Monday, March 31, 2008

SERIKALI YA MSETO ISIISHIE TANZANIA VISIWANI JAMANI

Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu yenu Wanazuoni.



Nikiwa natafakari juu ya vikao vya chama twawala, CCM, limenijia wazo kwamba, kwa madokezo tuliyopata, vikao hivyo muhimu vitajadili mambo muhimu likiwamo la muafaka wenye lengo la kumaliza mpasuko wa kisiasa (kijamii, kiuchumi nk) huko Tanzania Visiwani. Jambo kubwa linaloonekana kuwa mwarobaini wa mpasuko huo ni kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, kama ambavyo tulishadokezwa.


Hizo kwangu, ni habari njema sana. Ninaamini kwamba katika ulimwengu wa kisasa, siasa haina budi kuwa ya 'kisasa'. kwa hiyo ni vema basi tuache kubaguana, bali tukae pamoja tuijenge nchi yetu. Kenya mseto umeonekana na unaelekea kumaliza tafrani ya hivi karibuni, vivyo hivyo Afrika kusini, amani iliyofuatia Uhuru wa nchi hiyo imetokana na kukubali kuishi na kutawala pamoja.

hoja yangu ya msingi basi ni kwamba, kwa vile vikao vitakavyofanyika buti ama vya ccm ndivyo vikao muhimu zaidi vya chama kinachotawala, visiishie katika kujadili uwezekano wa kuundwa kwa serikali ya mseto huko visiwani. bali vikao hivyo viende hatua moja mbele ya kujadili uwezekano wa kuwa na serikali ya mseto kwa tanzania nzima. mseto ukiwa halali upande mmoja wa taifa hili, kwanini uwe haramu katika ngazi nyingine? ikiwa mseto umeoneka mwarobaini wa matatizo ya kisiasa mahali pengine, kwani 'kisiwa cha amani kisitazame mbele na kuufanya kuwa kinga ya matatizo yanayoweza kutokea na kukifanya kisiwa cha machafuko? isitoshe hili, litawatoa hofu baadhi wahafidhina wa visiwani wanaodhani wao tu ndiyo waliyozaliwa kwa ajili ya kutawala. wakati umefika vikao hivyo viwe pro active. tusingoje yatokee yaliyotokea zanzibar, ama kenya, ndiyo tufikiri mseto. umamkini wa ccm utajidhihirisha siyo kwa hotuba, porojo, propaganda, uzandiki n.k, bali kwa kutazama mbele.

TUFANYEJE SASA?
mimi nimeandika ujumbe mfupi wa simu ufuatao kwa mjumbe wa nec wa mkoa wangu, "mhenshimiwa mnec wa mkoa wangu mshikamoo. nadhani ni wakati sasa mtakapojadili suala la serikali ya mseto zanzibar, msiishie hapo, mwende hatua zaidi, muibue mjadala wa kitaifa, jamhuri ya muungano ya tanzania iwe na serikali ya umoja wa kitaifa/mseto kuanzia uchaguzi ujao. kikao chema."

WITO:
Mwanazuoni mwenzangu, mtumie mjumbe wa NEC yeyote unayemfahamu SMS yenye ujumbe kama huo, ikiwa unaamini katika serikali ya pamoja, ambayo uwezekano wake KUWEKA MASLAHI YA TAIFA MBELE NI MKUBWA ZAIDI. Kwa kutuma SMS hiyo tunaweza kuwa tumeanzisha mchakato muhimu sana kwa mustakabali mwema wa taifa letu

NAWASILISHA.


Kwa niaba ya
ADAM, L

Wizara ya MiundoMbinu inafanya nini?

Hii ni Mvua ya siku moja Dar Je! ingeendelea kunyesha kwa muda wa wiki moja sii ni kiama tena? Sababu kama mifereji ya kupelekea maji imeziba na wizara zinakodolea macho nini kinafuata mvua kama hii ikiendelea kwa wiki nzima.




Wednesday, March 26, 2008

Raisi Mstaafu Mkapa hamuelewi Raisi Kikwete!

Mkapa hamuelewi Kikwete, unaweza ukaona ni kama mchezo flani wa kuigiza lakini ukweli ni kwamba yanaendelea huko nyuma ya pazia ni mazito kuliko yale ambayo tunayaona na kuyasikia hata pale Habari maelezo na hali ni ya kutoaminiana hadi leo hii !

Wakati Rais Kikwete, Anaingia madarakani si kwamba alikuwa mgeni na serikali aliyokuwa anaifanyia kazi na ambayo angekuwa ndio kiongozi wake muda ule alipoingia rasmi kama Rais wa nchi, Hakuwa mgeni alikuwa anayaelewa mambo ya kifisadi yote yaliyokuwa yanaendelea hata kama naye atakuwa ni mmoja wa wahusika kama ambavyo mnyororo unavyoonyesha !

