Monday, May 26, 2008

Maswali Bungeni 26/5/2008

1. Kwa kuwa ni muda mrefu sasa ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi Kambi ya Finya, umesimama na kwa kuwa nyumba za makazi ya polisi zilizopo police line Wete ni mbovu sana, zimechakaa na zinavuja mno wakati wa mvua hali ambayo inasababisha usumbufu mkubwa na kuhatarisha usalama kwa familia zinazoishi humo na kwa kuwa polisi wengi na hasa wa vyeo vya chini wana ari ya kujenga nyumba binafsi za kuishi lakini kipato chao ni kidogo:-

(a) Je, Serikali itamalizia lini ujenzi wa nyumba za polisi Kambi ya Finya?

(b) Je, ni lini Serikali itazifanyia matengenezo nyumba za Police Line ili ziwe na hali nzuri?

(c) Je, Serikali haiwezi kuwasiliana na taasisi za fedha nchini ili polisi wapatiwe mikopo ya kujenga nyumba zao za binafsi?

bonyeza hapa kwa- majibu

2. Kwa kuwa, Wananchi wa Mji wa Mererani wanajishughulisha na biashara na uchimbaji wa madini ya Tanzanite, lakini wamekuwa wakipata taabu ya barabara kati ya Mererani na KIA; na kwa kuwa Rais wa Awamu ya Tatu na Awamu ya Nne walipoiona hali hiyo ngumu waliahidi kujenga barabara hiyo isiyozidi kilomita 20 kwa kiwango cha lami:- Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kujenga barabara hiyo muhimu sana kiuchumi, kutimzia ahadi zilizotolewa na Ma-Rais hao.

Jibu kutoka kwa Mh. Celina Ompeshi Kombani REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT

NAIBU WAZIRI alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, napenda kujibu Swali la Mheshimiwa Chrisopher Ole-Sendeka Mbunge wa Simanjiro kama ifuatavyo. Majibu


3. Kwa kuwa Serikali ina mikakati mizuri ya kuwawezesha wananchi hususan wanawake kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwapatia mikopo ya kufanyia biashara ndogo ndogo; na kwa kuwa Mkoa mpya wa Manyara una matatizo mengi makubwa ya mazingira ya kufanyia biashara hizo ikiwa ni pamoja na elimu ya ufahamu, kero za maji, uhaba wa Zahanati kwa baadhi ya vijiji na kutokuwepo na hospitali ya Mkoa.

(a) Je, Serikali ina mipango gani ya upendeleo kwa Mkoa wa Manyara ya kuboresha Mazingira chini ya Mpango wa MKUMBITA?

(b) Je, Serikali itafikisha lini mradi wa SELF Mkoani Manyara ikizingatiwa kuwa hakuna taasisi za fedha zinazofikisha huduma huko zaidi ya SACCOS zilizoanza hivi karibuni?

Jibu kutoka kwa Mh. Dr. Batilda Salha Burian PLANNING, ECONOMY AND EMPOWERMENT

NAIBU WAZIRI alijibu: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Martha Umbulla, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- Majibu

Maswali na Majibu Bungeni 26/5/2008

Swali

Kwa kuwa muda mrefu sasa, wananchi waishio Londrosi West Kilimanjaro katika Wilaya ya Siha, wamekuwa wakitaabika kutokana na ubovu wa barabara itokayo Ngare Nairobi Londrosi Gate; na kwa kuwa ubovu huo unakwamisha shughuli za kiuchumi hasa kwa upande wa watalii wanaotaka kupanda Mlima Kilimanjaro:-



(a) Je, ni Mamlaka gani inayotakiwa kushughulikia barabara hiyo?



(b) Je, ni hatua gani zinachukuliwa na Serikali kurekebisha hali hiyo?


ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION
Answer From Hon. Dr. Milton Makongoro Mahanga INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Aggrey D. J. Mwanri, Mbunge wa Siha, lenye sehemu (a) na (b), kwa pamoja kama ifuatavyo:-


Mheshimiwa Spika, barabara ya Ngare Nairobi - Londrosi Gate inashughulikiwa na Mamlaka mbili tofauti; sehemu ya Ngare Nairobi hadi Simba Farm yenye urefu wa kilomita 1.5 kwa upande moja ambayo ni barabara ya Mkoa (Sanyajuu – Kimwanga) iko chini ya uangalizi wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Kilimanjaro na kwa upande mwingine, barabara itokayo Simba Farm – Londrosi Gate yenye urefu wa kilomita 10, iko chini ya uangalizi wa KINAPA na kampuni ya West Kilimanjaro.


