Kijana Ramadhani Mussa (18) ambaye amekamatwa na kichwa cha mtoto mwenzie na kuanza kukinyoya damu hadharani pale kwenye lango la Hosptali ya Taifa Muhimbili, alishawahi kukutwa kwenye makanisa kadhaa ya jijini Dar es salaam akidai kudondoka na ungo na kisha kuombewa na wachungaji wa makanisa hayo, lakini mara ya mwisho alionekana ni kijana tapeli tu au wachungaji waliokuwa wakimuombea walikuwa wanafanya usanii kuvutia 'wauimini'!
Awali mtoto huyu inadaiwa alikutwa usiku wa manane kwenye Kanisa la Kilutheran pale Manzese na kuombewa na Mchungaji Jonathan wa Kanisa hilo baada ya kudai kuwa amedondoshwa na wachawi wakiwa kwenye ungo, ingawa waumini wengine walimuona kijana huyo kama mchawi na kutaka kumpiga.
Baadae inadaiwa alipelekwa Hospitali ya Mwananyamala ambako nako alitoweka kimiujiza, kabla ya kukutwa kwenye kanisa lingine Tabata na hatimaye Mikocheni kwa Mchungaji Rwakatare ambako ndiko alipoombewa akiwa na mwenzake kwa muda kabla ya kuambiwa kuwa ni 'matapeli' kwani hizo ndizo zao kujifanya wamedondoka kwenye ungo na kuibukia Makanisani ili kujipatia pesa!
Akiongea na kituo cha ITV jana, Mchungaji Rwakatare, ambaye pia ni Mbunge wa CCM wa kuteuliwa, alisema "Mungu amejitetea mwenyewe" kwa kuonesha kuwa walichokuwa wanakisema kuwa watoto hao walikuwa na mapepo hawakuwa wanaongopa.
"Laiti kama wangewaachia wawaombee, yule mtoto asingekufa wala yasingetokea yaliyotokea, lakini kwa sababu kuna watu wanajaribu kuwa kama Mungu, ndiyo maana haya yote yanatokea!
"Wamuache Mungu awe Mungu", alisema Mchungaji Rwakatare na katika hili inaoenekana mtumishi huyu wa Bwana amejipatia 'tano' zingine!




Binafsi anadhani hili suala linapaswa kutazamwa katika mapana na mazingira yake,kwa ufupi tumezoea kusikia wachawi wa aina ya huyo mtoto wakila nyama za maiti makaburini ingawa haijawahi kudhibitishwa, wakichukua watu kichawi na kuwapoteza lakini si kwa staili aliyochukuliwa huyu mtoto,huyu alitekwa akajichwa kiwiliwili kikatupwa chooni na kichwa akaondoka nacho huyo mtoto na huko anadai kwamba nyama nyingine wenzake wanaendelea kula!!iweje kikutwe kiwiliwili kama wenzie wapo kweli?na walikuwa wanakula? Hapa jeshi la polisi ikiwezekana kutumia staili ya Abu Ghraib ama hata Guantanamo bay kumhoji huyu mtuhumiwa namba moja nadhani hiyo ifanyike!mara nyingine inabidi tusahau kidogo kuhusu human right ya baadhi ya binadamu! yes apate kibano cha nguvu kama ni kichaa kimtoke na kama ni mashetani yapate adabu yake then atueleze kisa cha kuondoa uhai wa mtoto mzuri kama yule asiyejua hili wala lile!na hao akina Lwakatare na walokole wenzie waendeshe hizo sara basi tuondokane na aina hiyo ya watu!hasa mzizi akina Elizabeth na Kichaka kama anavyodai Sheikh Yahya.Ama hii ni mbinu ya mafisadi kutusahaulisha kwamba kuna EPA, RICHMOND<>
No comments:
Post a Comment