Tuesday, February 12, 2008

BUNGE LA TUKUFU LA TANZANIA:

MWENYEKITI TUME TEULE YA BUNGE: "Waziri Mkuu ameshiriki katika kuibeba Richmond" pwa pwa pwa pwaaaaaaaaaaaaaaa MAKOFIIIII (JANA

WAZIRI MKUU : "Nimemwandikia Rais barua ya kubwaga manyanga. Lakini sikubaliani kabisa na taarifa ya Kamati Teule ya Bunge. Ni mambo ya siasa za Dar Dar es Salaam. Kwanini wasinihoji. Wamenionea.. ..." Pwa pwa pwa pwaaaaaaaaaaaaaaa MAKOFIIIII (LEO)

BUNGE LETU HILO, BWANA

WACHA NA TUSIKIE MJADALA JIONI NDANI YA JUMBA. NA TUSIKIE RAIS ANASEMAJE. LAKINI YOTE KWA YOTE,KAMATI IMETIMIZA WAJIBU WAKE BARA BARA. NA WAZIRI MKUU KACHUKUA HATUA MUAFAKA (Hata kama kwa kuchelewa maana kelele zilishakuwa nyingi juu ya Waziri Mkuu. BADO LA MVUA YA 'WAGANGA WA THAILAND???? )

Nawasilisha

Hizi ndizo amri kumi za Tanzania, kama unataka kuinusuru Tanzania isiuzwe inakubidi izufuate:-
1. Usiwe mlaghai kama Karamagi

2. Usiwe fisadi kama Balali

3. Usiwe mbishi kama Zitto

4. Usiwe makelele kama Makamba

5. Usiwe mbabe kama Sitta

6. Usihukumu kama Mudhihiri

7. Usiuwe kama Ditopile

8. Usidandie hoja kama Mrema

9. Onea huruma nchi kama Dr. Slaa

10. Usiwe na tamaa kama Lowasa

Tanzania ya Nyerere: Mafunzo ya maendeleo, umoja na amani

Mgomo wa 6 wa Wanawake Duniani – Machi 8 2005
Wapendwa ndugu zangu,
Komesha Umasikini na Vita – Wekesha katika Kutunza na siyo Mauaji!
Malipo kwa kazi zetu na sawazisha malipo kwenye soko la Dunia
Kila iliposherehekewa Siku ya Kimataifa tangu Mwaka 2000,Wanawake katika zaidi ya Mataifa 60 wametumia kila hatua za pamoja kuanzia ngazi ya chini wakiitaka jamii iwekeze katika kutunza badala ya mauwaji, na kwamba fedha zinazoharibiwa kugharimia vita zingetumiwa badala yake kutimiliza mahitaji ya jamii. Mgomo huu umezidi kua imara katika kipindi cha miaka mitano,hususan katika Mataifa ya kusini mwa Dunia, ambapo wanawake na pia idadi ya wanaume inayozidi kuongezeka, kwa pamoja wanazingatia hatua hizi kila kukicha. Tumejionea jinsi manufaa ya ushirikiano wa kimatifa bila kujali mipaka .

Kupinga vita na kukomesha umasikini ni masuala mawili yasiyotengeka. Janga la hivi karibuni la Tsunami liliua karibu ya watu 300,000, lakini kila siku watu wanauawa kwa njaa,magonjwa, joto linalosababishwa na uharibifu wa mazingira pamoja na vita-yote yanayosababishwa na utawala wa uroho wa pesa na soko. Serikali pamoja na wapenzi wao wadhamini wa Kimataifa wanazungumzia bila kutimiza jinsi ya kukomesha umasikini lakini hawajawahi kutaja uwezekano wa kutukabidhi fedha tunazohitaji. Ni sisi wenyewe, tukianza na wanawake walezi wanaohangaika kila kukicha kuhifadhi maisha, juhudi zisizo lipiwa, ndiyo tutaweza kutekeleza mabadiliko haya. Mgomo ndiyo mfumo wetu wa kujiandalia lengo hili.
Madai ya Mgomo
· Malipo kwa kazi zote za huduma –katika mishahara,pensheni ya uzeeni,ardhi na njia nyingine za mapato.Nini la thamani kuliko malezi ya watoto na kuwatunza wengine? Wekeza katika uhai na mahitaji ya kimaisha,siyo bajeti ya majeshi au magereza.
· Usawa wa malipo kwa wote,wanawake kwa waume katika soko la Kimataifa.
· Upatikanaji wa chakula kwa mama anayenyonyesha, malipo ya likizo ya uzazi na likizo ya kujifungua. Komesheni kutuadhibu kwa sababu ya kuwa wanawake.
· Msilipe madeni ya Dunia ya Tatu’ Hatudaiwi ila tunawadai wao.
· Upatikanaji wa maji safi,huduma za afya,malazi, usafiri na elimu.
· Nguvu na Teknolojia zisizo haribu mazingira ambazo hufupisha saa za kazi.Wote tunahitaji majiko ya kisasa,majokofu, mashine za kufulia,kompyuta na mda wa kupumzika!
· Ulinzi a hifadhi dhidi ya fujo na unyanyasaji, pamoja na unaofanywa na watu katika familia na viongozi walio madarakani.
· Uhuru wa kusafiri. Hela inaruhusiwa kusafirishwa bila pingamizi,kwanini watu wasiwe na uhuru kama huo?