Bonyeza hapa - Muendelezo wa majibu

JK aenda japani leo:

Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka nchini leo jioni (25 Mei, 0 kuelekea Japan kuhudhuria mkutano wa nne unaohusu maendeleo ya Afrika, ujulikanao kama Tokyo International Conference on African Development (TICAD) utakaofanyika katika jiji la Yokohama.

Kabla ya kuhudhuria mkutano huo, Rais Kikwete atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Yasuo Fukuda, tarehe 27 Mei, 08 kuzungumzia mahusiano na ushirikiano wa nchi mbili hizi katika maswala ya kiuchumi na kidiplomasia na pia kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Kikwete anatarajiwa kumweleza mwenyeji wake juu ya maendeleo na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika na kujadili utatuzi wake.

Japan ni mshirika mkubwa wa maendeleo ya Tanzania ambapo Japan ni moja ya nchi zinazoisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuchangia katika bajeti na pia imechangia katika misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula, barabara na maji.

Mkutano wa nne wa TICAD utaanza tarehe 28-30 Mei, ambapo viongozi wote wa bara la Afrika wamealikwa kuhudhuria pamoja na viongozi wa Japan, wakuu wa mashirika mbalimbali ya kimataifa duniani kama vile Umoja wa Mataifa, mashirika ya fedha duniani, taasisi sizizo za kiserikali kutoka bara la Asia na Afrika, nchi rafiki na wenza katika maendeleo duniani.

Mbali na mkutano wa TICAD Rais pia atashiriki mikutano na makongamano mbalimbali yanayohusu uchumi, miundo mbinu, maendeleo na maswala mbalimbali yanayohusu utunzaji wa mazingira barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Aidha Rais Kikwete ataongoza mkutano utakaojadili tatizo la chakula duniani ambapo atazungumzia swala hili kwa kina hususan katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo barani Afrika na hatimaye atashiriki katika kupitisha azimio la Yokohama.

Rais pia anatarajia kutumia nafasi hiyo kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Afrika watakaohudhuria mkutano huo.

Rais atafuatana na

  1. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Benard Membe,
  2. Waziri wa Fedha - Mhe. Mustapha Mkulo,
  3. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Zanzibar - Mhe. Haroun Suleiman,
  4. Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko - Mhe. Cyril Chami
  5. na Mbunge wa Muleba Kusini
  6. na Mwenyekiti wa Kamati Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama - Mhe. Wilson Masilingi.

Rais anatarajiwa kurejea Dar-es-Salaam tarehe 31 Mei, 2008.

Imetolewa na Ikulu-Dar-es-salaam25.05.08

Wednesday, May 21, 2008

Balali ameaga dunia


Jamani kama Mungu anatusamehe kila inapoitwa leo naomba na sisi tumsamehe aliyekuwa Governor wa BOT (David Balali)


Mzee Daudi Balali (pichani) amefariki, (soma Jamii Forums) na mazishi yake yatakuwa Washington D.C. hapa Marekani!


Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema poponi Ameni.

Tuesday, May 20, 2008

Lipo tatizo la msingi ambalo sisi kama Watanzania au Waafrika tumegoma kabisa kulipa mjadala wa kina. Tunaogopa kabisa kuligusa kwa sababu ambazo kimsingi nilikwishazijadili huko nyuma.

Tatizo ni kwamba nchi hii haina misingi ya kile inachokiamini kwa dhati ambacho watu wake wanaweza kukipigania hata kama watakufa wakiwa wanakipigania. Msingi mkuu sasa hivi ni pesa. Kila mtu anapigania tumbo lake na la watoto wake.

Na kutokana na mlolongo wa matukio, na pia ukweli nilioueleza hapo juu ninaweza kabisa kuvaa joho la Sheikh Yahya Hussein na kutabiri kwa hakika kwamba kabla mwaka huu au kipindi hiki cha kwanza cha Rais Kikwete hakijafika ukingoni basi kutakuwa kumetokea mabadiliko zaidi katika Serikali.

Bonyeza hapa

Kweli Tanzania Haina Amani? (Hebu kuweni wakweli jamani)



Tanzania tuna Amani jamani.

Unajua ukiongelea ishu ya UFISADI Dunia nzima ni mafisadi na tanzania tunaichukulia mzaha mzaha ndio maana ishu inakwenda inarudi na tanzania tatizo sisi ni masikini ndio maana tuna pigana na Vijisenti alafu na wanoiba wanaiba nyingi kwa wakati mmoja badala ya kuiba kidogo kidogo.


