamikia zaidi ya hp wenyewe , na wenyewe watasema hatuyatambui maduka hayo yanayouza hizo bidhaa na hatuna mkataba nao wowote ule .