Ili kuendelea na Serikali yake safi na kutoa mambo yote ya kifisadi ambayo Watu wake wa karibu walikuwa wanamweleza kuhusu Mkapa na kama mlivyokuwa mnajua kuwa Kikwete hakua chaguo la Mkapa basi aliamua kuunda kikundi chake cha siri ambacho kilianika mambo yote ya Mkapa na kumletea kila Data za Mkapa na Kikwete akaa nazo !

Katika hali ambayo hata mwenyewe Mkapa alishangaa ni pale ,Alipomuita yule Mama Anna Mkapa siku moja pale Ikulu na kumuonyesha utitiri wa malimbikizo ya mali ambayo yule Mama pamoja ama kwa kutumia cheo cha Mumewe Mkapa aliamua kutumia kila njia na kuikamua nchi ,Ikiwa ni pamoja na sakata zima la makabidhiano la TASAF !

Baada ya Mama Anna Mkapa kukataa kuiacha pale Ikulu ,Kikwete alituma Jamaa wake waifuatilie na kuifumua kwa kuifanyia "ODITING" ya nguvu hadi walipogundua kuwa yule Mama alikwisha kuumaliza ule Mfuko na masurufu yake !

Alipomuita alimuonyesha kila kitu kuhusu TASAF, na yule Mama wa watu akabaki hana la kusema ,kwani aliombwa tu aendelee na safari zake na kumuachia jamaa afikirie namna ya kufanya !

Aliyomuonyesha yalimtoa yule Mama jasho Achilia yale Magorofa ya Kariakoo aliyonayo, wala ile hotel ya Lamada aliyojinyakulia pale Ilala karibu na Msimbazi center, Alionyeshwa ubadhirifu wote alioufanya kwa kutumia cheo cha Mumewe kama Rais.Mkapa hamuelewi Kikwete, unaweza ukaona ni kama mchezo flani wa kuigiza lakini ukweli ni kwamba yanaendelea huko nyuma ya pazia ni mazito kuliko yale ambayo tunayaona na kuyasikia hata pale Habari maelezo na hali ni ya kutoaminiana hadi leo hii !

Wakati Rais Kikwete, Anaingia madarakani si kwamba alikuwa mgeni na serikali aliyokuwa anaifanyia kazi na ambayo angekuwa ndio kiongozi wake muda ule alipoingia rasmi kama Rais wa nchi, Hakuwa mgeni alikuwa anayaelewa mambo ya kifisadi yote yaliyokuwa yanaendelea hata kama naye atakuwa ni mmoja wa wahusika kama ambavyo mnyororo unavyoonyesha !

Ili kuendelea na Serikali yake safi na kutoa mambo yote ya kifisadi ambayo Watu wake wa karibu walikuwa wanamweleza kuhusu Mkapa na kama mlivyokuwa mnajua kuwa Kikwete hakua chaguo la Mkapa basi aliamua kuunda kikundi chake cha siri ambacho kilianika mambo yote ya Mkapa na kumletea kila Data za Mkapa na Kikwete akaa nazo !

Katika hali ambayo hata mwenyewe Mkapa alishangaa ni pale ,Alipomuita yule Mama Anna Mkapa siku moja pale Ikulu na kumuonyesha utitiri wa malimbikizo ya mali ambayo yule Mama pamoja ama kwa kutumia cheo cha Mumewe Mkapa aliamua kutumia kila njia na kuikamua nchi ,Ikiwa ni pamoja na sakata zima la makabidhiano la TASAF !

Baada ya Mama Anna Mkapa kukataa kuiacha pale Ikulu ,Kikwete alituma Jamaa wake waifuatilie na kuifumua kwa kuifanyia "ODITING" ya nguvu hadi walipogundua kuwa yule Mama alikwisha kuumaliza ule Mfuko na masurufu yake !

Alipomuita alimuonyesha kila kitu kuhusu TASAF, na yule Mama wa watu akabaki hana la kusema ,kwani aliombwa tu aendelee na safari zake na kumuachia jamaa afikirie namna ya kufanya !

Aliyomuonyesha yalimtoa yule Mama jasho Achilia yale Magorofa ya Kariakoo aliyonayo, wala ile hotel ya Lamada aliyojinyakulia pale Ilala karibu na Msimbazi center, Alionyeshwa ubadhirifu wote alioufanya kwa kutumia cheo cha Mumewe kama Rais.