Mna lolote la kuchangia wadau?

Hoja hiyo Mezani................................Kazi kwenu



Wananchi Africa Kusini waua Wageni Nchini Mwao





MMalawi akiokolewa na Polisi!


Leo kuna habari ya fujo zilizotokea huko Afrika Kusini. Wanasema kuwa wananchi wenye hasira wanaua wageni/wahamiaji kutoka nchi zingine amboa wako kwao. Mpaka sasa watu 22 wameuliwa. Kisa eti ni chanzo cha wao kukosa kazi! Wengi ya waliouliwa wanatoka nchi za kiafrika kama Zimbabwe, Mozambique na Malawi.

Wageni huko wanakimbilia vituo vya polisi na makanisani kuomba hifadhi kusudi wasiuliwe.Hivi Afrika Kusini imelaaniwa nini? Watu ni wepesi kusahau. Miaka mingapi Tanzania na nchi nyingi za dunia ziliwasaidia waAfrika Kusini mpaka walivyopata Uhuru wao.


Mnakumbuka Mwalimu Nyerere alivyozuia timu ya Olympiki ya Tanzania kushiriki katika michezo kwa vile Wazungu kutoka Afrika Kusini walikuwa wanashiriki wakati weusi huko wananyanyaswa na Apartheid? Mnakumbuka Dakawa na Mzimbo huko Morogoro? Na tusisahau hao WaSouth Africa walioacha mbegu Bongo!Hebu tukumbuke ni MSouth Africa aliyesababisha ajali iliyotoa roho mpendwa Waziri Mkuu wetu, Edward Moringe Sokoine! Na yule jamaa yuko wapi?

Je, ni moja wa hao wanaotaka kuona waBongo huko wanauliwa!Askofu Desmond Tutu amewaomba waache kuua watoto wa watu waliowasaidia kutoka kwenye mikono ya Apartheid. Ni aibu!



BBC Yaongeza muda

BBC Yaongeza muda kwa vijana wafanyabiasharaTarehe ya mwisho ya kuwasilisha michanganuo sasa ni Ijumaa Mei 23.

Vinaja wanaowania kushiriki katika shindano la Faidika na BBC sasa wana muda zaidi hadi Ijumaa Mei 23 kuwasislisha michanganuo yao.

Vijana wenye umri kati ya miaka 16 hadi 24 wana wiki moja zaidi ya kuwaslisha mchanganuo unakaonufaisha jamii yao kwa kutumia zawadi yenye thamani ya dola Elfu Tano za Marekani.

Mchanganuo usizidi maneno 1,500,
lugha ni Kiswahili.

Unaweza kusikia maelezo zaidi ya jinsi ya kuandika mchanganuo bora katika matangazo ya Dira ya Dunia kila siku kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC na pia kwenye mtandao wetu bbcswahili.com.

Salim Kikeke, Meneja Mradi wa Fadika na BBC 2008, amesema “ Vijana wametuambia wanahitaji muda zaidi kufanyia kazi kile ambacho huenda kikabadili kabisa maisha yao, ndio maana tumeamua kuongeza wiki moja katika tarehe ya mwisho ya kupokea michanganuo”.

Michanganuo inaweza kutumwa kwa njia ya:
E-Mail kwa: faidika@bbc.co.uk,
au kutumwa kwa njia ya posta katika ofisi zetu za kanda.
Faidika na BBC 2008,
Building Maison de la Bible,
Avenue de la Mission,
2eme etage,
En face de PAR,
Bujumbura.

Tanzania
Faidika na BBC 2008,
Jengo la PPF,
Ghorofa ya 8,
Barabara ya Sokoine na Morogoro,
P O Box 79545, Dar es Salaam.

Uganda
Faidika na BBC 2008,
1A, Ruth Towers,Plot 15A,
Clement Hill Road,
P O Box 7620, Kampala.

Michuano ya kitaifa itafanyika kama ifuatavyo: Burundi, Jumatatu Juni 2; Rwanda na DRC, Jumanne Juni 3; Tanzania, Jumatano, Juni 4; Kenya, Ahamisi Juni 5, na Uganda Ijumaa Juni 6.