MAONI YA WANAHARAKATI KUHUSU RIPOTI YA RICHMOND ILIYOWASILISHWA BUNGENI DODOMA 06/02/08

MAONI YA WANAHARAKATI KUHUSU RIPOTI YA RICHMOND ILIYOWASILISHWA BUNGENI DODOMA 06/02/08

Wanaharakati wa masuala ya Jinsia, Haki za Binadamu na ukombozi wa wanawake kwa pamoja tunawapongeza wabunge wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania hususan walioanzisha hii hoja nzito na kuibua mjadala mzito wa Kitaifa, Kamati Teule, Vyama vya siasa, vyombo vya habari na wanaharakati wote kwa kuonyesha uzalendo juu ya mali za Taifa la Tanzania kwa kuweza kufichua na kuweka wazi mkataba wenye utata wa Richmond.

Pia tunawapongeza kwa kuona dalili kuwa Bunge limeanza kurudisha hadhi yake na tunatambua kuomba radhikulikofanywa na Spika wa Bunge kutokana na kauli yake kutumia neno ‘kukurupuka’ dhidi ya Naibu Spika wa Bunge
Tunalitaka Bunge lisirudi nyuma bali liendelee kusonga mbele kutetea na kusimamia maslahi ya wananchi

Sisi wanaharakati tunadai yafuatayo:
· Ripoti ya Kamati Teule ya Mkataba wa Richmond ichukuliwe kwa uzito wake kama ilivyo na iheshimiwe.
· Wahusika wote waliotajwa ( iwe Taasisi au mtu mmoja mmoja ) wawajibishwe kulingana na misingi ya Katiba na Sheria.
· Liundwe baraza jipya la mawaziri kufuata maadili ya uongozi
· Mikataba mipya inayotarajiwa kusainiwa iwe wazi na shirikishi
· Kamati ya Rais ya madini na ya BoT zibadilishwe na kuundwa kwa Kamati za Bunge za kuchunguza masuala ya madini, BoT pamoja na masuala yote ya raslimali za Taifa hili hususan katika vipindi vya urekebishaji wa uchumi.
· Mikataba yote yenye utata ifuatiliwe upya na iwe wazi
· Taasisi ya kudhibiti na kuzuia rushwa (TAKUKURU) iwe chini ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania
· Mali yote ya Taifa iliyopotea irejeshwe
· Turejee ripoti ya Warioba ya mwaka 1996 kama kweli tunahitaji kupingana na ufisadi wowote ule
· Tunatoa angalizo kwa Spika wa Bunge kwamba masuala yote nyeti yalenge maslahi ya wananchi na sio maslahi ya mtu mmoja mmoja au kikundi fulani

Mwisho, Suala hili linatoa changamoto kwa mfumo mzima wa demokrasia nchini. Mfumo tulionao wa demokrasia wakilishi haufai tunadai demokrasia shirikishi.

07/02/08

Tenda wema wende zako

Wakati ule kikwete amefanikiwa kuchaguliwa na watanzania kwa zaidi ya asilimia 80 ya kura zote kila mtu alikuwa anajiuliza baraza la mawaziri litakuwaje lakini hakuna aliyekuwa anajiuliza waziri mkuu atakuwa nani .