Bonyeza hapa

Vyama korija, demokrasia sufuri

RAI YA JENERALI


NIMEKWISHA kueleza huko nyuma jinsi Mwalimu Julius Nyerere alivyotaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kigawanyike ili viwepo vyama viwili vyenye nguvu karibu sawa ingawa vikitofautiana kuhusu masuala ya itikadi, sera na mbinu za utekelezaji.

Mantiki ya mtazamo wa Mwalimu ilijengeka juu ya uelewa aliokuwa nao kuhusu siasa za ushindani. Kwa mtazamo wake, hakuna maana ya kuwa na mfumo unaoitwa wa “vyama vingi” lakini wakati huo huo ukajenga utaratibu ambao hauruhusu upinzani wa maana.

Nyerere hakufanikiwa katika hilo, na chama chake kikaendelea kuwa kimoja na chenye nguvu kubwa miongoni mwa jamii. Umoja huu na nguvu hiyo havitokani na makubaliano ya kiitikadi wala maelewano au mwafaka kuhusu masuala makuu ya kitaifa.

Ukweli ni kwamba hakuna makubaliano ya kiitikadi kwa sababu katika chama kisichokuwa na itikadi kuu si rahisi kupata ukinzani kwani ukinzani huzuka kutokana na itikadi inayobishiwa na kundi fulani, na bila ukinzani haiwezekani yakawapo makubaliano.

Hali kadhalika, kwa mwafaka kuhusu masuala makuu ya kitaifa. Kiongozi mmoja wa chama hicho aliwahi kusema, mara tu baada ya uchaguzi kwisha, kwamba ilani ya chama chake, ambayo ndiyo ilipelekwa kwa wananchi wakamchagua, haitekelezeki. Maana halisi ya tamko lake hilo ni kwamba ilani ni ujanja unaobuniwa wa kuwazuga wapiga kura kwa kuwahadaa na ahadi nyingi ambazo hao wanaozitoa wanajua fika kwamba hawana nia ya kuzitimiza.

Kama hiyo ni kweli, basi hakuna njia ya kupata mwafaka kuhusu suala lo lote la kitaifa, kwa sababu hata hayo tuliyoyaorodhesha kwamba ni mambo yatakayopewa kipaumbele ni kiinimacho tu. Katika hali kama hiyo programu huzuka kutegemea na viongozi wakuu wanavyojihisi kwa wakati huo, na utekelezaji huwa daima ni wa zima-moto. Hapo haiwezekani kuwa na mwafaka wa kiutaratibu wala ukinzani ulioaratibiwa.

Kimsingi, Chama cha Mapinduzi kimeendelea kuwa kimoja kwa sababu bado kiko madarakani, na kimekuwa kikitumia madaraka ya dola kuendesha kazi zake za kichama. Mifano michache inaweza kusaidia kueleza ninachokisema hapa:

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri anapopanda ndege ya Serikali kwenda mikoani kukagua miradi ya maendeleo, na akiwa huko akaendesha mikutano ya chama chake, tunaweza kusema kwamba chama chake kinakuwa kimepokea ruzuku kutoka serikalini kwa maana ya usafiri, malazi, chakula, na vinywaji. Aidha, katika misafara hiyo anaambatana na maofisa kadhaa wa chama chake, ambao nao hudandia ‘takrima’ iliyoandaliwa kwa ajili ya Rais.

Hali ni hiyo hiyo inapoandaliwa ziara ya Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar, Waziri Kiongozi na mawaziri wa kila aina, pamoja na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Zaidi ya hayo tuongeze utaratibu unaotumika wa kuwateua maofisa waandamizi wa chama-tawala kuwa mawaziri wanaolipwa na Serikali, wanaosafiri kwa magari ya Serikali, n.k.

Tungeweza kupiga mahesabu yaliyotulia tungegundua kwamba Serikali ya Tanzania inatoa ruzuku kwa CCM bila kukiri hivyo. Na tukumbuke kwamba ruzuku hii ni mbali kabisa na ile inayotolewa kwa kila chama kulingana na wingi wa kura kilizopata katika uchaguzi wa Rais na wingi wa wabunge wa chama husika, huko nako chama-tawala kimetwaa mgao wa simba.

Hivi sasa iko minong’ono ambayo haikosi chembe ya ukweli kwamba hata baadhi ya masuala yanayoibuka kuhusu ‘ufisadi’ katika asasi nyeti za Taifa yametokana na chama-tawaka kuchotewa fedha kutoka asasi hizo kwa ajili ya kampeni za uchaguzi. Ni dhahiri kwamba chama hicho kimeegemea mno Serikali kiasi kwamba ni vigumu kukifikiria kikiendelea kuwapo iwapo, kwa sababu yo yote ile, kingepoteza madaraka.