Washindi sita kutoka katika michuano ya kitaifa, watapambana kuwania zawadi ya kwanza, katika fainali itakayofanyika Uganda, Jumatano Juni 18. Fainali itatangazwa moja kwa moja kupitia Idhaa ya Kiswahili ya BBC na pia kwenye mtandao, katika bbcswahili.com

UFISADI: Viongozi wameiweka CCM kwenye Auto-Pilot?



WENGI wetu tunafahamu kwamba ndege kubwa ya abiria inayosafiri masafa marefu, mathalan London hadi New York, kuna wakati rubani hutegesha mitambo ili ijiendeshe yenyewe (Automatic Pilot).

Kwa kawaida rubani na msaidizi wake hufanya hivyo ili nao wapate nafasi ya kunyoosha miguu, kunywa kahawa au hata kwenda maliwatoni.

Lakini si kila safari unaweza kuiweka ndege katika Auto-Pilot. Ni shurti safari iwe ya masafa marefu.

Aidha, ndege haiwezi kuwekwa Auto-Pilot kabla rubani hajaielekeza mambo fulani fulani; kama vile kule anakotaka ielekee, iende kasi gani na iruke umbali gani kutoka usawa wa bahari.

Kwa habari zaidi bonyeza hapa

Tsvangirai afuta mpango wa kurudi Zimbabwe kutokana na njama ya kutaka kumuuwa.



Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai.

Hofu za njama ya mauaji dhidi ya kiongozi wa upinzani Zimbabwe imechelewesha kurudi kwake nchini humo kulikokuwa kukisubiriwa kabla ya marudio ya uchaguzi dhidi ya Rais Robert Mugabe hapo tarehe 27 mwezi wa Juni.

Baada ya kuwepo nje kwa zaidi ya mwezi mmoja Morgan Tsvangirai alikuwa akitarajiwa kurudi nyumbani leo hii lakini amebadili mipango dakika ya mwisho baada ya kudokezwa juu ya jaribio la kutaka kumuuwa.

Msemaji wa kiongozi huyo George Sibotshiwe amesema wamepokea habari kutoka duru za kuaminika asubuhi hii ya kuwepo kwa mpango wa kumuuwa Tsvangirai. Msemaji huyo anasema kwa hivi sasa hawawezi kusema iwapo mpango huo umeungwa mkono na serikali na habari hizo tayari wamezifikisha kwa wakuu wengine wa nchi na kwamba ni jambo la uhakika kusema kuna ni tishio zito dhidi ya maisha yake na wanaamini kutokana na ushauri wa wanausalama wao isingelikuwa jambo la busara kwa Tsvangirai kwenda Zimbabwe leo hii.

Tsvangirai ambaye mwishoni mwa juma lililopita alisema angelirudi Zimbabwe hivi karibuni alitowa madai kadhaa ya kutaka kuhakikishwa maradio ya uchaguzi huo yanakuwa huru na wa haki ikiwa ni pamoja na kupelekwa nchini humo kwa wanajeshi wa kulinda amani wa kigeni na waangalizi wa uchaguzi.
Mohamed Dahman

Whose hands it's in....

As you see now, it depends whose hands it's in. So put your concerns, your worries, your fears, your hopes, your dreams, your families and your relationships in God's hands because... It depends whose hands it's in.

This message is now in YOUR hands.


What will YOU do with it?



It Depends on WHOSE Hands it's in!

Monday, May 19, 2008

VIJANA MNATUPELEKA WAPI?

Leo katika pita pita zangu nilinasa sehemu Fulani katika foleni eneo la ilala , tulikaa pale kwa muda mrefu kidogo karibu dakika 20 , magari hayaendi huku au kule , pembeni yetu kulikuwa na vijana wamepanda nyuma ya pick up , mbele yao wakina mama wako katika basi wanaenda katika msiba .

Ghafla hawa vijana wakaanza kuimba Nambari wani eehh nambari wani ni CCM , si mnaona sasa , mikanga yenu mliyopewa hiyo wakati ule ? angalia sasa hii ndio barabara waliyoahidi , rudisheni mikanga yenu hii ndio CCM iliyowapa mikanga hiyo mkawachagua .

Wale wakina mama hawakuwa na jibu lolote , lakini walikuwa wanaogopa sana manake vijana walikuwa na hasira walikaribia mpaka kushuka katika gari walilopanda wao waende kwa wale wakina mama waliovaa zile kanga .

Hawa ni mfano wa vijana ambao kwa siku za karibuni wameonekana kulaumu chama cha mapinduzi na serikali kwa ujumla wakiona chochote mbele yao , nilitaka kuwauliza hivi ccm inahusika nini na mkandarasi aliyejenga barabara hiyo ? au ccm ndio walikagua barabara hiyo kabla yaijakabidhiwa ? yote hayo ni maswali ambayo nilitaka kuuliza .

