Monday, February 18, 2008

Karibu Raisi Bush















Raisi George Bush wa Marekani akiwa ameongozana na mkewe wamewasili katika Kiwanja cha Ndege jijini Dar es Salaam

"Sema mwanahabari “
“ Shetani anakuja saa ngapi ?”
“ unaonaje msimamo wa waisilamu ?”

Huyo ni rafiki yangu mmoja alinipigia simu jana usiku katika maongezi yetu kwanza alianza kwa maneno na maswali hayo hapo juu , mimi nilibaki nimeduwaa tu kwanini anamwita bush shetani .

Sikutilia maanani sana anavyomuita bush shetani , kwa sababu hilo neno sasa limeshakuwa la kawaida na ni propaganda tu kama zingine , nilishituka alivyoniuliza kuhusu msimamo wa waisilamu katika suala zima la ujio wa bush .

Nilimwambia maneno machache kwanza atambue Tanzania ni nchi ambayo haina dini , ni nchi huru na watu wake wako huru , mtu anaweza kusema na kuongea chochote bila kuzuiwa ili mradi asivunje sheria za sehemu husika kila sehemu inasheria zake kutegemea na eneo alipo msikitini , kanisani , jamatini kila sehemu na lake .

Kwa kuwa watu wake wako huru , hata waisilamu nao wako huru kusema kile wanachotaka , kama wamekifanyia utafiti na kuwa na uhakika nacho na kwa uhakika walifanya maandamano jana kuelezea hisia zako kuhusu sera za taifa hilo za kimataifa .

Inawezekana hata leo wakaandamana tena kwa sababu hatujui jana walikubaliana nini baada ya maandamano yao , kwahiyo tusiwapuuze tu na kuacha mambo haya yafe hivi hivi .

Kama taifa lazima lifikirie kilio cha hawa waisilamu wachache kwa sababu ni sehemu ya Tanzania , kizazi hichi kitakuwa na fikira hizo na chuki hizo dhidi ya taifa la marekani kwa miaka mingi ijayo , mfano niliona moja ya malalamiko yao ni kuhusu baadhi ya masheikh kukamatwa na miradi yao kufungwa

Je nani anapenda miradi kama ya zahanati , shule na maendeleo mengine zifungwe kwa sababu ambazo haziko wazi kama hawa waisilamu wanavyojaribu kusema ? wao wanahusisha hayo na bush .

Pamoja na yote haya waisilamu wasimlaumu bush na serikali yake kwanza wajiulize kuhusu hawa masheikh wao waliokamatwa kama wanavyosema na miradi yao iliyofungwa , waweke mbali hisia zao za kidini watuambie hawa mashekh ni kina nani na ni mali ghani za waisilamu zilizofungwa au kusimamishwa .

Wasipokuwa wazi basi tutaendelea kuamini kwamba tatizo sio bush tatizo ni la waisilamu wenyewe na mambo yao , haswa hivi vikundi vichache , na hivi ndio vikundi ambavyo vilituletea balaa uwanja wa taifa katika sakata la kwenda mecca .

Hivi vikundi lazima tuwe navyo makini sana , na tuviangalie kwa karibu wasiposikilizwa wanaweza kuanza kulipa visasi kama tunavyoona katika nchi zingine haswa mashariki ya kati