Kwa hakika waziri mkuu alikuwa ameshajulikana kutokana na historia yenyewe ya raisi na jamaa zake wa karibu , kila mtu alijua ni lowasa bila kubisha .

Lowasa na kikwete wametoka mbali kuanzia chuoni pale UDSM , jeshini , kushika nyadhifa zingine serikalini na katika chama na mambo mengine mengi ya ushirikiano wao ukijumuisha wakina makamba .

Urafiki wao uliendelea kwa muda mrefu mpaka ilipofikia siku ambapo wote kwa pamoja lowasa na kikwete walipoamua kufanya biashara ya kusafirisha ngombe kwenda katika nchi za komoro .

Inasemekana walikuwa na ngombe zaidi ya 7000 hawa ngombe walitakiwa kusafirishwa kwa njia ya maji mpaka visiwa vya komoro , wakafikia makubaliano jinsi ya kusafirisha na mambo mengine .

Kwa kuwa lowasa ndio mtendaji mkuu akaamua kutafuta meli ya bei rahisi kupeleka hawa ngombe , meli yenyewe ilikuwa mbovu baada ya kufanyiwa maangalizi katika bandari ya dare s salaam .

Waziri mkuu pamoja na kujua ile meli ni mbovu akalazimisha ngombe wapakiwe kupelekwa komoro , meli ikaenda komoro kufika njiani meli ikapata matatizo , sehemu yenye ilikuwa ni ngumu kufikiwa kwa njia za karibu za maji .

Wale ngombe wakaanza kufa mmoja mmoja mpaka walipobakia ngombe 1400 , wakati huo lowasa ndio akaanza kutafuta njia za kupeleka chakula katika meli hiyo kwa njia ya ndege lakini alikuwa ameshachelewa sana .

Na hapo ndipo kisa cha kikwete na lowasa kilipoanza , kama unafuatilia vizuri utakumbuka kikwete alikataza wanasiasa kujihusisha katika siasa na biashara au sio ?

Wakati anasema vile alijua fika aliyekuwa anamwambia nae ni waziri mkuu wa wakati huo mh lowassa , lakini alisahau kitu kimoja kwamba na yeye pia ni mfanya biashara tena biashara yake ya mwisho ni hii ya ngombe kusafirishwa kupelekwa komoro hapa napo sijui raisi atueleze nini tumwelewe .

Pamoja na yote haya lowasa anaendesha biashara kadhaa kwa kutumia majina ya watoto wake akina fredy ambaye yuko jijini kwa sasa na richi ambaye yuko nchini afrika kusini kwa sasa .

Sasa basi;-

Kila unapoenda vijana kwa wazee mazungumzo ni Richmond tu , kila sehemu lowasa tu , wengi wanampongeza sana kikwete kwa kazi aliyoifanya ya kumwajibisa lowasa , hawajui kwamba lowassa aliamua kujiuzuru mwenyewe kutokana na hiyo kashfa ya Richmond .

Watanzania bwana na sasa wameshasahau kuhusu EPA , BOT , IPTL , BUZWAGI na kashfa zingine kubwa ambazo ni zaidi ya hii ya Richmond na kwa hakika tume zikiundwa hapa wataondoka wengi .

Jana nilipokuwa natazama TV naona viongozi wa dini nao wanaongelea masuala ya ufisadi bila woga na kujiamini lakini tukumbuke wachungaji hawa hawa ndio wanaomwita lowasa katika matamasha yao ya kuchangia shule na miradi mengine na anachangia pesa nyingi .

Kama lowasa akiwajibishwa na kusema zile hela amepeleka wapi naamini nyingi zitakuwa zimeenda katika kuchangia haya makanisa , hizi shule za makanisa , na taasisi zingine za kikanisa je kanisa liko tayari kurudisha pesa husika ?

Wakati tunataka lowasa arudishe pesa za watanzania , tuwanyooshee vidole kuwaonya viongozi wa dini kwamba nao wanaohusika katika kupokea haya mapesa ya lowasa katika michango yake ya kanisa tunawaomba waelezee hiii michango ya lowasa wameitumia vipi au nao wajiuzuru.