Ni sawa na wale vijana wengine waliotiwa nguvuni kwa tuhuma za kumzomea raisi mstaafu Benjamin William mkapa kwa sababu zao binafsi , au sijui hawa vijana wanalipwa au wanapewa kitu gani mpaka wanakuwa na ujasiri wa kudhalilisha wenzao kiasi hicho .

Tabia hizi kwa kweli zinauzi na kukatisha tamaa sana , kama vijana wa leo ambao tunategemea wawe mstari wa mbele katika kujenga jamii bora zinazoangalia mbele kuanza kuzomeana njiani , kuimba nyimbo za ajabu ajabu , kuandamana katika mavyuo na mashuleni sijui kuchoma moto na kufanya vurugu nyingine .

Kwa mtindo huu vijana wasitegemee kufika popote au kusikilizwa na mtu wowote , kama mawazo yao ni kuungwa mkono na vyama vya upinzani kama wale wananchi wa tabata dampo basi watafute mengine na kama kuzomea huku , au kuimba nyimbo za kashfa hizi zinafadhiliwa na upinzani au mtu wowote yule

Waelewe nyimbo hizo na aina nyingine zozote za vitu wanavyofanya ni kuvunja sheria za jamhuri ya muugano wa Tanzania , na sheria ina mkono mrefu itakufuata popote ulipo na kukufikisha katika vyombo husika ili uweze kujibu tuhuma zinazokukabili

Vijana sasa wafanye mengine kuna mengi ya kufanya zaidi ya kuzomea , kuimba nyimbo za kashfa , kuchoma moto shule , kufanya fujo mashuleni na sehemu zingine .

Ni ushauri kutoka kwa kaka Yona Maro

UFISADI NHIF

Jamani wadau nasikia kuna ufisadi ndani ya NHIF,

  1. Mgongano wa Kimaslahi na “Hongo” kwa viongozi wa Bodi na Wizara ya Afya
  2. Kupindisha taratibu maksudi kwa maslahi Binafsi
  3. Ufujaji wa fedha
  4. Huduma Mbovu za Mfuko
  5. Dharau na Mienendo isiyokubalika katika jamii
Je mnalolote la kuongelea juu ya huu UFISADI

Wednesday, May 14, 2008

KANUNI YA BUNGE INAYOMPA NGUVU MWANANCHI (JAPO HAITUMIKI)

Hapa chini nakuleteeni nukuu ya kanuni moja ya Bunge kama ilivyowasilishwa na Dkt. Wilbroad Slaa, hivi majuzi (Mei 2, 2008) kwenye mdahalo wa ulingo wa maendeleo hapa mjini Arusha.

Kanuni ya 34 ya Kanuni za Bunge inatoa nafasi adimu sana ambayo katika Bunge letu haijawahi kutumika tangu uhuru kwa vile si Wabunge au Wananchi wanaoielewa vizuri kanuni hii. Kanuni hii inatamka ifuatavyo, Mbunge yeyote anaweza kuwasilisha Bungeni maombi kuhusu jambo lolote kwa niaba ya watu wanaotoa ombi hilo Ombi la aina hii linachukua nafasi kubwa Bungeni, na linachukua nafasi precedence kuliko hata shughuli za Serikali. Matakwa pekee ni kuwa lazima liwe limewekewa saini na Wananchi (Wasiopungua 200) wenye kutaka ombi hilo liwasilishwe, na mbunge asiwe na maslahi yoyote na ombi hilo yeye mwenyewe. Hii ni nafasi muhimu sana, kama ingeliweza kutumika. Inahitaji uelewa mkubwa, ujasiri wa wananchi na wananchi kutokuwa na uwoga katika kutafuta na kudai haki zao.

Je, hapo hapawezi kuwa mahali pa kuingilia ikizingatiwa hii ni kanuni ya Bunge, si ya chama chochote? Je tuendelee kungoja utashi wa wabunge kuwasilisha hoja binafsi? Je inatosha wananchi waendelee kuwalaumu wabunge kwamba hawasikilizi kero zao?

Dkt. Slaa anasema, Inahitaji uelewa mkubwa.
Nani atawajengea uelewa mkubwa wananchi? Mimi nimekutumia wewe mbiu hii (bila kujali iwapo unajua au la), ni vema ukiimuvuzisha zaidiĆ¢.