Saturday, March 1, 2008

Wakimbizi wa Katumba kuanza kurejeshwa makwao Machi 9

Zoezi la kuwarejesha wakimbizi wa makambi ya Katumba na Mishamo wilayani Mpanda, mkoani Rukwa nchini mwao litaanza rasmi Machi 9, hadi Novemba, Mwaka huu.

Mgeni rasmi katika zoezi hilo anatarajiwa kuwa Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

Hayo yamo katika taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Bw. Thobias Mazanzala, kwa Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda, katika ziara yake ya siku tatu wilayani Mpanda.

Aidha zoezi la kutoa uraia litaanza mara moja baada ya uzinduzi wa urejeshaji kuanza ambapo muda ulipangwa kwa wakimbizi wa makazi ya Katumba kurejea nchini Burundi ni Machi hadi Novemba mwaka huu ambapo kwa wakimbizi wa makazi ya Katumba ni Machi hadi Julai.

Bw. Mazanzala alifafanua kuwa kwa wakimbizi waishio katika makambi ya Katumba wamepewa muda mrefu wa kuondoka kutokana na uwingi wa waliojiandikisha.

Alisema kuwa makazi ya wakimbizi ya Katumba yana watu 109,243 ambapo makazi ya Mishamo yana wakimbizi 56,251 na zoezi la maandalizi la kuwasajili wakimbizi wote wanaotaka kurejea burundi na wanaotaka kubaki Tanzania na kuomba uraia lilifanywa kwa ushirikiano wa UNHCR na serikali ya Tanzania na ya Burundi.

Alifafanua kuwa jumla ya familia 23,527 za makazi ya katumba yenye wakimbizi 108,925 waliosajiriwa ambapo wakimbizi 35,000 sawa na asilimia 35 ndio waliokubali kurejea nchini kwao kwa hiari na asilima 3 kutochagua chochote.

Alisema kuwa katika makazi ya Mishamo jumla ya wakimbizi 1500 kati ya 56,251 ndio waliokubali kurejea nchini kwao kwa hiari.

SOURCE: Nipashe

Nidhamu ndio silaha yetu

Nidhamu ndio silaha yetu


kiongozi wa kundi la Ze Comedy Isaya Mwakilasa almaarufu kama Wakuvwanga amedai kua nidhamu ndio silaha yao kubwa inayowafanya wadumu hadi leoAkiongea na darhotwire Wakuvwanga ambaye anafahamika kama waziri mkuu aliyejiuzuru au Mama beleee alisema nidhamu ndo silaha ya kundi lao kuwepo hadi leoKumekuwa na udaku wa mara kwa mara unavumishwa kama sie tumesambaratika kutokana na didhamu yetu hilo itakuwa ngumu..


Tofauti yetu na wachekeshaji wengine ni hiyo tu nidhamu na wote kujiona level moja hakuna super star wote ni wamoja na ndio maana kiapokuwepo mwnzetu mmoja nasisi wote tu...alisema WakuvwangaNa walidokeza kinachowapa kiburi cha kuwaigiza watu ni kutokana na kuwa na uhakika na wanachoigiza na ushahidi wa vithibitisho na kuzingatia kuelimisha na kukosoa pamoja na kuburudisha kwa watati mmojaMsomaji wa safu hii endelea kuzuru ukurasa huu ili upate makala za viumbe hawa hivi karibuni.


safari hii ni mavazi ya ngozi


safari hii ni mavazi ya ngozi
Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, mwaka huu inatarajiwa kupambwa na mavazi ya ngozi za mbuzi, magome ya miti na magunia kutoka kwa mwanamitindo Fatuma Amour. Akiongea na Darhotwire , mbunifu huyo alisema sherehe hizo zitafanyika katika ukumbi wa Movenpick jijini na kaulimbiu yake ni ‘heshima kwa akina mama’.


Aidha, alisema hafla hiyo pia itatumika kuwaburudisha watu watakaofika kwa lengo la kutuliza nyoyo zao, huku wakibadilishana mawazo na kufahamishana mambo mbalimbali. Alisema, ili kutoa burudani ya heshima na kuhakikisha siku hiyo inakuwa ya kupendeza, kutakuwapo na bidhaa kama mikoba na malapa vilivyobuniwa katika mtindo wa kiutamaduni. Alisema, vikundi vya burudani vitakavyotumbuiza siku hiyo ni Unique Sisters na kikundi cha sanaa cha Saidi Comorien. Mwaka jana tulisherehekea siku hii kuambiwa tubebe vikapu na tuachane na mifuko ya karatasi ili tuweze tunza mazingira...mwaka huu ni mwenzo wa ngozi Hallow!!