Kikiwa kinaendelea kuwa madarakani kitaendelea kuvuta kila aina ya watu, wema na waovu, waongofu na mafisadi, wazalendo na wahaini, alimradi chama bado ni chimbuko la neema, ndicho kitovu cha mgawanyo wa madaraka ya dola katika ngazi zote, na kituo cha kushamirisha biashara za wanachama waaminifu.

Kuhusu suala la mlolongo wa viongozi na watawala waliopewa madaraka mbalimbali kutokana na kuwa waaminifu kwa chama-tawala, sehemu ya Zanzibar huwa naiona kama kichekesho.

Hivi kuna sababu gani hasa kwa kisiwa kisichokuwa na ukubwa wa mkoa mmoja wa Tanzania Bara (Tanganyika) kuwa na Rais, Waziri Kiongozi, Naibu Waziri Kiongozi, mawaziri dazeni na naibu mawaziri korija, makatibu wakuu wa wizara, naibu makatibu wakuu, wakurugenzi, naibu wakurugenzi, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, masheha, n.k. Inaelekea Visiwa hivyo vina viongozi wengi kuliko raia.

Lakini hata upande wa Tanzania Bara hali si tofauti sana kama tukiangalia mlololongo wa mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu na manaibu wao, wakurugenzi, wakuu wa mikoa, maofisa utawala wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa wilaya, watendaji wa tarafa na kata, hadi wenyeviti na makatibu wa vijiji.

Dhahiri, hii ni nchi inayotawaliwa kupindukia (over-governed) ingawaje maendeleo hayaonekani kwa uwiano unaofanana na ukubwa wa utawala. Dhahiri vile vile, watu wengi watakusanyika katika chombo kinachotoa fursa ya kushiriki katika hilo ‘Treni la Michuzi’ kwa sababu kuna ajira kwa ajili ya watu wengi. Hata wasiokuwa waumini wa jambo lo lote wataimba wimbo wo wote unaowahakikishia kipato kinono na maisha nafuu.

Sasa, kutokana na ukubwa wa chama, udhibiti kilichonao juu ya rasilimali za Taifa na mkusanyiko wa kimaslahi wa watu wa kila aina na tabia (silika ya kokolo), chama kimejiundia chenyewe matatizo ambayo hakikutaraji yangechukua sura iliyokuja kujitokeza. Hapa napo, kwa mara nyingine, tena, tunakutana na ile sheria ya matokeo yasiyotarajiwa (unintended consequences). Hebu tuangalie kilichotokea bila kutarajiwa.

Mwalimu Nyerere alisema kwamba hakuna mantiki ya kuwa na mfumo unaoitwa wa “vyama vingi” bila kuwa na vyama vya kweli. Wakuu wa CCM walikuwa na mawazo mengine. Walikwisha kuona jinsi walivyosumbuliwa na kile kilichoitwa G-55 wakati wa chama kimoja. Sasa, ujio wa vyama vingi uliwapa fursa ambayo waliiona kama fursa ya dhahabu.

Ni hivi: Wakati wa chama kimoja, kwa kutumia nadharia ya ubishani ndani ya chama, iliwezekana kuwa na kundi la wabunge wa chama tawala linaloipinga serikali katika masuala kadhaa na likavumiliwa, kwa sababu tulikuwa tumekumbatia nadharia ya demokrasi katika chama kimoja. Kundi la wabunge kama hao walionekana kama wanaotoa mchango muhimu katika kuifanya serikali ifanye kazi yake, na kwa maana hii lilikuwa ni kundi la upinzani usio rasmi.

Lakini baada ya kuingia katika “vyama vingi” kazi hiyo ya upinzani ilikabidhiwa rasmi kwa vyama vya upinzani, na kwa hiyo wabunge wa CCM walikuwa hawana tena nafasi ya kusimama bungeni na kukosoa serikali, hata kwa jambo ambalo hata kipofu angeona kwamba ni hovyo. Wakuu wa chama walisikika wakisema (katika kipindi cha maandalizi ya ujio wa “vyama vingi”) wakituambia baadhi yetu:

“Sasa tutawaona. Vyama vingi vinakuja, na huo ndio mwisho wenu. Ukisema fyoo dhidi ya serikali yako unapigwa ‘whip’ hata tatu. Mtakoma.”

