Monday, March 31, 2008

SERIKALI YA MSETO ISIISHIE TANZANIA VISIWANI JAMANI

Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu yenu Wanazuoni.



Nikiwa natafakari juu ya vikao vya chama twawala, CCM, limenijia wazo kwamba, kwa madokezo tuliyopata, vikao hivyo muhimu vitajadili mambo muhimu likiwamo la muafaka wenye lengo la kumaliza mpasuko wa kisiasa (kijamii, kiuchumi nk) huko Tanzania Visiwani. Jambo kubwa linaloonekana kuwa mwarobaini wa mpasuko huo ni kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, kama ambavyo tulishadokezwa.


Hizo kwangu, ni habari njema sana. Ninaamini kwamba katika ulimwengu wa kisasa, siasa haina budi kuwa ya 'kisasa'. kwa hiyo ni vema basi tuache kubaguana, bali tukae pamoja tuijenge nchi yetu. Kenya mseto umeonekana na unaelekea kumaliza tafrani ya hivi karibuni, vivyo hivyo Afrika kusini, amani iliyofuatia Uhuru wa nchi hiyo imetokana na kukubali kuishi na kutawala pamoja.

hoja yangu ya msingi basi ni kwamba, kwa vile vikao vitakavyofanyika buti ama vya ccm ndivyo vikao muhimu zaidi vya chama kinachotawala, visiishie katika kujadili uwezekano wa kuundwa kwa serikali ya mseto huko visiwani. bali vikao hivyo viende hatua moja mbele ya kujadili uwezekano wa kuwa na serikali ya mseto kwa tanzania nzima. mseto ukiwa halali upande mmoja wa taifa hili, kwanini uwe haramu katika ngazi nyingine? ikiwa mseto umeoneka mwarobaini wa matatizo ya kisiasa mahali pengine, kwani 'kisiwa cha amani kisitazame mbele na kuufanya kuwa kinga ya matatizo yanayoweza kutokea na kukifanya kisiwa cha machafuko? isitoshe hili, litawatoa hofu baadhi wahafidhina wa visiwani wanaodhani wao tu ndiyo waliyozaliwa kwa ajili ya kutawala. wakati umefika vikao hivyo viwe pro active. tusingoje yatokee yaliyotokea zanzibar, ama kenya, ndiyo tufikiri mseto. umamkini wa ccm utajidhihirisha siyo kwa hotuba, porojo, propaganda, uzandiki n.k, bali kwa kutazama mbele.

TUFANYEJE SASA?
mimi nimeandika ujumbe mfupi wa simu ufuatao kwa mjumbe wa nec wa mkoa wangu, "mhenshimiwa mnec wa mkoa wangu mshikamoo. nadhani ni wakati sasa mtakapojadili suala la serikali ya mseto zanzibar, msiishie hapo, mwende hatua zaidi, muibue mjadala wa kitaifa, jamhuri ya muungano ya tanzania iwe na serikali ya umoja wa kitaifa/mseto kuanzia uchaguzi ujao. kikao chema."

WITO:
Mwanazuoni mwenzangu, mtumie mjumbe wa NEC yeyote unayemfahamu SMS yenye ujumbe kama huo, ikiwa unaamini katika serikali ya pamoja, ambayo uwezekano wake KUWEKA MASLAHI YA TAIFA MBELE NI MKUBWA ZAIDI. Kwa kutuma SMS hiyo tunaweza kuwa tumeanzisha mchakato muhimu sana kwa mustakabali mwema wa taifa letu

NAWASILISHA.


Kwa niaba ya
ADAM, L

Wizara ya MiundoMbinu inafanya nini?

Hii ni Mvua ya siku moja Dar Je! ingeendelea kunyesha kwa muda wa wiki moja sii ni kiama tena? Sababu kama mifereji ya kupelekea maji imeziba na wizara zinakodolea macho nini kinafuata mvua kama hii ikiendelea kwa wiki nzima.