Kasi ya maambukizi ya ukimwi katika maeneo ya Feri jijini inazidi kuongezeka

Kasi ya maambukizi ya ukimwi katika maeneo ya Feri jijini Dar es Salaam inazidi kuongezeka kutokana na kushamiri kwa vitendo vya ukahaba na matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana.

Hayo yamebanishwa na mratibu wa mafunzo kuhusu udhibiti wa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi Bibi Elina Nachibona. Awali akifungua mafunzo hayo, naibu Meya wa manispaa ya Ilala Mohamed Yakoub amesema kampeni ya elimu ya ukimwi itaendeshwa katika kata zote za manispaa ya Iala na kuwapatia waathirika dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.

SOURCE: ITV

Bilioni 50/- zarejeshwa 2008-03-01 09:01:31 Na Mwandishi Wetu

Zaidi ya Sh. bilioni 50 kati ya bilioni 133 zilizochotwa na mafisadi kupitia akaunti ya madeni ya nje ya Benki Kuu (BoT) zimerudishwa serikalini.

Pamoja na fedha hizo, mali nyingine za watuhumiwa hao zilizoko nje na ndani ya nchi zikiwemo nyumba zimegundulika kwa mujibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Bw. Mustapha Mkulo.

Bw. Mkulo alitaja kiwango hicho kwenye mkutano wa waandishi wa habari, uliofanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Timu ya Maofisa wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) na kushirikisha maofisa kadhaa wa wizara hiyo na BoT.

Waziri aliyekuwa anajibu maswali ya waandishi wa habari alisema mali hizo zimenaswa katika kipindi cha mwezi mmoja na lengo ni kurudisha fedha zote, kukamata mali za watuhumiwa na kuwachukulia hatua za kisheria.

Alipoombwa kutaja majina ya wahusika na kampuni zao Bw. Mkulo alisema kwa sasa si wakati muafaka kwani kutavuruga upelelezi na jitihada za kurudisha fedha hizo na kuwafikisha mbele ya sheria watuhumiwa.

Tume iliyogundua mali hizo ni ile iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete , mwezi uliopita inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika na wajumbe wengine kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kwa kushirikiana na Bodi ya Wakurugenzi wa BoT.

Tume hiyo imepewa kazi ya kurudisha mali na fedha za watuhumiwa na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.

Makampuni 22 yaliyotuhumiwa kulipwa Sh. bilioni 133 na BoT kinyume cha sheria katika kipindi cha 2005/06 kupitia akaunti ya EPA ni pamoja na Bencon, VB & Associates, Bina Resorts, Venus Hotel, Njake Hotels and Tours, Maltan Mining Companies, Money Planners &Consultants.

Mengine ni Bora Hotels and Apartments, BV Holdings , Ndovu Soap, Navy Cuts Tobacco, Changanyikeni Residential Complex, Kagoda Agricultre, G&T International, Excellent Services, Mibale Farm, Liquidity Service, Clayton Marketing, M/S Rastash, Maregesi Law Chamber (Advocates), Kiloloma & Brothers, Karnel Ltd.

Makampuni hayo yalilipwa baada ya kuwasilisha vielelezo vya kughushi, hati batili na baadhi hayakuwa na nyaraka zozote na kwa ujumla hayakustahili kulipwa chochote.

Makampuni hayo yaliibuliwa na kampuni ya Ernst & Young ya Uingereza iliyopewa zabuni na serikali kuchunguza madai ya upotevu wa mabilioni ndani ya BoT kupitia akaunti ya madeni ya nje (EPA).

Katika mkutano huo, Waziri Mkulo, alisema majadiliano kati ya serikali na maofisa wa IMF yalilenga kwenye usimamizi na utunzaji wa fedha. `

`Tumezungumzia hali ya uchumi na kuazimia kuweka mkazo katika kukuza uchumi katika kiwango cha juu na cha chini.`` ``

Kadhalika tumeazimia kuboresha na kusimamia ipasavyo ukusanyaji mapato ili kuliondosha taifa na utegemezi na umaskini,`` alisema.

Alisema pamoja na hayo serikali imeazimia kuimarisha sekta ya nishati mijini na vijijini ili kuondoa matatizo yasiyokwisha ya nishati.

Waziri alisema mazungumzo hayo yaliazimia pia kuwa lazima Tanzania izingatie utawala bora unaofuata sheria.


SOURCE: Nipashe