Kwa maneno mengine nao pia walikuwa wamegundua ile sheria yangu ya matokeo yasiyotarajiwa: Kwamba lile wingu la “vyama vingi” (ambalo liliwatisha mno) lilikuwa na msitari wa fedha: Tofauti na walivyokuwa wakihofu (kwamba mfumo wa vyama vingi vingeleta demokrasia) sasa wakawa wamegundua kwamba mfumo huo ungesaidia kuua hata kale ka-demokrasia kalikokuwa kamejengeka ndani ya mfumo wa chama kimoja. Na hili wakalifanyia kazi kwa ari kubwa ili kuhakikisha kwamba “vyama vingi” maana yake ni kutokuwa na demokrasia

Walikosea sana.

Itaendelea

Raia Mwema ( Jenerali Ulimwengu)

Marekani kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa Tanzania

Marekani ina mpago wa kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa Tanzania, yanayolenga kuwajengea uwezo wa kufanya biashara na nchi hiyo kupitia soko la Agoa.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Tim Cleacke amesema umuhimu wa kutoa mafunzo hayo unatokana na nia ya serikali ya nchi yake ya kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kukuza uchumi na kujikwamua na umaskini.

Alikuwa akizungumza na baadhi ya wafanyabiasha wa mkoa Arusha katika mkutano ulioandaliwa na chama cha wafanyabiashara wa mkoa huo TCCIA

John Malecela Ameanguka

John MalecelaAmeanguka
WAKATI mwanasiasa mkongwe na Waziri Mkuu wa zamani, John Malecela, ameangushwa katika kuwania kuongoza Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, mageuzi yamefanyika bungeni kwa kamati zote tatu zinazosimamia matumizi ya fedha za umma, kuongozwa na wabunge wa Upinzani.

Aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati mpya ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ni Mbunge wa Muleba Kaskazini, Wilson Masilingi aliyepata kura 13, akiwashinda Malecela (5) na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Anna Abdalah (3).


Kabla ya mwaka 2006, Malecela ambaye ni Mbunge wa Mtera (CCM), alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, ambayo sasa imeunganishwa na Kamati ya Mambo ya Nje, wakati Anna Abdalah, alikuwa akiongoza Kamati ya Mambo ya Njee
John Malecela
Kwa mujibu wa habari kutoka ofisi za Bunge, awali Masilingi alitajwa kuwania kuongoza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, akishindana na mke wa Malecela, Anne Kilango, ambaye ameshinda nafasi hiyo.


Haikuweza kufahamika mara moja sababu hasa ya Masilingi kuwania Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na kuachia Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, pamoja na kuwapo uvumi kwamba kulikua na makubaliano yasiyo rasmi kati yao.


Anne Kilango ambaye ni Mbunge wa Same Mashariki (CCM) amekuwa mwanamke mwenye kuheshimika ndani na nje ya Bunge kutokana na misimamo yake na alielezwa awali kuwa tishio katika kamati hiyo, jambo ambalo lilikuwa mtihani mkubwa kwa yeyote ambaye angeshindana naye.


Masilingi atasaidiwa na Mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Azan Zungu, wakati Anne Kilango, atasaidiwa na Mbunge wa Mafia (CCM), Abdulkarim Shah.


Kati ya kamati tatu zilizokwenda upinzani, kamati iliyokuwa na upinzani mkali ilikua ni Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POC) ambako, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, alimshinda Mbunge wa Wete (CUF), Mwadini Abbas Jecha, ambaye hakutarajiwa kabisa kuwania nafasi hiyo.

Zitto ambaye alipata kura tisa dhidi ya tatu za Jecha, ni Katibu wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni lakini alielezwa kupata upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya wabunge wa CCM waliokuwa wakimpigia kampeni Jecha.

Wabunge wengine wa upinzani walioshinda, kama ilivyotarajiwa, ni Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, aliyeshinda kuongoza Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, ambaye anaendelea kuongoza Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).



Zitto Kabwe


Kamati nyingine ambazo zimeendelea kuongozwa na wenyeviti wa awali ni pamoja na Kamati ya Fedha na Uchumi, inayoongozwa na Mbunge wa Handeni (CCM), Dk. Abdalah Kigoda na Kamati ya Miuondombinu, inayoongozwa na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.


Kamati mpya ya Nishati na Madini, imekabidhiwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara, Mbunge wa Bumbuli (CCM), William Shelukindo na aliyekuwa Makamu wake, Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harison Mwakyembe, wakiwa ni wabunge waliolivalia njuga sakata la umeme wa dharura la Richmond.


Kuundwa kwa kamati hiyo, kunaelezwa kutokana na kuibuka kwa mambo mengi yanayohusiana na nishati na madini na kukabidhiwa kwa Shelukindo na Dk. Mwakyembe kumeelezwa na wabunge kuwa ni mkakati mahususi wa Bunge kulimulika zaidi eneo hilo.


Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, inaendelea kuongozwa na Mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Lubeleje, akisaidiwa na Mbunge wa Chalinze (CCM), Ramadhani Maneno.


Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Abdisalaam Issa Khatib, ameombwa na wabunge wenzake wachache waliohudhuria kikao cha kwanza kuongoza kamati ya Viwanda na Biashara akisaidiwa na Mbunge wa Mkinga (CCM), Mbaruk Mwandoro. Wajumbe wengi wa kamati hiyo wakiwamo mawaziri wa zamani na wabunge mashuhuri hawakufika kwenye uchaguzi huo.


Kamati mpya ya Mambo ya Ukimwi, imekabidhiwa kwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Lediana Mng’ong’o akisaidiwa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, aneyeshughulikia Maafa na Kampeni dhidi ya Ukimwi, Dk. Luka Siyame.


Mbunge wa Ileje (CCM), Gideon Cheyo, ameendelea kuwa Mwenyekiti katika kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, ambayo sasa imefanyiwa marekebisho, akisaidiwa na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Kidawa Salehe.
Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, inaongozwa na Mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai, ambaye awali alikuwa akiongoza kamati hiyo ikiwa inahusika na Maliasili na Mazingira pekee.
Lediana Mng’ong’o
Atasaidiwa na Mbunge wa Koani (CCM), Haroub Masoud wakati Kamati ya Sheria Ndogo, itaongozwa na Mbunge wa Kibakwe (CCM), George Simbachawene.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, anaendelea kuwa Mbunge wa Peramiho (CCM), Jenista Mhagama akisaidiwa na Mbunge wa Koani (CCM), Haroub Masoud, ambaye naye anarejea katika wadhifa wake wa awali.



Kwa hisani ya Raia Mwema.

Tuesday, March 11, 2008

JOHN Nolan, yule raia wa Ireland aliyejaribu kuighilibu Serikali ya Tanzania imruhusu aanzishe mashamba ya kamba (prawns) ambayo yangeiharibu kabisa Delta ya Rufiji, alipata kuliambia gazeti moja la Uingereza kwamba kati ya nchi za "ajabu" alizopata kuishi ni Tanzania .

Nolan aliliambia gazeti hilo ya kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee duniani ambayo Mzungu anaweza kuingia akiwa na dola tano tu mfukoni na akaondoka miaka mitano baadaye akiwa milionea! Alitoa mfano wa yeye mwenyewe kwamba aliingia Tanzania akiwa hana kitu, lakini 'akatengeneza pesa' akiwa katika chumba chake cha hoteli kutokana na dili walizochonga na viongozi ambao walimwamini kwa kuwa tu ni Mzungu!Lakini Nolan si mgeni pekee aliyepata kuikejeli Tanzania .

Mwaka jana gazeti la Mtanzania lilipata kumnukuu mwekezaji mmoja kutoka China , anayefanya biashara ya kuuza kamba na kambakochi Mashariki ya Mbali, akiikejeli Tanzania kwamba rushwa yake ni "poa".

Kwa mujibu wa Mchina huyo, ni katika Tanzania tu ambapo unaweza kumwita hakimu nyumbani kwako na kumpa rushwa ya Sh. 100,000 tu, na kisha kumpa maelekezo ya namna ya kutoa hukumu ya kesi ya mamilioni ya pesa inayokuhusu!Lakini kama utashangaa na kutoziamini kauli hizo za Nolan na za Mchina huyo, utasemaje kuhusu hii ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kuanzisha kampuni yake ya biashara (ANBEM) yeye na mkewe, mwaka 1999, akiwa bado Ikulu?. Kwa kufanya hivyo, Mkapa akawa Rais wa kwanza katika historia ya Tanzania kufanya biashara akiwa Ikulu. Historia bwana, nani hapendi kuweka historia ya ujasiriamali?Lakini hakuishia hapo.

Mwaka mmoja kabla ya kuondoka madarakani; yaani Desemba 29, 2004, Mkapa huyo huyo akashirikiana na aliyekuwa Waziri wake wa Fedha na baadaye Nishati na Madini, Daniel Yona, kusajili kampuni nyingine binafsi iitwayo Tanpower Resources Company, na akaisimamia kununua asilimia 85 ya uliokuwa mradi wa umma wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya.Lakini pia hakuishia hapo.

Akautumia wadhifa wake wa urais kuhakikisha kampuni yake hiyo mpya – wakurugenzi wakiwa ni pamoja na mkewe na mtoto wake, kuingia mkataba wa kuiuzia Tanesco megawati 200 za umeme katika gridi ya taifa.Raia wema waliohoji iwapo hakuna mgongano wa maslahi kwa Rais kufanya biashara akiwa bado Ikulu; huku akinunua kampuni ya umma (Kiwira) na kuingia mkataba wa kibiashara na kampuni nyingine ya umma (Tanesco), walinyamazishwa haraka kwa kuambiwa Mkapa ni "mjasiriamali" , na kwamba anaonyesha "ujasiriamali" kwa vitendo akiwa Ikulu! Upo hapo?

