Monday, May 26, 2008

Maswali Bungeni 26/5/2008

1. Kwa kuwa ni muda mrefu sasa ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi Kambi ya Finya, umesimama na kwa kuwa nyumba za makazi ya polisi zilizopo police line Wete ni mbovu sana, zimechakaa na zinavuja mno wakati wa mvua hali ambayo inasababisha usumbufu mkubwa na kuhatarisha usalama kwa familia zinazoishi humo na kwa kuwa polisi wengi na hasa wa vyeo vya chini wana ari ya kujenga nyumba binafsi za kuishi lakini kipato chao ni kidogo:-

(a) Je, Serikali itamalizia lini ujenzi wa nyumba za polisi Kambi ya Finya?

(b) Je, ni lini Serikali itazifanyia matengenezo nyumba za Police Line ili ziwe na hali nzuri?

(c) Je, Serikali haiwezi kuwasiliana na taasisi za fedha nchini ili polisi wapatiwe mikopo ya kujenga nyumba zao za binafsi?

bonyeza hapa kwa- majibu

2. Kwa kuwa, Wananchi wa Mji wa Mererani wanajishughulisha na biashara na uchimbaji wa madini ya Tanzanite, lakini wamekuwa wakipata taabu ya barabara kati ya Mererani na KIA; na kwa kuwa Rais wa Awamu ya Tatu na Awamu ya Nne walipoiona hali hiyo ngumu waliahidi kujenga barabara hiyo isiyozidi kilomita 20 kwa kiwango cha lami:- Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kujenga barabara hiyo muhimu sana kiuchumi, kutimzia ahadi zilizotolewa na Ma-Rais hao.

Jibu kutoka kwa Mh. Celina Ompeshi Kombani REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT

NAIBU WAZIRI alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, napenda kujibu Swali la Mheshimiwa Chrisopher Ole-Sendeka Mbunge wa Simanjiro kama ifuatavyo. Majibu


3. Kwa kuwa Serikali ina mikakati mizuri ya kuwawezesha wananchi hususan wanawake kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwapatia mikopo ya kufanyia biashara ndogo ndogo; na kwa kuwa Mkoa mpya wa Manyara una matatizo mengi makubwa ya mazingira ya kufanyia biashara hizo ikiwa ni pamoja na elimu ya ufahamu, kero za maji, uhaba wa Zahanati kwa baadhi ya vijiji na kutokuwepo na hospitali ya Mkoa.

(a) Je, Serikali ina mipango gani ya upendeleo kwa Mkoa wa Manyara ya kuboresha Mazingira chini ya Mpango wa MKUMBITA?

(b) Je, Serikali itafikisha lini mradi wa SELF Mkoani Manyara ikizingatiwa kuwa hakuna taasisi za fedha zinazofikisha huduma huko zaidi ya SACCOS zilizoanza hivi karibuni?

Jibu kutoka kwa Mh. Dr. Batilda Salha Burian PLANNING, ECONOMY AND EMPOWERMENT

NAIBU WAZIRI alijibu: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Martha Umbulla, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- Majibu

Maswali na Majibu Bungeni 26/5/2008

Swali

Kwa kuwa muda mrefu sasa, wananchi waishio Londrosi West Kilimanjaro katika Wilaya ya Siha, wamekuwa wakitaabika kutokana na ubovu wa barabara itokayo Ngare Nairobi Londrosi Gate; na kwa kuwa ubovu huo unakwamisha shughuli za kiuchumi hasa kwa upande wa watalii wanaotaka kupanda Mlima Kilimanjaro:-



(a) Je, ni Mamlaka gani inayotakiwa kushughulikia barabara hiyo?



(b) Je, ni hatua gani zinachukuliwa na Serikali kurekebisha hali hiyo?


ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION
Answer From Hon. Dr. Milton Makongoro Mahanga INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Aggrey D. J. Mwanri, Mbunge wa Siha, lenye sehemu (a) na (b), kwa pamoja kama ifuatavyo:-


Mheshimiwa Spika, barabara ya Ngare Nairobi - Londrosi Gate inashughulikiwa na Mamlaka mbili tofauti; sehemu ya Ngare Nairobi hadi Simba Farm yenye urefu wa kilomita 1.5 kwa upande moja ambayo ni barabara ya Mkoa (Sanyajuu – Kimwanga) iko chini ya uangalizi wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Kilimanjaro na kwa upande mwingine, barabara itokayo Simba Farm – Londrosi Gate yenye urefu wa kilomita 10, iko chini ya uangalizi wa KINAPA na kampuni ya West Kilimanjaro.


Bonyeza hapa - Muendelezo wa majibu

JK aenda japani leo:

Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka nchini leo jioni (25 Mei, 0 kuelekea Japan kuhudhuria mkutano wa nne unaohusu maendeleo ya Afrika, ujulikanao kama Tokyo International Conference on African Development (TICAD) utakaofanyika katika jiji la Yokohama.

Kabla ya kuhudhuria mkutano huo, Rais Kikwete atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Yasuo Fukuda, tarehe 27 Mei, 08 kuzungumzia mahusiano na ushirikiano wa nchi mbili hizi katika maswala ya kiuchumi na kidiplomasia na pia kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Kikwete anatarajiwa kumweleza mwenyeji wake juu ya maendeleo na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika na kujadili utatuzi wake.

Japan ni mshirika mkubwa wa maendeleo ya Tanzania ambapo Japan ni moja ya nchi zinazoisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuchangia katika bajeti na pia imechangia katika misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula, barabara na maji.

Mkutano wa nne wa TICAD utaanza tarehe 28-30 Mei, ambapo viongozi wote wa bara la Afrika wamealikwa kuhudhuria pamoja na viongozi wa Japan, wakuu wa mashirika mbalimbali ya kimataifa duniani kama vile Umoja wa Mataifa, mashirika ya fedha duniani, taasisi sizizo za kiserikali kutoka bara la Asia na Afrika, nchi rafiki na wenza katika maendeleo duniani.

Mbali na mkutano wa TICAD Rais pia atashiriki mikutano na makongamano mbalimbali yanayohusu uchumi, miundo mbinu, maendeleo na maswala mbalimbali yanayohusu utunzaji wa mazingira barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Aidha Rais Kikwete ataongoza mkutano utakaojadili tatizo la chakula duniani ambapo atazungumzia swala hili kwa kina hususan katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo barani Afrika na hatimaye atashiriki katika kupitisha azimio la Yokohama.

Rais pia anatarajia kutumia nafasi hiyo kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Afrika watakaohudhuria mkutano huo.

Rais atafuatana na

  1. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Benard Membe,
  2. Waziri wa Fedha - Mhe. Mustapha Mkulo,
  3. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Zanzibar - Mhe. Haroun Suleiman,
  4. Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko - Mhe. Cyril Chami
  5. na Mbunge wa Muleba Kusini
  6. na Mwenyekiti wa Kamati Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama - Mhe. Wilson Masilingi.

Rais anatarajiwa kurejea Dar-es-Salaam tarehe 31 Mei, 2008.

Imetolewa na Ikulu-Dar-es-salaam25.05.08