Leo jioni wakati naelekea nyumbani nilipita katika kizuizi Fulani cha gari , wale jamaa wakawa wanataka mchango kwa sababu wametengeneza hiyo bara bara mara dala dala likapita yule konda akawaambia abiria zake
Eehh angalia ile ndio Richmond yao nao wanakula kiulaini .

Na usiku huu hapa nilipo nimeshituka toka usingizini , najiuliza kikwete atatushawishi vipi ili tuweze kuamini baraza lake la mawaziri litakalo tangazwa kesho , kutakuwa hakuna wafanyabiashara wanaokodisha meli mbovu na iharibikie baharini ?

Au atatuletea mawaziri ambao nao wana virichmond vyao huko pembeni ? wanakuja kuendelea na tabia zile zile za kuchota kufukuzwa , kujiuzuru au kuamua kuchoka tu ?

Ngoja tuone kila mtu na kirichmond chake

AJARI MBAYA YAUA SINGIDA


Naaungana na watanzania wenzangu kuwapa pole ndugu zetu walopata ajali iliyotokea Singida, Pia nawaomea wale wote walifaliki dunia.

Mungu azilaze roho za marehemu "Pema Peponi".Ameni

Watu saba wamefariki dunia na wengine 64 wajeruhiwa vibaya na baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo.

Ajali hiyo iliyotokea jana kati ya saa 4.30 na saa tano usiku katika Kijiji cha Utaho,tarafa ya Ihanja,wilaya ya Singida vijijini ililihusisha basi la Adventure lenye namba za usajili T.576 ABL aina ya Scania lililokuwa likisafiri kutoka Dar-es-Salaam kwenda Mwanza kugongana uso na lori la mafuta.

Marehemu wawili tu ndiyo mpaka sasa waliokuwa wametambuliwa kwa majina ambao ni Edita Elisha na mwingine ametambulika kwa jina moja tu la mzee Kipara. Hata hivyo habari zaidi zimesema kati ya majeruhi hao waliolazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu, na 31wapo kwenye Hospitali ya Mkoa wa Singida wakati kwenye hospitali ya misheni ya Mtakatifu Maria kuna majeruhi 33. Majeruhi ni pamoja na:-



  1. Amina Twalibu(41) mkazi wa Kigoma,

  2. Robert Wilsoni (37)mkazi wa Kigoma,

  3. Lameck Habibu (48) mkazi wa Kigoma,

  4. Samsoni Shadrack(40) ,mkazi wa Kigoma,

  5. Huseni Simoni (38)mkazi wa kigoma,

  6. Toda Jumanne(26) mkazi wa Kigoma,

  7. Mary Lotenga(18) mkazi wa Kigoma,

  8. Olbert Ernesti(15) mkazi wa Kigoma,

  9. Mwanahawa Twalibu (18)mkazi wa Kigoma

  10. Ramadhani Hassani(41) mkazi wa kigoma.

  11. Bakari (28) mkazi wa Kigoma,

  12. Haruna Juma(54) mkazi wa Kigoma,

  13. Michaeli Julius(23) mkazi wa Kigoma,

  14. Phenusi Jonathani(32) mkazi wa Kigoma,

  15. Hamadi Milongo(43) Kigoma,

  16. Roxima Protasi (26) mkazi wa Ujiji,

  17. Benard Francis (32) mkazi wa Kigoma,

  18. Muhile Emanueli(32) mkazi wa Kigoma,

  19. Nestory Salumu (48) mkazi wa Kigoma

  20. Jeraldi Marcel (34) mkazi wa Kigoma.

Kwa mujibu wa Bi Kaluba wengine ni



  1. Revocatus Philibert (20) mkazi wa Kigoma,

  2. Elia Ntinyaku (31) mkazi wa Kigoma,

  3. Eliasi Eliudi (20) mkazi wa Kasulu,

  4. Renatus Mkarunga (44) mkazi wa Kigoma,

  5. Mikidadi Kongwe(23) mkazi wa Kigoma,

  6. Jumanne Mtaba (30) mkazi wa Kigoma,

  7. Husseni Yasini (34) mkazi wa Kigoma,

  8. Musa Danieli (34) mkazi wa Kasulu,

  9. Mwimbwa Ladiscaus (53) mkazi wa Kigoma,

  10. Bestina Methew (16) mkazi wa Kigoma

  11. Walivyo Athumani (17) mkazi wa Kigoma.