Saturday, March 1, 2008

Wakimbizi wa Katumba kuanza kurejeshwa makwao Machi 9

Zoezi la kuwarejesha wakimbizi wa makambi ya Katumba na Mishamo wilayani Mpanda, mkoani Rukwa nchini mwao litaanza rasmi Machi 9, hadi Novemba, Mwaka huu.

Mgeni rasmi katika zoezi hilo anatarajiwa kuwa Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

Hayo yamo katika taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Bw. Thobias Mazanzala, kwa Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda, katika ziara yake ya siku tatu wilayani Mpanda.

Aidha zoezi la kutoa uraia litaanza mara moja baada ya uzinduzi wa urejeshaji kuanza ambapo muda ulipangwa kwa wakimbizi wa makazi ya Katumba kurejea nchini Burundi ni Machi hadi Novemba mwaka huu ambapo kwa wakimbizi wa makazi ya Katumba ni Machi hadi Julai.

Bw. Mazanzala alifafanua kuwa kwa wakimbizi waishio katika makambi ya Katumba wamepewa muda mrefu wa kuondoka kutokana na uwingi wa waliojiandikisha.

Alisema kuwa makazi ya wakimbizi ya Katumba yana watu 109,243 ambapo makazi ya Mishamo yana wakimbizi 56,251 na zoezi la maandalizi la kuwasajili wakimbizi wote wanaotaka kurejea burundi na wanaotaka kubaki Tanzania na kuomba uraia lilifanywa kwa ushirikiano wa UNHCR na serikali ya Tanzania na ya Burundi.

Alifafanua kuwa jumla ya familia 23,527 za makazi ya katumba yenye wakimbizi 108,925 waliosajiriwa ambapo wakimbizi 35,000 sawa na asilimia 35 ndio waliokubali kurejea nchini kwao kwa hiari na asilima 3 kutochagua chochote.

Alisema kuwa katika makazi ya Mishamo jumla ya wakimbizi 1500 kati ya 56,251 ndio waliokubali kurejea nchini kwao kwa hiari.

SOURCE: Nipashe

Nidhamu ndio silaha yetu

Nidhamu ndio silaha yetu


kiongozi wa kundi la Ze Comedy Isaya Mwakilasa almaarufu kama Wakuvwanga amedai kua nidhamu ndio silaha yao kubwa inayowafanya wadumu hadi leoAkiongea na darhotwire Wakuvwanga ambaye anafahamika kama waziri mkuu aliyejiuzuru au Mama beleee alisema nidhamu ndo silaha ya kundi lao kuwepo hadi leoKumekuwa na udaku wa mara kwa mara unavumishwa kama sie tumesambaratika kutokana na didhamu yetu hilo itakuwa ngumu..


Tofauti yetu na wachekeshaji wengine ni hiyo tu nidhamu na wote kujiona level moja hakuna super star wote ni wamoja na ndio maana kiapokuwepo mwnzetu mmoja nasisi wote tu...alisema WakuvwangaNa walidokeza kinachowapa kiburi cha kuwaigiza watu ni kutokana na kuwa na uhakika na wanachoigiza na ushahidi wa vithibitisho na kuzingatia kuelimisha na kukosoa pamoja na kuburudisha kwa watati mmojaMsomaji wa safu hii endelea kuzuru ukurasa huu ili upate makala za viumbe hawa hivi karibuni.


safari hii ni mavazi ya ngozi


safari hii ni mavazi ya ngozi
Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, mwaka huu inatarajiwa kupambwa na mavazi ya ngozi za mbuzi, magome ya miti na magunia kutoka kwa mwanamitindo Fatuma Amour. Akiongea na Darhotwire , mbunifu huyo alisema sherehe hizo zitafanyika katika ukumbi wa Movenpick jijini na kaulimbiu yake ni ‘heshima kwa akina mama’.


Aidha, alisema hafla hiyo pia itatumika kuwaburudisha watu watakaofika kwa lengo la kutuliza nyoyo zao, huku wakibadilishana mawazo na kufahamishana mambo mbalimbali. Alisema, ili kutoa burudani ya heshima na kuhakikisha siku hiyo inakuwa ya kupendeza, kutakuwapo na bidhaa kama mikoba na malapa vilivyobuniwa katika mtindo wa kiutamaduni. Alisema, vikundi vya burudani vitakavyotumbuiza siku hiyo ni Unique Sisters na kikundi cha sanaa cha Saidi Comorien. Mwaka jana tulisherehekea siku hii kuambiwa tubebe vikapu na tuachane na mifuko ya karatasi ili tuweze tunza mazingira...mwaka huu ni mwenzo wa ngozi Hallow!!


Kasi ya maambukizi ya ukimwi katika maeneo ya Feri jijini inazidi kuongezeka

Kasi ya maambukizi ya ukimwi katika maeneo ya Feri jijini Dar es Salaam inazidi kuongezeka kutokana na kushamiri kwa vitendo vya ukahaba na matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana.

Hayo yamebanishwa na mratibu wa mafunzo kuhusu udhibiti wa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi Bibi Elina Nachibona. Awali akifungua mafunzo hayo, naibu Meya wa manispaa ya Ilala Mohamed Yakoub amesema kampeni ya elimu ya ukimwi itaendeshwa katika kata zote za manispaa ya Iala na kuwapatia waathirika dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.

SOURCE: ITV

Bilioni 50/- zarejeshwa 2008-03-01 09:01:31 Na Mwandishi Wetu

Zaidi ya Sh. bilioni 50 kati ya bilioni 133 zilizochotwa na mafisadi kupitia akaunti ya madeni ya nje ya Benki Kuu (BoT) zimerudishwa serikalini.

Pamoja na fedha hizo, mali nyingine za watuhumiwa hao zilizoko nje na ndani ya nchi zikiwemo nyumba zimegundulika kwa mujibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Bw. Mustapha Mkulo.

Bw. Mkulo alitaja kiwango hicho kwenye mkutano wa waandishi wa habari, uliofanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Timu ya Maofisa wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) na kushirikisha maofisa kadhaa wa wizara hiyo na BoT.

Waziri aliyekuwa anajibu maswali ya waandishi wa habari alisema mali hizo zimenaswa katika kipindi cha mwezi mmoja na lengo ni kurudisha fedha zote, kukamata mali za watuhumiwa na kuwachukulia hatua za kisheria.

Alipoombwa kutaja majina ya wahusika na kampuni zao Bw. Mkulo alisema kwa sasa si wakati muafaka kwani kutavuruga upelelezi na jitihada za kurudisha fedha hizo na kuwafikisha mbele ya sheria watuhumiwa.

Tume iliyogundua mali hizo ni ile iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete , mwezi uliopita inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika na wajumbe wengine kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kwa kushirikiana na Bodi ya Wakurugenzi wa BoT.

Tume hiyo imepewa kazi ya kurudisha mali na fedha za watuhumiwa na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.

Makampuni 22 yaliyotuhumiwa kulipwa Sh. bilioni 133 na BoT kinyume cha sheria katika kipindi cha 2005/06 kupitia akaunti ya EPA ni pamoja na Bencon, VB & Associates, Bina Resorts, Venus Hotel, Njake Hotels and Tours, Maltan Mining Companies, Money Planners &Consultants.

Mengine ni Bora Hotels and Apartments, BV Holdings , Ndovu Soap, Navy Cuts Tobacco, Changanyikeni Residential Complex, Kagoda Agricultre, G&T International, Excellent Services, Mibale Farm, Liquidity Service, Clayton Marketing, M/S Rastash, Maregesi Law Chamber (Advocates), Kiloloma & Brothers, Karnel Ltd.

Makampuni hayo yalilipwa baada ya kuwasilisha vielelezo vya kughushi, hati batili na baadhi hayakuwa na nyaraka zozote na kwa ujumla hayakustahili kulipwa chochote.

Makampuni hayo yaliibuliwa na kampuni ya Ernst & Young ya Uingereza iliyopewa zabuni na serikali kuchunguza madai ya upotevu wa mabilioni ndani ya BoT kupitia akaunti ya madeni ya nje (EPA).

Katika mkutano huo, Waziri Mkulo, alisema majadiliano kati ya serikali na maofisa wa IMF yalilenga kwenye usimamizi na utunzaji wa fedha. `

`Tumezungumzia hali ya uchumi na kuazimia kuweka mkazo katika kukuza uchumi katika kiwango cha juu na cha chini.`` ``

Kadhalika tumeazimia kuboresha na kusimamia ipasavyo ukusanyaji mapato ili kuliondosha taifa na utegemezi na umaskini,`` alisema.

Alisema pamoja na hayo serikali imeazimia kuimarisha sekta ya nishati mijini na vijijini ili kuondoa matatizo yasiyokwisha ya nishati.

Waziri alisema mazungumzo hayo yaliazimia pia kuwa lazima Tanzania izingatie utawala bora unaofuata sheria.


SOURCE: Nipashe